Naomba swali hili aulizwe Msemaji wa Chama Bungeni ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Mimi ninajisemea binafsi. Ninatekeleza msimamo huu kivitendo. Sipokei posho za vikao Bungeni na mahala popote ambapo ninahudhuria vikao kama sehemu ya kazi yangu. ( huu ni mfano wa namna ninavyokataa posho #1 Say NO to Posho! « Zitto na Demokrasia)Najua msimamo wa Chama chako juu ya posho ni kuzipinga, je Chama chako kinatekelezaje msimamo huo kwa vitendo?
Ndio maana tulikaa kikao na kuamua kuandika barua kwa Spika ili atupe fomu nyingine za mahudhurio na nyingine za posho. Hajafanya hivyo na mimi siandiki mahudhurio. Mimi kama Waziri kivuli wa Fedha nilikuwa nazungumzia na kutekeleza msimamo wa kukataa posho kama sehemu ya kazi yangu. Ndio mandate yangu. I walked the talk. Wengine watajisemea wenyewe maana mimi sio msemaji wao na wala sio msemaji wa Wabunge wa upinzani.Je, katika suala hili ulipata ushirikiano wa kutosha toka kwa wapinzani wenzako bungeni?
Mbunge pekee wa CCM aliyekuwa na msimamo kama wangu ni ndugu Januari Makamba. Alishambuliwa sana kwenye chama chake lakini alisimama kidete. Nafurahi kuona wabunge vijana kama hawa ambao wanaleta aina mpya ya siasa. Ninamtakia kila la kheri. Ndugu Filikunjombe alinipa moyo sana kuhusu suala hili lakini sikumbuki kama naye aliacha kuchukua posho. But he was on my side all the time. January najua alikataa kuchukua posho. Wengine sijui.Je, ulipata ushirikiano wa kiwango gani toka kwa Wabunge wa CCM?
Sipokei posho ya kikao (sitting allowances) na sitapokea posho hiyo katika kipindi chote ambacho mimi ni Mbunge. Nikiwa Rais moja wa uamuzi wangu wa kwanza utakuwa ni kufuta posho za aina hii kwenye Serikali nzima. Nisipokuwa Rais nitamshawishi Rais atakayekuja afute posho hizi na kuelekeza fedha tutakazookoa kwenye kuondoa umasikini vijijini.Je, hadi sasa hupokei posho za vikao?
Nimekuwa nikitoa maoni yangu kuhusu suala la nishati ya Umeme nchini toka nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya POAC. Suala hili wakati mmoja lilitaka kunimaliza kabisa kisiasa kwani msimamo niliochukua niliamua ni msimamo mzuri lakini haukupendwa na wengi ( Sakata la Ununuzi wa Mitambo ya Dowans: Barua ya Zitto kwa Watanzania ).Una maoni gani kuhusiana na hali ya umeme nchini kwa wakati huu? Itaichukua Tanzania miaka mingapi kuwa na uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme?
Pia uliposema mikataba iwekwe wazi, ulikuwa na maana gani? Ulimaanisha ikiwekwa wazi hata sisi wananchi wa kawaida tutaweza kuiona ama ulimaanisha iwe wazi kwa wabunge peke yake?
Tulitoa kauli kupitia Waziri wetu kivuli wa Nishati kuwa Sera ya Gesi iwekwe kwa lugha ya Kiswahili. Imewekwa. Natoa wito kwa watanzania wajadili na kutoa maoni namna ya kuhakikisha kuwa gesi inakuwa kwa maendeleo ya nchi na sio kwa ajili ya watu wachache.Una maoni gani juu ya sera ya Nishati ya Gesi kutafsiriwa kwa Kiswahili?
Mkuu Zitto asante kwa majibu, swali linalofuata lina wadau wengi sana waliouliza na wana interest ya kujua kwa hamu kabisa, idadi ya Jf members waliowakilisha ikitoa picha ni kwa kiasi gani.
