Mahojiano yangu na JamboLeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahojiano yangu na JamboLeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zitto, Nov 16, 2009.

 1. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu, ninawaomba radhi niweke mahojiano yangu haya na gazeti la Jambo Leo katika uwanja wetu. Humo kuna kauli yangu rasmi kuhusu mijadala inayoendelea. Baada ya muda naomba mod akusanye hizi thread nyingi zinazomhusu Zitto na kuziweka pamoja. Nadhani kwenye ile thread ya Rev. Kishoka.

  Pili, unazungumziaje mustakabali wa siasa nchini, ukilinganisha na nchi nyingine za bara la Afrika.

  Unasemaje kuhusu hali ya kisiasa nchini?

  Hali ya kisiasa ya Tanzania kwa hivi sasa ni tete sana. Utulivu tuliozoea katika tasnia ya siasa umetoka kufuatia vyama vya siasa kuonekana kuwa na makundi makundi. Kama unavyojua kuwa CCM inashikilia kwa nguvu sana siasa za nchi kiasi kwamba inakuwa ni vigumu kutofautisha CCM na Dola. Hii ni kutokana na CCM kuwa na idadi kubwa ya wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

  Hali ni hiyo hiyo katika serikali za mitaa. Hivyo mgogoro woowte ndani ya CCM unaonekana kama mgogoro wa Taifa. Hali hii itaondoka pale tu vyama vingine vya upinzani vitakapoweza kuongeza idadi ya wabunge na kumali ukiritimba wa CCM katika siasa za nchi. Vyama vya upinzani navyo vinaonesha kutetereka. Kumekuwa na fikra kuwa kuna mgogoro ndani ya chama changu cha CHADEMA na hivyo kutia wasiwasi wananchi.

  Ninataka kuwahakikishia wananchi kuwa hakuna mgogoro CHADEMA na wasiwe na hofu.

  Unaonekana kuwa na msimamo sana na jasiri katika hoja mbalimbali unazozitoa hasa bungeni naimani ndio zilizokujengea umaarufu mpaka sasa, tofauti na wanasiasa wengine huogopi hali hiyo inaweza kukuondoa katika wadhifa wako mapema?

  Mimi sina hofu hata kidogo. Maisha yangu yote nimekuwa mtu ninayesimamia haki na kutetea wanyonge. Mimi huwa sionei mtu na ninaposema jambo ninakuwa nimelifanyia utafiti wa kutosha na sifanyi ili kukomoa watu binafsi. Hivyo yeyote ambaye atanichukia kwa kazi yangu atakuwa amependa tu kunichukia maana mimi sina chuki na mtu. Nilipoamua kuwa mbunge niliamua kutekeleza ajenda maalumu ya kutetea rasilimali za nchi yetu na kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma.

  Pia niliazimia kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unasaidia kuongeza ubora wa maisha ya wananchi. Kazi ambayo nimeifanya kwa ufanisi sana. Nimekuwa mbunge kwa miaka 4 tu lakini kazi niliyofanya ni kana kwamba nimekuwa mbunge kwa miaka 10 au zaidi. Kazi yangu imefahamika kwa wananchi kuliko wabunge wengi ambao wamekuwa bungeni kabla yangu.

  Nimeifanya ajenda ya madini iwe ya kitaifa na hata kupelekea Rais kuunda kamati ambayo imetoa taarifa nzuri sana na sasa sheria mpya ya madini imetungwa na kusubiri kupitishwa Bungeni. Niliandika mabadaliiko ya sheria ili mahesabu ya vyama vya siasa yakaguliwe na CAG na sheria tayari imepita. Hii itadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma katika vyama vya siasa.

  Toka mwaka 2006 Bunge limepitisha bajeti ya ruzuku kwa vyama ya zaidi ya shilingi 67 bilioni lakini fedha zote hizi zilikuwa hazikaguliwi na CAG. Kuanzia mwaka huu wa fedha zitakaguliwa. Hii ni kazi ya kujivunia sana na siamini kama kna mtu atanichukia kwa kazi hii.

