Mahojiano yangu na JamboLeo

Mahojiano yangu na JamboLeo

Zitto,

Mimi nakuaminia sana, lakini katika kukujenga... nakuomba ujirekebishe kwenye haya.

1. Punguza umimi, unao sana mkuu, mfano hii interview haikuwa lazima uilete wewe.

2. Punguza kuona wengine wajinga, hii mara nyingi umetukana wazee wenye heshima zao Bungeni, tumia lugha laini lakini ujumbe ufike... Nyerere alikuwa akimtusi Mwinyi lakini kwa lugha ya kiutu uzima.

3. Munkari, sio kila jambo linahitaji majibu, jifunze kutoka kwa Mzee John Samuel Malecela. Usiwe kama Mh. Sitta.

Mwisho nakukubali sana mzee endeleza libene.
Kasheshe,

Namnukuu Zitto:

ndugu zangu, ninawaomba radhi niweke mahojiano yangu haya na gazeti la jambo leo katika uwanja wetu. Humo kuna kauli yangu rasmi kuhusu mijadala inayoendelea. Baada ya muda naomba mod akusanye hizi thread nyingi zinazomhusu zitto na kuziweka pamoja. Nadhani kwenye ile thread ya rev. Kishoka.

......

nawaomba radhi tena kwa kuweka hii interview. Nadhani ni muhimu wakati huu. Naelewa kuna zitto sana, mniwie radhi kwa hili langu mwenyewe!

Sasa Zitto kama mwanachama wa JF sidhani kama kakosea, ni kwakuwa alikuwa na access ya information hizi sisi hatuna, kutushirikisha nadhani hajakosea. Tena, katumia lugha ya kiungwana sana...!

Aidha, sipendi kumsemea kuhusiana na ushauri mwingine lakini nadhani atakuwa kakusoma.
 
lakini mh.zitto naomba unijibu haya yafuatayo

je, ni kweli kampeni zako za kugombea uenyekiti wa chadema zilikuwa zinafadhiliwa ni fisadi nimrod mkono?
- Sio kweli.

ni nini msimamo wako kuhusu wezi wa fedha za EPA? hasa mwizi rostam azizi ambaye inasemekana wewe ni best wako? mbiona sijakusikia ikikemea hili?
- Nimesema sana kuhusu EPA na nimetoa nyaraka nyingi sana kuhusu EPA kwa watu na viongozi wenzangu wanaosema pia kuhusu EPA. Kwangu mimi KAGODA ni CCM kama chama na sio mtu mmoja ambao tumeaminishwa. Nimsema hapa JF toka mwaka 2008, kwamba KAGODA ni CCM! executors wa plan ni suala lingine. Nikutonye tu, i met Balali. I spoke to Balali before he died. If we want to address KAGODA once and for all we have to tackle it holistically. Wabunge wote wa CCM walipata fedha za KAGODA kwenye kampeni zao. I asked for a special audit of CCM campaign funds by CAG to CCM denial. However, i made ammendment to Political Parties bill on party finances and for the future CAG will have the power to audit books of accounts of political parties.

Kwamba sisemi kuhusu EPA ni uongo mtupu. Sio tu nimesema bali nimekuwa source ya nyaraka confidential kuhusu Wizi huu mkubwa sana kuwahi kutokea katika Taifa letu.

Ninaendelea kusema na kutafiti zaidi kuhusu MEREMETA na nimeorder special audit kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge on MEREMETA.

Rostam Aziz? What do you want me say about him?

Weka wazi, je utagombea ubunge Kigoma au hata hapa Dsm? Isije ikawa hii mbinu ya kukimbilia kusoma ni kukimbia harakati in the holy name of mafisadi.
- I better don't respond to this.

je? huoni kuwa huu si wakati wa kukimbia uwanja wa mapambano?
- This as well. Sina majibu

Naamini nimekujibu ndugu yangu
 
Mh. Zitto, hongera kwa mafanikio na pole kwa kukatishwa tamaa mara nyingi

1. Naomba kujua vipi nafasi ya vijna ndani ya vyama vyetu yote vya siasa Tanzania? Maana kwa haraka haraka naona vijana wengi hawako kwenye siasa na hii ni hatari sana, Ukiondoka let say ukaenda kwenye academic. Kuna vijana uliowatayarisha personally, ambao una hakika watafika mbali katika siasa za nchi zeu hizi, au unataka kufanya kosa la Nyerere la kutokutuachia kiongozi yeyote anayefanana na yeye?

