Mahojiano yangu na JamboLeo

Mahojiano yangu na JamboLeo

Zito alisema,
Wabunge wote wa CCM walipata fedha za KAGODA kwenye kampeni zao
JokaKuu unafafanua,
..kama CCM walichota fedha za Kagoda na kuzitumbukiza kwenye kasma ya fedha za uchaguzi basi wabunge WOTE wa CCM wamechafuka.

JokaKuu kama ni kweli,nakubaliana nawe hasa ulipochagua kwa umakini kutumia neno wamechafuka. Kwa maana halisi ya kuchafuka, hakika tunaweza kusema kuwa Watanzania wote (wakiwemo mimi na wewe) wamechafuka, maana tumechafuliwa na kitendo cha mtu au watu wachache kutumia fedha za Umma kinyume na taratibu na sheria ziongozazo.

Hata hivyo ni bayana kuwa kuchafuliwa huko hakuwezi kuwa sawa na kusema Wabunge wa CCM wote au in this matter Watanzania wote tulipokea pesa hizo za kifisadi.

Unajua mara nyingi tunaposhindwa kusingle out clearly nani kafanya kosa gani kwa ushahidi usio mashaka ndipo tunapoteza hata namna ya kuwaajibisha wahusika wakosefu. Mfano huu uko wazi katika hukumu ya hivi karibuni iliyowaacha Watz wengi hoi pamoja na kwamba kweli raia wasio na hatia waliuawa. Unaona hapo tunaweza kusema kuwa Jeshi la Polisi lilichafuliwa (lilichafuka) kwa kitendo cha Askari / baadhi ya Askari wake lakini hatuwezi kusema kuwa Jeshi la Polisi lote kama Taasisi walihusika kuua.

Yaani tunawashauri na siyo kuwatisha Wabunge wetu kuwa makini wanapotuumu ili kauli zao zisiendelee kubaki kuwa kelele baada ya kutupwa nje kwa TKO ama kwa kukosea kueleza kosa lililotendwa au kuonyesha Mhusika / Wahusika au kwa kukosa kuwasilisha ushahidi mwanana.
 
Yah,it was a very good interview, but i think Zitto una tatizo moja, if you wont accept it and change, huna muda nrefu ktk ulimwengu wa siasa,wako wapo wengi tu ambao nadhani unawafaham, wakoo wapi now!!

Be carefull Zitto, sifa unazopambwa na vyombo vya habari vya watuhumiwa wa vita ambayo ulikuwa unaipgania (UFISADI) ambayo now sikusikii kabisa ukiipigania, inakushushia reputation yako especial mbele ya watu wanao think deep, hope unanisoma, its time now kwa wewe kuvishushua hivyo vyombo vya habari vinavyokupamba for nothing, otherwise utabakia midomoni mwa watu wa tabaka la chini sana as far as thinking capacity is concerned, utabakia midomoni mwa wajinga nchini na hao wanaokupamba watakaa pembeni na kukucheka,

Be carefull Zitto, sio siri, ume shake kwa kiasi kikubwa sana, sit down, settle jirudi, angukia wazee wa CHADEMA na watanzania wapendao mabadiliko nikiwa ni mmoja wao.
 
Asante Zitto Kabwe, na Hongera sana kwa kuja hapa na kutoa maelezo mazuri kama haya ambayo una historia ya kwako pekee yako
 
Sina neno sana na majibu yako, bali sikufurahishwa sana na aliyekuwa anakuuliza maswali, yaani mwandishi, alikufagilia sana kwa too manye leading questions hivyo kukupa mteremko.

Pia nampongeza mwandishi, lazima atakuwa ni mchanga kama gazeti lenyewe lakini huu ni mwanzo mzuri, hili gazeti siku za usoni litakuja kuwa kisu kama Tanzania daima, japo kisu chake sasa kinakwenda butu.

Nijukue na fursa hii kumpongeza Pinto na timu mzima ya Jambo leo bila kumsahau 'Mfadhili'

Mpiganaji Pasco, kile kipindi cha KITIMOTO kinaweza kurudi tena? Hivi nani alikuwa "mfadhili" wakati ule tuangalie kama anaweza akafadhili tena...
 