Zitto katika Uongozi/Ubunge na Urais 2015
Katika kipengele hiki, kinachogusa watanzania ni nia yako ya kugombea urais ambapo tayari katika vyombo mbalimbali umeshanukuliwa ukitoa msimamo wako juu ya kuwa na nia ya kugombea Urais (kwa tiketi ya CHADEMA?) 2015. Inaaminika pia wewe ni mmoja wa Wabunge waliokubaliana na mapendekezo ya moja ya kipengele kati ya vipengele vilivyowasilishwa na wabunge mapema mwezi huu wa Novemba kwa tume ya katiba juu ya kushusha umri wa kugombea urais na kuwa kati ya miaka 35-40 kati ya mengine mengi yaliowakilishwa.
Umesikika pia kwa kunukuliwa na vyombo vya habari juu ya niya yako ya kutokuwa na nia tena ya kugombea Ubunge 2015 Kigoma ama popote pale.
Kwa maelezo hapo juu, naomba ujibu maswali yafuatayo:
- Naomba kujua ni kwanini hasa umekuwa na uamuzi wa kuachana kabisa na Ubunge na kutogombea tena; na kama hayo ni maamuzi yako na hujaeshinikizwa na kitu ama mtu yeyote. Je utaendeshaje maisha yako ya kisiasa nje ya Bunge na nje ya taasisi ya Urais?
- CHADEMA kina utaratibu gani wa kutangaza nafasi za wagombea katika ngazi mbali mbali hasa ya urais?
- Katika moja ya ‘school of thought', inasemekana umetangaza haraka nia ya kugombea Urais kwa misingi ya kuwa Dr. Slaa hana tena mpango huo na kwamba nje ya Slaa huoni zaidi yako ambaye anaweza wakilisha vema. Unalizungumziaje hili mkuu?
- Ikitokea kuwa hujateuliwa na chama chako (CHADEMA) kugombea Urais 2015 kwa tiketi ya chama hicho, una nia ya kutafuta chama kingine kitakachokuruhusu kugombea nafasi hii ya Urais?
- Kabla ya uchaguzi wa 2010 ulishawahi tangaza kutogombea tena ubunge 2010; ni kitu gani kilifanya ubadilishe huo msimamo?
- Tokana na kauli yako hivi karibuni kuhusu kwamba Uongozi wa nchi hautakiwi kuwa mikononi mwa watanzania waliozaliwa kabla ya uhuru; Je kulikuwa na ulazima kutamka haya? Huoni kwamba iwapo utafanikiwa kuwa rais wa nchi yetu, urais wako unaweza kuja kutuletea generational conflicts (misuguano/migongano/mifarakano ya vizazi)?
Naomba kujua ni kwanini hasa umekuwa na uamuzi wa kuachana kabisa na Ubunge na kutogombea tena; na kama hayo ni maamuzi yako na hujaeshinikizwa na kitu ama mtu yeyote. Je utaendeshaje maisha yako ya kisiasa nje ya Bunge na nje ya taasisi ya Urais?
CHADEMA kina utaratibu gani wa kutangaza nafasi za wagombea katika ngazi mbali mbali hasa ya urais?
Katika moja ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];school of thought', inasemekana umetangaza haraka nia ya kugombea Urais kwa misingi ya kuwa Dr. Slaa hana tena mpango huo na kwamba nje ya Slaa huoni zaidi yako ambaye anaweza wakilisha vema. Unalizungumziaje hili mkuu?
Ikitokea kuwa hujateuliwa na chama chako (CHADEMA) kugombea Urais 2015 kwa tiketi ya chama hicho, una nia ya kutafuta chama kingine kitakachokuruhusu kugombea nafasi hii ya Urais?
Kabla ya uchaguzi wa 2010 ulishawahi tangaza kutogombea tena ubunge 2010; ni kitu gani kilifanya ubadilishe huo msimamo?