2. Je ni rahisi kwa vijana wa kitanzania kutimiza ndoto zao katika vyama vya siasa nchini, lets say I am dreaming to be president katika nchi hii, unafikiri ni rahisi kupenya katika vyama hivi?

3. Kila mtu anajua hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA na mara nyingi unasema hali ni shwari, ni kama vile unajikaza kuwa ndani ya hicho chama, unavumilia, kukejeliwa, majungu, n.k Hivi siyo kuwa hali hii imekufanya ubadili mawazo na kuelekeza kwenye academic? (I assume) au ulikuwa na mawazo haya tangu zamani? Naogopa!!

4. Sijajua utajibu vipi swali la 3, ila kama yalikuwa mawazo yako tangu awali, basi you need to 'make' people like you. Lakini kama ni mawazo yamekuja after hali za kisiasa ndani ya vyama vyetu basi, naogopa kusema kama watu strong kama wewe mnakimbia huko, nani ataenda?

Vijana wa kitanzania hasa wasomi wengi, mawazo yao ni kuwa wenyeviti wa kamati za harusi. Something is wrong na ukiwa mkweli wa maswali hayo hapo juu utaokoa wengi au uta-enlighten watu wajue tatizo tulilo nalo. Hatuwezi kulia mabadiliko mabadiliko wakati misingi yake haipo. ''Afadhali ni mwenyekiti wa vikao vya harusi 10, nitakuwa appreciated kuliko kwenda kwenye siasa na kuwa frustrated'' wanasema hivi vijana graduated form our universities!

5. Msingi upi ambao Tanzani umeukosa ambao kwayo leo hii tumefika hapa? na vyama vya upinzani vimejua hilo tatizo na kulitatua kwa kiasi gani??

asante
 
Naamini nimekujibu ndugu yangu
Lovely, kaka wewe uko tofauti sana na wanasiasa wetu Bongo, walau unaweza kukabiliana na maswali na kujitahidi kuyajibu...

Uko tofauti sana! Bravo for this
 
Mh Zitto

Ulikuwa unahojiwa au uliandika maswali mwenyewe, ukajijibu halafu ukawapelekea hao Jamboleo? Maana ukiacha swali la kwanza kuhusu hali ya kisiasa nchini, labda na lile la ukabila CHADEMA mengine yooote ni too personal.

Kama ulihojiwa basi naona ni ile hali ya waandishi wetu kuwa na focus ndogo, hasa wakilenga mtu na sio masuala ya kitaifa.

Kama kijana wa kitanzania ninayeona mengi yakitokea nchini na yanayotaka serious attention yetu, kujua na kujadili who your role model is naona ni kupoteza muda

All in all, you seem to be good writer

Ni hayo tuu
 
Lovely, kaka wewe uko tofauti sana na wanasiasa wetu Bongo, walau unaweza kukabiliana na maswali na kujitahidi kuyajibu...

Uko tofauti sana! Bravo for this

Umeona Mkuu, na hata majibu yaliyonyooka tu huwa ni shida sana kwa wanasiasa wetu wa Bongo ( I wish ningemvuta huyu jamaa CCM ila ndio hivyo tena amekula yamini... kidding)
 
je? huoni kuwa huu si wakati wa kukimbia uwanja wa mapambano?

1. Ni kwa namna gani wanakuwa supported ili wasikimbie mapambano?

2. Ni wanasiasa wangapi walioacha upinzani wakarudi makazini? uliwauliza au Zito amekufumbua macho?

3. Je umeshawahi kushiriki katika siasa za nchi hii hata kwa kupiga kura tu, kutoa michango ama kuhudhuria mikutano ya siasa?