Yah,it was a very good interview, but i think Zitto una tatizo moja, if you wont accept it and change, huna muda nrefu ktk ulimwengu wa siasa,wako wapo wengi tu ambao nadhani unawafaham, wakoo wapi now!!

Be carefull Zitto, sifa unazopambwa na vyombo vya habari vya watuhumiwa wa vita ambayo ulikuwa unaipgania (UFISADI) ambayo now sikusikii kabisa ukiipigania, inakushushia reputation yako especial mbele ya watu wanao think deep, hope unanisoma, its time now kwa wewe kuvishushua hivyo vyombo vya habari vinavyokupamba for nothing, otherwise utabakia midomoni mwa watu wa tabaka la chini sana as far as thinking capacity is concerned, utabakia midomoni mwa wajinga nchini na hao wanaokupamba watakaa pembeni na kukucheka,

Be carefull Zitto, sio siri, ume shake kwa kiasi kikubwa sana, sit down, settle jirudi, angukia wazee wa CHADEMA na watanzania wapendao mabadiliko nikiwa ni mmoja wao.
Mkuu wangu hii sii kazi ya Zitto peke yake ni yetu sote inclunding viongozi wengine wa Chadema... Kina Mnyika, Slaa Mbowe hata huyo Rwakatale wako wapi? Leo hii siwasikii kabisa wakiuza sera, kupinga ufisadi kiasi kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wamechukua dhamana hiyo.

Zitto anachojaribu kufanya pengine ni MAKOSA ni hii tabia ya kujieleza sana kwa watu wasiohusu! Yeye anachotakiwa ni kujieleza (kama kuna hoja) ni kwa wadhamini wake wananchi wa Kigoma na chama chake...
Kwa Wadanganyika hata siku moja huwezi kuwa msafi kama hujaungama. Na sifa ama maana halisi ya kuungama ni kukubali na kutubu makosa, jambo ambalo sidhani kuna sababu ya kufanya hivyo ikiwa hujafanya makosa hayo na huendi kwa vyombo vinavyohusika...Ukweli siku zote hujitenga na uongo..
 
Zitto cha msingi ni kuangalia misingi ya chadema ni nini na utume wa chama kwa kizazi hiki.Migogoro ndani ya chama makini ni upotevu.nimesoma post zako nyingi na ukieleza mengi hadi kipato chako kinachohalalisha wewe kumiliki magari mazuri zaidi ya matano sasa sio sifa kulipwa laki tatu na hamsini kwa siku wakati mwalimu kwa mwezi hafiki huko na unaona sawa ni upotevu.Zitto nilikuamini sana lakini sasa mhh. kuna nja mnazo ndani ya chadema za kutatua matatizo ni bora mzifuate kuliko kuanikana kwenye JF.

Bado unaweza ukafanya vizuri katika siasa zetu hizi za bongo but you have to be real and usiendekeze makundi.

Kwa kusema ukweli kipatao cha mtu ni siri ya mtu binafsi hakuna mtu mwenye shida ya kujua unapatat shs ngapi... it is a sense of immaturity to share such information ooh nina hammer,prado moja la partner moja sijui nimempa nani .. sijui nini.. what for?
 
Zitto

You have inspired me so much!. Keep it up!.

Lakini jambo moja ambalo ninaliona Chadema itaangamizwa isipokuwa makini, ni kuungana na CUF na NCCR na TLP! Ninafurahi kwamba ile coalition ya vyama vinne ilibomoka!. Ile ilitaka kuua vuguvugu la mageuzi mlilolibeba ndani ya mioyo yenu. Vyama vingine vitatu (CUF, TLP na NCCR) havina proper direction, vinaigilizia, na vingine vimetawalia na siasa za kidini, eg CUF. Kwa mfano TLP wao wanasubiri matukio yaliyofanywa na wenzao ndipo Mh Lyatonga ainuke kutoa comments. Hawana hata maono ya kuamka na kuwafanya wananchi wahamasike kudai haki zao. Nadhani wanafikiri wata - win mass support wa kujiingiza tu katika kampeni za 2010. kinachowafanya CHADEMA mkubalike ni jithada zenu za kuwaelimisha wananchi hatapasipokuwa na kampeni za uchaguzi. Hiyo ni kazi kubwa, kuliko kusubiri chaguzi kama wafanyavyo TLP nk. Believe me TLP kwisha habari yake!.