Tokana na kauli yako hivi karibuni kuhusu kwamba Uongozi wa nchi hautakiwi kuwa mikononi mwa watanzania waliozaliwa kabla ya uhuru; Je kulikuwa na ulazima kutamka haya? Huoni kwamba iwapo utafanikiwa kuwa rais wa nchi yetu, urais wako unaweza kuja kutuletea generational conflicts (misuguano/migongano/mifarakano ya vizazi)?
Let us be serious guys. Mnataka tutambae? Wazee wameishi maisha yao. Wameishi yetu na sasa tunataka kuwakopesha maisha ya watoto wetu?
Nadhani hivi ndivyo ungefanya wewe maana wakati mwingine watu hudhani vyao kwa wengine.Unaposema kuwa ni jitihada zako mwenyewe za kupata hayo majina ya mafisadi wa Uswisi si inakuwa sawa na kuwa una maslahi yako binafsi kama vile kutaka kuyauza hayo majina kwa wale ambao wapo kwenye list?
Kwangu mimi suala hili ni pana na majina ni sehemu tu ya suala hili. Nimeshasema mara kadhaa kwamba, nina akaunti mbili hapa nchini, CRDB na NMB. CRDB kwa ajili ya mshahara wangu na NMB kwa ajili ya fedha za kujikimu ninazolipwa na Bunge. Sio tu Uswisi, hapa Tanzania sina akaunti benki nyingine yeyote ukiachana na kuwa signatory kwenye akaunti za chama au za kifamilia.Unachukuliaje mawazo/kauli ya baadhi kuwa kuwasilisha kwako hoja hiyo ya fedha za Uswizi bungeni bila kutaja majina ni moja ya njia ya kujisafisha katika uvumi/tetesi ya kuwepo katika list hiyo ya wenye fedha Uswizi?
Nimetoa kauli jana kuhusu suala hili. Nimesema Watanzania tusiwe mazezeta. Kauli hizi ndio ambazo hata Marekani waliambiwa. Hata Ujerumani waliambiwa. Sisi kuzishabikia badala ya kufanya uchunguzi wetu kwa njia zetu ni dalili za kutaka kuua hoja hii. Hoja hii haitakufa. Tutaisimamia mpaka mwisho.Kuna ukweli wowote kuwa taarifa ile ya USWISI kuiwekea masharti Tanzania, ilitoka ndani ya serikali ya USWISI au ni mkakati wa mafisadi hawa kuzima jaribio la kurejesha pesa hizo?
Tunaweza kurejesha. Kuna Azimio la Bunge na nitahakikisha Azimio la Bunge linatekelezwa. Senegal wanafanikiwa sana. Kenya walifanikiwa kwa kutumia wachunguzi binafsi. Kama Serikali ya CCM itashindwa kufuatilia suala hili, Serikali ya CHADEMA itafanya hivyo. Hawana pa kujificha katika dunia ya sasa.Je, kuna nafasi ya nchi yetu kufanikiwa kuyarejesha mabilioni hayo ambayo ni kodi ya wanachi?
Idara ya Usalama wa Taifa ni lazima isaidie nchi kwenye masuala kama haya, vinginevyo hawapaswi kuwepo. Sheria ya TISS ya mwaka 1996 inawazuia kuchukua hatua fulani fulani. Tutarekebisha sheria hiyo. CCM wasiporekebisha sisi CHADEMA tutapata ridhaa ya wananchi kuiandika upya sheria ya Usalama wa Taifa. Tunataka usalama wa Taifa na sio usalama wa viongozi au vyama vya siasa.Ikumbukwe kuwa, tangu nchi hii itumbukie ktk ufisadi mkubwa, chombo chetu TISS kipo kama hakipo, na kama kipo basi ni kwa msaada wa mafisadi tu, Katika mtazamoo na tafsiri ya ripoti yako, taasisi ya Usalama wa Taifa (TISS) Unaiweka katika mizani ipi au haihusiki katika hili?