  Ni ujasiri wako unatokana na nini?

  Ujasiri? Sidhani kama ni sahihi kusema Zitto ni jasiri au mimi mwenyewe kujisema kuwa mimi ni jasiri. Ninatimiza wajibu wangu. Nimekuwa nikifanya hivi kila mahali nilipopewa majukumu ya kuongoza.

  Kama nilivyosema hapo awali kuwa mimi nachukizwa ninapoona mtu anaonewa. Vilevile ninakasirika ninaoopona mtu anatumia madaraka yake kwa faida yake bianfsi. Misingi ya utu ndio inanipa ujasiri kama nina ujasiri. Kusimamia ukweli ndio kunanipa nguvu ya kufanya kazi zangu. Watu niliosoma nao chuo kikuu wanafahamu hili kwamba siku zote nimekuwa mtu wa haki.

  Ulitaka kugombea u-enyekiti Chadema baadae ukajitoa huoni msimamo wako umeanza kulegalega na nini malengo yako ndani ya chama kwa nafasi yako?

  Nilitaka kugombea uenyekiti wa chama changu kwa kuwa nilikuwa nina sababu za kugombea. Nilijitoa kwa kuwa niliombwa kujitoa na Wazee wa chama.

  Sasa kama gharama ya kukubali ushauri wa wazee ni kuonekana sina msimamo, gharama hizo nimeikubali. Lakini kumbuka kuwa kila chama kina utamaduni wake na utamaduni wa CHADEMA ni kuheshimu ushauri wa wazee wa chama.

  Chadema kinatuhumiwa chama cha kikabila (wachaga) wanawatenga baadhi ya makabila unampango wa kwenda CCM?

  - Kwamba CHADEMA ni chama cha kikabila ni propaganda tu za mahasimu wetu wa kisiasa. Chama cha kikabila hakiwezi kusajiliwa Tanzania maana ni kinyume cha sheria. CHADEMA ni chama cha kitaifa na kinakubaliaka zaidi maeneo yasiyo ya kilimanjaro kuliko kilimanjaro.

  Kwa mfano mkoa wa Kigoma ndio mkoa unaongoza sasa kwa kuwa na wenyeviti wengi wa vijiji na mitaa kutoka CHADEMA kuliko mkoa mwingine wowote ule. Hizi siasa za ukabila, udini nk ni siasa tu. CHADEMA ni chama cha kitaifa.

  - Kwamba nina mpango wa kuhamia CCM nazo ni propaganda. Sasa utakuwa ni mpango tena kama hata wewe mwandishi unaujua na kuuliza? Katika siasa kuna kitu kinaitwa imani.

  Mtaji wa mwanasiasa ni imani ambayo watu wanayo juu yake. Hivyo njia nyepesi sana ya kumharibia mwanasiasa ni kujenga hisia za kutoaminika. Hili ndilo ambalo mahasimu wangu wa kisiasa wanafanya - wa ndani na nje ya chama changu. Kueneza uongo na uzushi kuwa ninahamia CCM. Haya ni mawazo ya kipuuzi tu.

  Mimi sikuingia CHADEMA bahati mbaya. Nimeingia CHADEMA nikiwa na umri wa miaka 16 na nimekulia ndani ya chama changu miaka yote hii mpaka nimekuwa mbunge na kisha Naibu Katibu Mkuu. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa na sikuingia CHADEMA kwa kuwa nilikosa nafasi CCM au niligombana na watu fulani wa CCM. Mimi ni kizazi kipya kabisa cha wanasiasa ambao wamekulia ndani ya chama chake na upewa mamlaka. Nitakuwa mtu wa ajabu sana kuingia CCM...