Hongera pia kwa moyo wako wa unyenyekevu kumwachia Mbowe, kugombea uenyekiti na hatimaye kupitishwa. Ulizingatia maslahi ya chama na hata taifa. Usikimbilie kugombea Urais, ninyi mwachieni Mbowe kwa sasa, hali ninyi mkikamatisha na kupambisha moto bungeni. Bila shaka nitapata nafasi ya kukutana nawe soon. You have inspired me so much.

Best regards
 
... hao wanaoeneza kuwa mimi nitahamia CCM kwanza walikuwa CCM kabla, na pili wataenda CCM wataniacha mimi CHADEMA. CHADEMA kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni Movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa Taifa letu. Kijiji kwangu watu waliteswa kuijenga CHADEMA, watu walifungwa, vijana wenzangu walilala juu ya paa za nyumba ili kuijenga CHADEMA na toka hapo kijiji changu ch MWANDIGA hakijawahi kuwa na kiongozi wa CCM, toka mwaka 1994. Hao wanaosema mimi ntaenda CCM wajiulize wana historia gani na CHADEMA? Wana machungu gani na CHADEMA?

Mhe.Zitto hapo unataka kusema kuwa Dr.Slaa alikuwa CCM na hivyo atarejea nyumbani?
_Naunga mkono hoja labda wewe tu na CUF yako ndio hutaki kukubali; na kama Slaa ni target yako wala huko hayupo kabisa

Mhe.Zitto, ina maana wewe peke yako ndio una historia na CHADEMA?
-Wapo kibao ila yeye ni miongoni mwao
AMA ulikuwa unatuma ujumbe gani na ni historia gani hiyo?
_Du maswali mengine naona hata Zitto sijui kama ana haja ya kujibu-sio kila swali hujibiwa mheshimiwa

Ina maana wewe historia ya hao vijana wa kijijini kwako ndio ya kwako ama unamaanisha nini?mbona hukuenda na wewe kulazwa juu ya paa ? unajenga historia kwenye migongo ya watu?
-Du mmhh sina la kusema mwenye ubongo anataona this too l ow
Mhe.Zitto, ina maana wewe ndio una machungu na CHADEMA kuliko walioko huko ?
Yeye ni miongoni tu ndg wapo kibao wenye uchuungu na Chadema
Ina maana wengine hawana uchungu na ndioo maana kazi yao ni kuitafuna ruzuku ya chama , wakati wewe tuu ndio huitafuni?
_unaweza kuthibitisha mama/baba hili?
Mhe.Zitto, nitashukuru sana ukijibu maswali yangu kwani nimesoma hapo na kuona fumbo kubwa sana kuwa kumbe huko CHADEMA wapo wengye historia na wengine hawana historia, na nimejenga tafsiri kuwa ili uweze kuwa mwanachama na uweze kuzungumzia mambo ya chama ni lazima uwe na histori, na kama ulikuwa chama kingine basi ukija huko utakuwa kila siku unatazamwa kama mtu adui na ambaye kuna siku utarejea kwenye chama chako cha zamani, hivyo basi kwa sisi ambao tuko vyama vingine tusije?
-Matendo ndio yatakufanya usitazamwe la sivyo yes lazima uangaliwe; maana mamluki mbona wako wengi tu na hawastahili hata kidogo
 
_Naunga mkono hoja labda wewe tu na CUF yako ndio hutaki kukubali; na kama Slaa ni target yako wala huko hayupo kabisa

-Wapo kibao ila yeye ni miongoni mwao
_Du maswali mengine naona hata Zitto sijui kama ana haja ya kujibu-sio kila swali hujibiwa mheshimiwa

-Du mmhh sina la kusema mwenye ubongo anataona this too l ow
Yeye ni miongoni tu ndg wapo kibao wenye uchuungu na Chadema
_unaweza kuthibitisha mama/baba hili?
-Matendo ndio yatakufanya usitazamwe la sivyo yes lazima uangaliwe; maana mamluki mbona wako wengi tu na hawastahili hata kidogo

Wanaume wengine Bwana kwa kujipendekeza tuu hawajambo, hivi amekuteua kuwa msemaji wake hapa?