4. Ikiwa swali la 1 na 3 hujajibu swali lako lina kuwa nullified!
 
Safi sana wewe umeweza kuzungumzia watu maarufu na Mh. wetu Rais K. Hongera kwa hili hasa ukitaja hivi taja kwa majina hao mafisadi unawachukia kwani wanajulikana au sema Mafisadi PAPA sisi tunawajua Big UP wewe SIASA unaiweza sio Ualimu hapo utakuwa upo wrong. Big UP.
 
Samahani Mh. hapo juu niliuliza hili gazeti Jamboleo linamilikiwa nani sikujibiwa.

Naomba kama ukipata muda kama ungetuelezea kuhusu Mh. Spika na changamoto Bungeni (Speed & Standard) kwenye hiki kipindi chake, jinsi anavyoliendesha Bunge je unakubaliana kuwa amefanya mageuzi makubwa mpaka hapa kulikofikiwa ni kwa kujivunia na wewe ukiwa mmojawapo wa wabunge?? je kuhusu mtikisiko Bungeni kwenye Richmond mpaka serikali kupelekea kutotimiza maazimio 23 ya kamati?? na TAKUKURU?? wewe hii unaionaje
 
Samahani Mh. hapo juu niliuliza hili gazeti Jamboleo linamilikiwa nani sikujibiwa.

Naomba kama ukipata muda kama ungetuelezea kuhusu Mh. Spika na changamoto Bungeni (Speed & Standard) kwenye hiki kipindi chake, jinsi anavyoliendesha Bunge je unakubaliana kuwa amefanya mageuzi makubwa mpaka hapa kulikofikiwa ni kwa kujivunia na wewe ukiwa mmojawapo wa wabunge?? je kuhusu mtikisiko Bungeni kwenye Richmond mpaka serikali kupelekea kutotimiza maazimio 23 ya kamati?? na TAKUKURU?? wewe hii unaionaje


Jambo leo ni gazeti linahusiana na LOWASSA kwani lilianzishwa na fedha za TANAPA , kama mnakumbuka jarida moja la TANAPA lililokuwa na picha ya LOWASSA -Anayebisha aje hapa aseme .

Hata Zitto anajua kwani yeye ni mwenyekiti wa mashirika na miongoni mwa mashirika ni TANAPA na hata kwenye vikao vya kamati hili suala la Tanapa kutumia zaidi ya bilioni 1 kwa ajili ya jarida lilihojiwa.
 
Naomba kuuliza, hili gazeti la JamboLeo linamilikiwa na nani, linatoka lini na wapi?? kwani sijawahi kulinunua na kulisoma.


Jambo Leo ni mali ya Juma Pinto , katokea wapi hadi ana gazeti ni siri na move za kisiasa . Ulizia zaidi utajua Nchi ina maajabu na ni sehemu kubwa mwandishi na mpambe wa CCM na hasa JK .Chanzo chake London .
 
-
Kwangu mimi KAGODA ni CCM kama chama na sio mtu mmoja ambao tumeaminishwa. Nimsema hapa JF toka mwaka 2008, kwamba KAGODA ni CCM! executors wa plan ni suala lingine. Nikutonye tu, i met Balali. I spoke to Balali before he died. If we want to address KAGODA once and for all we have to tackle it holistically. Wabunge wote wa CCM walipata fedha za KAGODA kwenye kampeni zao. I asked for a special audit of CCM campaign funds by CAG to CCM denial. However, i made ammendment to Political Parties bill on party finances and for the future CAG will have the power to audit books of accounts of political parties.

Naamini nimekujibu ndugu yangu

Mmesikia nyie mlioweka pamba masikioni?

Wabunge woteeee wa CCM walilamba pesa. Hapa hakuna WAPIGANAJI wala WASIOPIGANA. Sophia Simba na HOSEA sasa naanza kuamini kuwa wanayosema ni kweli kuwa "CCM WOTE SI WASAFI".

Sasa aje mtu hapa anasema eti Sitta, Selleli, Nkumba, Mwakyembe, Malecela, Kilango na sijui nani ni WASAFI. Wote ni akina MAKONGORO MAHANGA tu kwa njia moja au nyingine.

Kwa wale mnapanga kugombea ubunge kama Masanilo, Mwakalinga, John Mashaka na wengineo, hii ni pointi ya kuanzia.

generation-Y: Mbona unarusha shutuma kwamba Zitto alijichagulia maswali rahisi? Kama una swali gumu sana si umuulize? Ndiyo bahati kwamba Zitto tunaye hapa na twaweza kumlima madongo.