  .... hao wanaoeneza kuwa mimi nitahamia CCM kwanza walikuwa CCM kabla, na pili wataenda CCM wataniacha mimi CHADEMA. CHADEMA kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni Movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa Taifa letu. Kijiji kwangu watu waliteswa kuijenga CHADEMA, watu walifungwa, vijana wenzangu walilala juu ya paa za nyumba ili kuijenga CHADEMA na toka hapo kijiji changu ch MWANDIGA hakijawahi kuwa na kiongozi wa CCM, toka mwaka 1994. Hao wanaosema mimi ntaenda CCM wajiulize wana historia gani na CHADEMA? Wana machungu gani na CHADEMA?

  Ni kiongozi gani ambaye anakuvutia na unafuata nyayo zake?

  DR. Salim Ahmed Salim - amekuwa role model wangu toka nikiwa mtoto mdogo kabisa.

  Nakumbuka sana, siku moja nilikuwa na mama yangu mbele ya nyumba yetu mara baada ya Sokoine kufariki. Mama alikuwa anazungumza na mmoja wa jirani zetu kuhusu nani atachukua nafasi ya Sokoine mwaka huo 1984. Mimi nikasema Salim..... mara akafoka kuniambia toka hapa unaingilia mazungumzo ya wakubwa! Akawa Salim... sikumbuki kama mama anakumbuka kisa hiki.

  Nilikuwa darasa la kwanza shule ya msingi Kigoma. Salim alikuja Kigoma nikiwa darasa la pili na nikapanga mstari barabarani kwenda kumwona. Nilikuja kukutana na Salim uso kwa uso mwaka 2002 baada ya kurudi kutoka OAU wakati huo nikiwa Katibu Mkuu wa Pan Afirca Movement Tanzania, tulikwenda kumkaribisha nyumbani. Leo ninakutana naye mara kwa mara na kuchota mawazo! Hekima, uadilifu na uanadiplomasia na hasa mafanikio makubwa aliyoyapata katika siasa umekuwa ukinivutia sana kuhusu Dr. Salim.

  Lakini sio Salim peke yake, Jaji Joseph Warioba na wabunge wazee Dodoma kama Mzee Makwetta ni watu ambao ninavutiwa na uadilifu wao na mapenzi yao kwa nchi yetu. Uvumilivu wa kisiasa wa Rais Kikwete unanivutia sana na ninaufuatilia sana kama sifa moja ya kiongozi (tolerance). Ujasiri na uana mikakati wa Raila Odinga unanifanya nimfuatilie na kumwiga siasa zake.

  Nimemaliza kusoma Kitabu cha King Hussein wa Jordan! Alivyoweza kuilinda Jordan na kuwa Taifa lililosimama leo ni miujiza mikubwa sana. Kama mawazo yake yangesikilizwa na viongozi wenzake wa kiarabu leo tungekuwa na Taifa la Palestine. Thabo Mbeki's pragmatism is admirable and worth noting.....

  Nini matarajio yako ya baadaye?

  Ninatamani kuwa mwalimu wa chuo kikuu, kufundisha, kutafiti na kuandika vitabu. Nitakapoacha siasa, hii ndio kazi ambayo ningependa kufanya. Kufundisha.

  Kiongozi gani unamchukia kutokana na mfumo/msimamo wake?

  Kiongozi yeyote anayekandamiza watu wengine. Kiongozi yeyote asiyejali haki za watu wengine. Kiongozi yeyote anayetumia dhamana aliyopewa kuongoza kwa faida yake mwenyewe. Huyo ndiyo kiongozi ninayemchukia.

  Ulitaka kugombea nafasi ya m/kiti CHADEMA, je zilikuwa mbio za kuelekea ikulu 2010?

  Haya ndio mawazo ya watu ambayo nadhani wanakosea kabisa. Kwanza sio lazima mwenyekiti wa chama awe mgombea Urais. Pili, sina umri wa kugombea Urais mwaka 2010 wala mwaka 2015. Niligombea uenyekiti wa CHADEMA ili kujenga chadema kwa kuanzia pale ambapo mwenzangu amefikia.