Kama ni mwananmke basi wewe hujachezwa ndio maana unakuwa mpashkuna hivyo.
 
Wanaume wengine Bwana kwa kujipendekeza tuu hawajambo, hivi amekuteua kuwa msemaji wake hapa?

Kama ni mwananmke basi wewe hujachezwa ndio maana unakuwa mpashkuna hivyo.
Maswali ya kitoto yanaudhi- au tuko ktk mipasho- watu tuko serious ukiongea ugoro pasu kwa pasu maana huna hoja- najua ni hasira ya kuambiwa ukweli uwe mstarabu- endeleza mipasho mtu wa mwambao- huna jipya hapo tafuta vitu vya maana
 
Uvumilivu wa kisiasa wa Rais Kikwete unanivutia sana na ninaufuatilia sana kama sifa moja ya kiongozi (tolerance).

Uvumilivu wa kutochukua hatua dhidi ya wezi na mafisadi?

Ujasiri na uana mikakati wa Raila Odinga unanifanya nimfuatilie na kumwiga siasa zake

Kukubali kuwa Waziri Mkuu kibaraka kwa kukubali serikali ya mseto wakati kapokonywa ushindi?

Thabo Mbeki's pragmatism is admirable and worth noting.....

This is a man who claimed that AIDS was not caused by HIV....you admire him?
 
Uvumilivu wa kutochukua hatua dhidi ya wezi na mafisadi?

Kukubali kuwa Waziri Mkuu kibaraka kwa kukubali serikali ya mseto wakati kapokonywa ushindi?

This is a man who claimed that AIDS was not caused by HIV....you admire him?

Kumbuka kuwa kwa kila jambo kuna advantages na disadvantage zake, hivyo Kijana kuwakubali hao viongozi kuna kitu ambacho unatakiwa uiangalie kwa uangalifu wa hali ya juu. Ndiyo kuna makosa waliyofanya hao katika siasa lakini kuna mambo ya kujifunza na kuyachukuwa kuwa yako na kuyamodify kuondoa mabaya yake. Mimi nakubaliana na huyu Kijana.
 
Zitto

You have inspired me so much!. Keep it up!.

Lakini jambo moja ambalo ninaliona Chadema itaangamizwa isipokuwa makini, ni kuungana na CUF na NCCR na TLP! Ninafurahi kwamba ile coalition ya vyama vinne ilibomoka!. Ile ilitaka kuua vuguvugu la mageuzi mlilolibeba ndani ya mioyo yenu. Vyama vingine vitatu (CUF, TLP na NCCR) havina proper direction, vinaigilizia, na vingine vimetawalia na siasa za kidini, eg CUF. Kwa mfano TLP wao wanasubiri matukio yaliyofanywa na wenzao ndipo Mh Lyatonga ainuke kutoa comments. Hawana hata maono ya kuamka na kuwafanya wananchi wahamasike kudai haki zao. Nadhani wanafikiri wata - win mass support wa kujiingiza tu katika kampeni za 2010. kinachowafanya CHADEMA mkubalike ni jithada zenu za kuwaelimisha wananchi hatapasipokuwa na kampeni za uchaguzi. Hiyo ni kazi kubwa, kuliko kusubiri chaguzi kama wafanyavyo TLP nk. Believe me TLP kwisha habari yake!.

Hongera pia kwa moyo wako wa unyenyekevu kumwachia Mbowe, kugombea uenyekiti na hatimaye kupitishwa. Ulizingatia maslahi ya chama na hata taifa. Usikimbilie kugombea Urais, ninyi mwachieni Mbowe kwa sasa, hali ninyi mkikamatisha na kupambisha moto bungeni. Bila shaka nitapata nafasi ya kukutana nawe soon. You have inspired me so much.

Best regards

DU....
 
"Nitakuwa mtu wa ajabu sana kuingia CCM......... hao wanaoeneza kuwa mimi nitahamia CCM kwanza walikuwa CCM kabla, na pili wataenda CCM wataniacha mimi CHADEMA. CHADEMA kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni Movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa Taifa letu".Nukuu ya Zitto Kabwe.

Haya maneno nitayahifadhi sana ......

TEHTEH! Lets wait and see, now its 2013.
 
Back
Top Bottom