Uzuri wa Kamati Teule ya Bunge ni kwamba kila kitu huwa wazi kwenye hansards za Bunge na hivyo ni rahisi kufichua uchakachuaji. Pia ngoja niwamegee siasa za Bunge kidogo. Bungeni unapokuwa na hoja unaingia na hitaji kubwa sana wakati unajua fall back ni nini. Tulijua kwa hatua ya sasa hawatakubali kuundwa kwa kamati teule, tulitaka hoja ipite ili kujenga msingi wa kupanua uchunguzi siku za usoni. Tukafanikiwa. Tulitumia approach hiyo hiyo kwenye hoja ya ndugu Halima Mdee. Ni mikakati tu. Sisi tumekuwa ni Bunge la kwanza katika eneo la SADC kutoka na Azimio kuhusu 'illicit money flows'. Sasa tunapaswa kuhakikisha Azimio linakuwa enforced na kisha a public inquiry....Kwanini umependekeza kuundwa kwa tume, na kuendelea kumaliza pesa za watanzania wakati kimantiki ripoti yako ilikuwa ni ya kuiwasilisha vyombo vya dola tu, na ikiwa hawajaridhika, TAKUKURU kwa utaratibu wao wa ndani waendeshe uchunguzi na kuchukua hatua?
Kwa faida ya uchunguzi. Lazima Serikali ijenge uwezo wake wa kuchunguza na kuweka mambo sawa baada ya uchunguzi. Sasa ikiwa mimi kama mbunge nitatoa jina la walio torosha pesa kwa sasa, nani atatoa majina hapo kesho? Mbunge mpya wa Kigoma kaskazini?Huku ukijua serikali haina nia ya kuwataja walioficha fedha mabenki ya nje huku wewe ukiwa na majina; unayashikilia hadi sasa ili nini na kwa faida ya nani?
Uchunguzi bado unaendeleaYale majina ya baadhi ya watanzania unaowatuhumu kumiliki fedha haramu/halali (nyingi) nje ya nchi kwanini huyaweki bayana kwa umma? Wewe kama Mtanzania mzalendo na nchi yako kwanini umeshindwa (na chama chako) kuwapeleka mahakamani na kuwafungulia mashitaka?
Kulikuwa na tetesi kuwa nawe umeficha fedha nje. Hii inaweza kulenga kukuchafua ili uwagwaye waliofanya hivyo, je huoni kuwa hii ni nafasi adimu ya kuondoa shaka? Tuondoe wasiwasi katika hili…
Sijaelewa swali lako. Mimi ndio Waziri kivuli wa Kambi ya Upinzani kuhusu Fedha. Upinzani gani tena? Unadhani chama makini kama CHADEMA kinaweza kuacha mbunge wake apeleke hoja bungeni bila kuungwa mkono na chama? Wale wabunge waliosimama kuunga mkono niliposema 'naomba kutoa hoja' ni wabunge wa CHADEMA wale(isipokuwa ndugu Kessy na Kangi Lugola ambao ni CCM).Kwanini ulipeleka hoja binafsi ndani ya bunge na si kupitia uwakilishi wa upinzani? Je, umefanikiwa kwa kile alichotaraji kutokana na hoja hii? Uliungwa mkono na chama?
Ni wazo zuri lakini lifuate mpango wa Ports Masterplan. Sio suala jipya hili.Vipi, unauongeleaje ujenzi wa bandari ya Bagamoyo?
Nimetoa kauli jana kuhusu suala hili. Nimesema Watanzania tusiwe mazezeta. Kauli hizi ndio ambazo hata Marekani waliambiwa. Hata Ujerumani waliambiwa. Sisi kuzishabikia badala ya kufanya uchunguzi wetu kwa njia zetu ni dalili za kutaka kuua hoja hii. Hoja hii haitakufa. Tutaisimamia mpaka mwisho.