ZITTO: Pamoja na madongo yote haya, bado unakuja na kujianika wazi na ile duara ya kulengea shabaha unajibandika - Nakupa hongera. Lazima nikiri kuwa kama UJASIRI basi unao maana kwa wengi tunakuwa tumepata sehemu ya kulengea mashambulizi kwa wabunge wetu, ingawa wewe ni moja ya 300 na kitu ya wabunge wote na unatoka UPINZANI.
 
Hivi kupitisha miswaada na sheria za Ruzuku na Madini Bungeni ndiyo ajenda waliyokupa Wapiga kura wa Kigoma Kaskazini hadi uchukulie kama mafaniko makubwa ya ubunge wako hailiwiadi sasa? Siyo tu Miswaada na Sheria haviliwi, kwa Tanzania ni kama kazi bure kwani hakuna anayefuata au kuheshimu haswa vikiwa kwenye "abstract level" kwa mtu wa kawaida kama ishu za Madini na Ruzuku. Watu tungekuelewa kama ungetaja kliniki ngapi, madarasa mangapi, mabomba ya maji na visima vingapi, barabara kilomita ngapi, nk umefanikisha tangu uwe Mbunge.
 
Kwa wale mnapanga kugombea ubunge kama Masanilo, Mwakalinga, John Mashaka na wengineo, hii ni pointi ya kuanzia.

Sikuwa na habari kama huyu yupo mbioni, na wewe sikonge karibu kwetu Chabutwa jimbo halina mtu hili.
 
Sasa aje mtu hapa anasema eti Sitta, Selleli, Nkumba, Mwakyembe, Malecela, Kilango na sijui nani ni WASAFI. Wote ni akina MAKONGORO MAHANGA tu kwa njia moja au nyingine.
Ishu ni kwamba walijua zimetoka kwa Kagoda? maana hiyo ilikua ni siri sana!!
 
Mmesikia nyie mlioweka pamba masikioni?

generation-Y: Mbona unarusha shutuma kwamba Zitto alijichagulia maswali rahisi? Kama una swali gumu sana si umuulize? Ndiyo bahati kwamba Zitto tunaye hapa na twaweza kumlima madongo.

Sio shutuma mkuu ni maoni tu, na sikusema maswali ni rahisi, nimesema ni too personal. Sasa forum hii ikiwa kila siku inajadili vitu vidogovidogo tena personal kama hivi....i dont know

Halafu sio kwamba hua simuulizi, namuuliza sana, ila huwa hajibu

Unajua tena forum hii ina mwenyewe, sie kama wadandiaji tu. So mtu mpaka aone ni comment ya Mwanakijiji au sijui nani ndo ajibu

by the way, nashukuru kwa observation yako
 
Sikuwa na habari kama huyu yupo mbioni, na wewe sikonge karibu kwetu Chabutwa jimbo halina mtu hili.

Mkuu,
Chabutwa siyo jimbo. Kama Chabutwa kungelikuwa ni jimbo, basi nisingeenda kugombea kule maana hapo kuna familia ya Yongolo, ni wazito sana pale na wapo siku nyingi huku baba yao/kaka yao akiwa mwalimu wa sehemu hiyo na kufundisha watu wengi sana ambao leo ndiyo wapiga kura.


Chabutwa ni kata kama sikosei kwenye wilaya/jimbo la Sikonge. Hivyo hata nikisema nigombee, sanasana Sikonge. Kugombea siwezi maana mie na siasa ni mbalimbali. Siwezi kukubali NIDANGANYE watu hivihivi kweupe. Itabidi nijifunze kuvuta bangi ili nivae miwani (wanyamwezi wanasema kuondoa nishai).

Masanilo amepanga kugombea huko kwao Usukumani na kampeni zinaenda undergound sana kiasi kwamba hadi leo watu wanapata taarifana kula kiapo cha kutafuta member wengine kimya kimya bila kutoa siri....
 
Tunashukuru kwa mahojiano wengine siasa sasa inaanza kutukimbia
 
Back
Top Bottom