Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,626
- 18,233
Una uhakika upi kuwa hao "Wakristo" hawakuwa Waislaam waliolazimishwa kubadilishwa majina na "mapdri" wa "kizungu"?
Unajuwa kuwa neno "Mzungu" kibantu lina maanisha "Mungu" au "aliyetoka kwa Mungu"?
Mkuu, Waislaam wa Bukoba sio wengi sana lakini nakuhakikishia ni wauumini wa Kislaam kweli kweli na walikuwa na mshikamano wa hali ya juu wakati huo mpaka sasa, katika mazigira kama hayo hakuna Padri au Askofu angeweza kuwa na ubavu wa kuwalazimisha Waislaam kubadilishwa majina yao - Waislaam mashuhuri wa wakati huo wakina Mzee Sued Kagasheki, Ali Migeyo (Ali Matata), Mzee Kachwamba na wengine wasingeruhusu kitu kama hicho kitokee, they were well highly organised, nilikuwa na baba yangu mdogo mwislaam kwa hiyo nilisimuliwa kila kitu mkuu; sorry my swahili is a bit rusty. Mkuu mimi ndio mara yangu ya kwanza kufahamu maana ya neno "MZUNGU" - thanks a lot
Umenikumbusha kisa kimoja: Bibi yangu mzaa baba alikuwa mkatoliki, J'pili moja alikwenda kusali Kanisa la Kashozi, alipo toka huko kaja nyumbani anasimulia kwamba Padri wa Kiholanzi aliwaonya kwamba MKOMUNIST ni shetani, kwa umri wangu wa kitoto nami niliamini hivyo ingawa mimi na Baba tulikuwa walutheri, niliogopa kumuhuliza mzee kuhusu hilo. Sasa baada ya kuwa mtu mzima nikawa najiuliza hivi kwa nini Mapadri Wazungu walikuwa wanawatisha wauumini wao kiasi hicho!! Je hizo zilikuwa agenda zao za siri za kupinga siasa za ukomunist/ujamaa, je walikuwa wanawambia mambo gani ya ziada ya kuwatisha kuhusu creed nyingine?