  Ninaamini kabisa kuwa tunahitaji kubadili mikakati kukabiliana na CCM ili kushika dola. Ninaamini kabisa kuwa ndani ya miaka michache ijayo CHADEMA itashika dola.

  -------------------------------------------------

  Nawaomba radhi tena kwa kuweka hii interview. Nadhani ni muhimu wakati huu. Naelewa kuna Zitto sana, mniwie radhi kwa hili langu mwenyewe!
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Inspiring...the future is bright for this young politician
   
 3. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  gazeti la leo halikuandika hivyo waliandika tuu sehemu ya kuwa wewe huendi CCM na ndio ilikuwa headline ya gazeti.

  Kumbe ulizungumza mambo mengi ila wao waliifanya kama vile ulizungumzia tuu la kwenda CCM na kuacha kabisa kuandika hayo mengine.

  Struggle should continue.
   
 4. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii interview mhhh .... Natafuta jina kati ya soft ball na informercial?
   
 5. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha uongo wewe.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ok. Zitto, it seems to me, you are neutral and at the same time objective!!! Yah!! Examples za potential politicians, umezingatia sana Chama tawala na umepoint out important names, including the President!!! (tolerance!!!). I respect your opinion man!!!

  Kwa hapa I am a bit frustrated with politics!!! I am happy, that I am not a politician!!! Duu kali hii.
   
 7. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  umejibu maswali vizuri
  ujitahidi kuachana na maneno ya kwenye red
  labda ungesema nimekuwa mbunge kwa miaka 4 na nimejitahidi kufanya hivi na hivi na mafanikio ni haya na haya

  sidhani kama kazi ya miaka 10 inaweza kufanyika kwa miaka 4
  au labda ulitaka kusema umekuwa mmbunge kwa miaka 4 na kazi uliyoifanya umewapita wabunge walioka bungeni zaidi ya miaka 10
   
 8. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #8
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  I saw that.......... i had to put it as i responded (didnt want to edit)! Thanks for observation....
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  This is for those whose heads are reasoning well.
  Mkuu wewe unaona vipi,najuwa kwasababu si mpango wa kifisadi fisadi ndo maana unaona uwongo au...labda nyinyi mkiacha siasa mnakuwa wawekezaji...au?
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ma hardcore tunaweza kusema Zitto hakuwa steadfast enough kuwakandamiza mafisadi na CCM.
   
 11. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2009
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  "Nitakuwa mtu wa ajabu sana kuingia CCM......... hao wanaoeneza kuwa mimi nitahamia CCM kwanza walikuwa CCM kabla, na pili wataenda CCM wataniacha mimi CHADEMA. CHADEMA kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni Movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa Taifa letu".Nukuu ya Zitto Kabwe.

  Haya maneno nitayahifadhi sana ......
   
 12. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hujaelezea msimamo wako kwenye jambo moja muhimu sana, kuhusu maafisa waliovuliwa madaraka CHADEMA!?????
   
 13. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uvumilivu wa kisiasa wa Rais Kikwete unanivutia sana na ninaufuatilia sana kama sifa moja ya kiongozi (tolerance).

  kutokuchukua hatua unalichukulia kama uvumilivu wa kisiasa?
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Nov 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zitto,
  Mkuu wangu heshima mbele. Nashukuru sana umeweka vitu waazii na hasa kile kipande cha kugombea Urais ambcho umeeleza kile watu hawakufikiria kwanza kabla hawajabwabwaja.. Kweli kabisa huna UMRI wa kugom,bea Urais mwaka 2010 na hata 2015 iweje watuy hapa JF walikuja moto kwa shtuma zisizokuwa na msingi.
  Pili nakubaliana na Blueray, umekuwa mpole sana kwa CCM, hukuwavika kanzu wanalostahili hata kama una mvuto na JK ambaye ni rais wa Jamhuri kinyume cha mwenyekiti wa chama hicho.
  Mwisho, Una kila haki ya kueleza vitu ambavyo umeweza kukamilisha...Kujivunia mafanikio ni hatua moja kubwa sana ya kutomlalamikia Mungu..waache waseme watakaosema lakini the fact remains. Bravo!
   
