Mahusiano dini tofauti, kipi ni sahihi cha kufanya?

SPSS

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
711
388
Wasalaam wana bodi,

Naomba kupata ufafanuzi wenu juu ya suala hili kua kwa mfano umekutana na binti wa dini tofauti,wazazi wake ni watu wadini sana lakin na wewe pia wazazi wako wana dini means kwa wao kuridhia wewe kubadil dini ni kitendo ambacho hawataweza kamwe kukiruhusu.

So kutoka mwanzo mlilifahamu hili na mkaamua kuanza mdogo mdogo imefikia mahali mnaona kuna umuhimu wakulizungumzia,baada ya mazungumzo ya muda unagundua binti (mara nying mwanamke ndie anaemfuata mwanaume linapokuja suala la dini tofauti) hawezi kukubali kubadili dini (ingawa msimamo wake sio imara sana isipokua anaamini wazazi wake kamwe hawawezi kumruhusu) na wewe hauwezi kufunga ndoa ya bomani

What will be the best option kuachana au ku-hold on until it gest worse.
 
Swala la dini tofauti ni changamoto sana katika mahusiano. Kuna jirani yetu kijana alikuwa na rafiki wa kike mwarabu wazazi wamegoma dada kubadili dini na kijana kagoma mwisho wa siku wana watoto 3 mdada anatamani sana kubadili hata maisha anayoishi yamebadilika kuna wakati anakwenda hata kanisani. Mwisho wa siku wamefunga ndoa ya serikali. Maisha yanaendelea
 
Swala la dini tofauti ni changamoto sana katika mahusiano. Kuna jirani yetu kijana alikuwa na rafiki wa kike mwarabu wazazi wamegoma dada kubadili dini na kijana kagoma mwisho wa siku wana watoto 3 mdada anatamani sana kubadili hata maisha anayoishi yamebadilika kuna wakati anakwenda hata kanisani. Mwisho wa siku wamefunga ndoa ya serikali. Maisha yanaendelea
so its true it never works
 
Mzee wangu ni mristo wife muislam tena swala tano-mtoto wa kizenji!

Wameoana ni wana miaka 28 kwenye ndoa na hawajawahi nyooshean hata kidole na maisha yanasona
oooh is see...naona kma kuna commitment inawezekana aisee
 
Inatakiwa kabla ya kuwa deep in love muwe mmefikia muafaka wa dini zenu ili msije mkaanza kulialia baadae,mnasubiri hadi mpeane mimba ndo mnaanza kuzungumzia dini, nonesense, zungumzeni mapema from the first date.
 
Mm yalishanikuta hayo mambo ya dini nayajua vizuri yanavyoumiza moyo, siku hizi kabla sijamtongoza demu namuuliza jina nikishajua dini yake tofauti na yangu nabadili gia angani sitaki tena ijirudie
 
Dunia hii itakuwa mahali Pema sana pa kuishi Siku hizi dini mbili za kimagumshi zikifutwa na dini nyingine kama Buddha's ziachwe tu hazina madhala.
 
Back
Top Bottom