Mahojiano ya polisi na Sheikh Ponda Issa Ponda

Mahojiano ya polisi na Sheikh Ponda Issa Ponda

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
5,372
Reaction score
4,141
Asalaam Alaykum! Saa 4 asubuhi nilifika Central Police kusimamia mahojiano yake na Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO baada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10 kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni hawakumfanyia lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi.
Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:-
1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
i. kwanini waliandamana ii. nani aliandaa mabango
iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda kumng'oa Mufti na Ndalichako
iv. nani aliandaa maandamano
Sheikh alikiri kuhamasisha maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani aliyaandika hayo mabango. Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.
2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe
Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.
3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu
4. Vurugu mbagala.
Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi.
DHAMANA.
Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo. NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WAIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA

​
 
Kova naona anajikanyaga tu,mara armed robbery,mara kavamia kiwanja cha watu hata sijaelewa vizuri mie!
 
Nani anamlipa ponda pesa za kuhamasisha v8rugu?
 
Acha uongo we zoba si useme tuu ulimpelekea chai vitumbua pamoja na tende na mchana utampelekea ubwabwa nyama!
 
DHAMANA.
Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo. NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WAIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA[/FONT][/COLOR]
[/LEFT][/QUOTE]



Hapo kwenye red saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaffffffffffffffffffiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kesho si Ijumaa........!!
swala ifanyike pale Central police.....!!
 
انتقلوا الشيخ سحق طلب! كل شخص يحق لإنقاذ لأنها ليست جريمة
 
Kova naona anajikanyaga tu,mara armed robbery,mara kavamia kiwanja cha watu hata sijaelewa vizuri mie!

Armed robbery inahusisha tukio la mbagala,kama pia yeye alihusika kuhamasisha vurugu zile that mean pia hilo litakuwa kati ya makosa yake,kimsingi tuache sheria ichukue mkondo wake.what we need haki itendeke hatutofurahia kama sheikh ponda akionewa wala hatuwezi kuridhia kama sheikh ponda atapendelewa!sheria ni msumeno hivyo hakuna aliye juu ya sheria.
 
Punguza jazba mkuu! Aliyeandika hii makala ni huyo hapo jina lake kaliweka chini ya maelezo yake!Mimi nimecopy tu na kuiwakilisha jamvini!


Mkuu hilo ni tatizo letu waswahili, hatupendi kusoma na kuelewa. Mtu hajasoma mpaka mwisho wa habari, ana comment! Someni wakuu, someni!
 
Hongera kamanda Ponga majibu yako yamekwenda shule .

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Good!Nadhani tusubiri sheria tuone mambo yatakavyokuwa!Ni mapema sana kuzungumzia chochote juu ya kadhia hii!!
 
Mimi simpendi ponda kwa kuwa ni gaidi wa kimataifa na anahatarisha usalama wa nchi!!
 
Wadau nasikia sheikh Farid wa UAMSHO ametekwa nyara na pia Sheikh maarufu Mombasa pia katiwa nguvuni!haya ni ya kweli??
 
tumeshaambiwa Shehe Ponda ni Mkimbizi toka Burundi, na ndio maana anatumiwa kwa kulipwa na kundi kubwa la watu walioko nje. hasa arabuni na hajaanza kutumika leo tangu enzi za rais mwinyi na hadi fujo za mwembechai.
 
Back
Top Bottom