 15. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  It is clear kwamba JK ametupa uwanja mpana sana wa uhuru, wakati mwingine ukijadili jambo lazima uweke mambo mengine constant au uweke scope, otherwise kila jambo liko linked na kitu kingine...

  Zitto nakuelewa unavyosema JK ana political tolerance ya hali ya juu sana, na kama asingekuwa nayo mwaka wa BOT/EPA, RICHMOND etc... Taifa lingewaka motto.
   
 16. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hi Zitto keep on and pullup your sox, our politics needs more that we have already done so, at least you young politicians you can go on the game with new ideas. The main objective should be to findout how to get an international support in order to pointout the things which our leader are not fair to our society and what make Tanzania in more than 40 years of independence still happy to be so called as a young nation this is a shame. We are at your back as you know politics is ambitions and given is not easy for everyone to do things you do even if they know number of things about dos and don'ts of our Nation.

  keep on, your nation will pay you in return when things are fine.
   
 17. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Mimi sikuingia CHADEMA bahati mbaya. Nimeingia CHADEMA nikiwa na umri wa miaka 16 na nimekulia ndani ya chama changu miaka yote hii mpaka nimekuwa mbunge na kisha Naibu Katibu Mkuu. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote cha siasa na sikuingia CHADEMA kwa kuwa nilikosa nafasi CCM au niligombana na watu fulani wa CCM. Mimi ni kizazi kipya kabisa cha wanasiasa ambao wamekulia ndani ya chama chake na upewa mamlaka."

  Then should we consider Chadema as a machinery for future leaders to our nation? If the answer is yes. then they should not think or invest on presidential post for now, effort and energy should be invested on the strategy of how to increasing the number of member of paliaments, immediately from next year. and most their candidates should be young generations. Mkinihakikishia kuwa mtapeleka vijana tu na helikopta zitawasaidia basi nami nitagombea ubunge.
   
 18. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huwa wanasiasa mara nyingi ni opportunist!!! Zitto ni mwanasiasa anayejijenga na natumai sifa hiyoo atakuwa nayooo..

  Kwa majina aliyotaja amezingatia pia heshima za watu hao katika jamii au kikundi na mwelekeo wake kisiasa.. Kumtaja Mh Mkuluu naona ni mbinu nzuri kwa mwanasiasa kijana kama zitto..

  Warioba bado sijamkubaliia sifa hizoo kwani wakati wa utawala wake (EX PM) hana historia ya kusonga mbelee...Salim kipimo chake cha uanadiplomasia kiko mizania ya juu pamoja na kwamba tofauti aliyoileta katika jamii wakati na baada ya utumishi wake haujakidhi haja ya hadhi yake!!!
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Asante sana Zitto, NI interview fupi, clear na strategic, mimi nina haya yafuatayo;

  • Kwanini ulkichagua Jamboleo na sio gazeti kama Tanzania Daima, au magazeti yenye coverage zaidi kama ya IPP, Mwananchi, na ya serikali?
  • Ukiwa kama one of the most potential guyz in our country kutuongoza siku zijazo, je kwanini tusifanye mahojiano humuhumu jamvini (sort of Q and A) kwa maeneo kadha wa kadha? Naamini hili litakupika vizuri sana na hata utaweza kupokea mawazo mazuri sana... [tutaomba mods wadelete posts za mabingwa wa kuharibu mijadala]

  Hongera

  MTM
   
 20. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kuuliza, hili gazeti la JamboLeo linamilikiwa na nani, linatoka lini na wapi?? kwani sijawahi kulinunua na kulisoma.
   
Loading...