ITEGAMATWI
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 5,310
- 4,040
- Thread starter
- #41
Samahani mkuu,mimi nilijua wewe ndiye wakili uliyeshughulikia suala la yule gaidi wa kimataifa!Mkuu wangu mimi na sheria mbalimbali! Huyo wakili aliyemuhoji ndiyo anajua sheria!Mimi ni mwanajamvi huru tu niliyeleta hii habari kwenu!Au nimekosea?
Hizi lugha za kigaidi zinatafuta nini humu??
Huyu jamaa wakati wa utawala wa Mkapa alikimbia nchi,nakumbuka lile sekeseke la mwembe chai,akarudi baada ya mkapa kuondoka madarakani!Etiiiii??? Huyo ni panya mdogo sana. Subiri tu utaskia mustakabali wake sasa hivi. Kwanini alikimbia basi alipogundua kashaingia kwenye mtego?
وقف النكات والمتدينين، وأنا هنا أنا أكتب ليس فقط الأكاديمية العربيةnakunya sasa...
Unakasirika uku unajua natania...
Duh!mkojo gani tena au ule wa Emmanuel Josephat!!zinatafuta Mkojo
Asalaam Alaykum! Saa 4 asubuhi nilifika Central Police kusimamia mahojiano yake na Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO baada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10 kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni hawakumfanyia lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi.
Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:-
1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
i. kwanini waliandamana ii. nani aliandaa mabango
iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda kumng'oa Mufti na Ndalichako
iv. nani aliandaa maandamano
Sheikh alikiri kuhamasisha maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani aliyaandika hayo mabango. Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.
2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe
Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.
3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu
4. Vurugu mbagala.
Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi.
DHAMANA.
Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP. Lakini zaidi akasema kwa kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo. NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WAIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA UISLAMU MANENO YA KUSEMA
Maasalamu!
By Brother Juma Nassoro - Wakili
Source:RAHA ZA PWANI: MAHOJIANO KAMILI KATI YA JESHI LA POLISI NA SHEIKH PONDA HAYA HAPA.
TEh teh teh!Hii ni lugha ya kiarabu au kiislamu!!وقف النكات والمتدينين، وأنا هنا أنا أكتب ليس فقط الأكاديمية العربية
ukikojoa utaharibu computer yako! mkuu hiko ni kiaarabu tutukojolee??
Sisi waislam hata tukisoma hatuelewi kaka!
ha ha ha ha JF Rahaaaa!! nawaonea huruma sana wamwaminiao subuana
Sisi waislam hata tukisoma hatuelewi kaka![/QUOTE
وقف النكات والمتدينين، وأنا هنا أنا أكتب ليس فقط الأكاديمية العربية
ha ha ha ha JF Rahaaaa!! nawaonea huruma sana wamwaminiao subuana
Kova naona anajikanyaga tu,mara armed robbery,mara kavamia kiwanja cha watu hata sijaelewa vizuri mie!
chonde chonde sana ndugu, nawaunga mkono muundelee kudai haki zenu kama zipo,lakini tunaomba mambo ya BOKOHARAMU yasijetokea hapa nchini kwetu. Moja ya jambo ambalo mimi nalikubali sana ni kwa upande weak always unadai haki kwa upande strong. Kwa mfano weusi Marekani tunadai haki kutoka kwa Wazungu. Weusi South Afrika tunadai haki kutoka kwa Boers. Wanawake wanadai haki kutoka wanaume.Wasudani kusini na Wadaful wanadai haki kutoka kwa North Sudan. Waislamu wa india wanadai haki kutoka kwa Wahindu.Wasuni wachache wa Iran wanadai haki kutoka kwa washia waliowengi wa Irani. Wakurdi wachache wa Iraki wanadai haki kutoka kwa washia na wasunni wa Iraki. Na waislamu wa Tanzania wanadai haki kutoka kwa Wakristo wa Tanzania. Wafanyakazi wanadai haki kutoka kwa Matajiri wao.Raia wanadai haki kutoka kwa Serikali. Watoto wanadai haki kutoka kwa Baba zao. Nchi za dunia ya tatu zinadai haki kutoka kwa nchi za dunia ya kwanza. Maskini wanadai haki kutoka kwa matajiri. Wasiojiweza na wazembe wanadai haki kwa wanajioweza na wenye bidii. Hii ndiyo dunia na hata yesu alisema wenye uwezo wawasaidie wasio na uwezo na maskini, na hakuangalia hata kama asiye na uwezo ni mzembe au la. Tutengeneze sera ya kuwasaidia wengine ili kupunguza migongano.Kila kundi hapo juu linalodai haki linapenda kuhalalisha kwamba upande strong ndio ulisababisha madhira ya upande wao Weak.Hawatajali wala kuangalia ulifanya nini kufikia hapo.
mnitafurahijeeeeeeeeeeeeee we tukae kwa amani jamaniwakimpa armed robbery itakuwa ni kesi mbaya sana maana akipatikana na hatia hukumu yake si chini ya miaka 30n jela!!!!
Kesho si Ijumaa........!!
swala ifanyike pale Central police.....!!