Ninaamini katika familia imara na ni mwumini wa familia ya kiafrika ambapo familia sio tu ni mke, mume na watoto bali pia ndugu na jamaa mbalimbali. Ndio maana ninaishi na ndugu zangu, nimelea wadogo zangu na wazazi wangu na hivi sasa ni nguzo katika ukoo wetu mkubwa sana ambao kuuweka pamoja kunahitaji uvumilivu na busara nyingi sana kuliko hata busara inayohitajika kwa mke na watoto. Mimi sijaoa. Muda ukifika nitaoa. Sitaoa kwa sababu ya kuonekana kiongozi ameoa. Nitaoa pindi nitakaporidhika na huyo mwenzangu ambaye nitafunga naye ndoa. Historia inatuonyesha viongozi wengi sana ambao wameoa na wameshindwa kuongoza nchi zao. Vilevile tuna viongozi wengi sana ambao hawana wake au waume na waliongoza nchi zao vizuri sana.Nini uelewa wako kuhusu familia? Umeoa? Maana Kuishi au kuwa na mke siyo jambo jepesi, linahitaji uvumilivu na busara nyingi sana, kama vile ilivyo kuishi na mume. Kama hili limekushinda, vipi utaweza kuwaongoza watanzania wote wake kwa waume?
Sijui mshahara wa Rais na naamini ni katika vitu ambavyo walipa kodi wanatakiwa kujua. Mshahara wa Rais hautakiwi kuwa siri kwa mtanzania yeyote. Inapaswa kuwa wazi kabisa na kila Raia ajue. TRA watakuwa wanajua kama sio tax exempt. Nadhani tukifatilia kupitia Utumishi tunaweza kupata hizo data. Hebu ngoja nipeleke swali Bungeni kuhusu jambo hili ili lijibiwe Mkutano ujao wa Bunge. Haya ni mambo ambayo tuna overlook sana.Mkuu Zitto is there any chance unajua mshahara wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mshahara wa makamu wa rais wa JMT, na ule wa rais wa Zanzibar? Ni mahala gani pa kwenda kufuatilia hizo data kwa yeyote yule anayetaka kufahamu hayo? Pia katika hili unadhani ni kwanini hiyo mishahara inawekwa siri sana kwa wananchi hali kimantiki wananchi ndio waajiri wao?
Sina maoniMkuu unadhani unakubaliana na mfumo wa Uongozi wa serikali uliopo sasa? Kama HAPANA unadhani ni mfumo upi ambao ni mzuri na unafaa kwa kupata viongozi wa vyama vyetu kwa ngazi za juu kama M/Kiti, Makamu M/Kiti na Katibu Mkuu – Ule wa kuteua na kupigiwa kura za wajumbe au kugombea na kupigiwa kura na wajumbe na kwanini?
Nilikuwa kwenye jopo la Rais Kohler kuhusu Afrika. Nilimaliza kazi hiyo mwaka 2009. Niliteuliwa tu na Rais Kohler wa UjerumaniNi ukweli kuwa wewe ni mshauri wa uchumi wa Ujerumani. Kama ni kweli, je ni kitu gani kilichokutambulisha hadi kufikia kupewa hiyo nafasi?
Nimewahi kusema ninamiliki nini ili kufuta uzushi unaoenezwa kuwa mimi nina ukwasi wa kutisha. Nina gari 2, moja Freelander na nyingine Toyota vista. Ninajenga nyumba Kigoma, kijijini Mwandiga. Nina shamba lenye mikorosho 400 Mtwara, Nina shamba la ekari 3 eneo la Mbutu, Kigamboni. Ninadaiwa na CRDB milioni 120 nilizokopa kwa ajili ya kununua vitu hivyo. Nina mkopo wa Bunge wa kununua gari wa tshs 90 milioni ambao tunalipa nusu yake! Nina exemption ya kodi ya kuingiza gari lakini nimekataa kuitumia kwa sababu mimi kama Waziri kivuli wa Fedha ninapinga tax exemptions na hivyo nimeamua ku walk the talk. Sijaitumia na sitaitumia exemption hiyo.Umewahi kuanika utajiri wako (vitu unavyomiliki); unaweza walau kutufafanulia unamiliki magari mangapi, nyumba ngapi n.k?
Kuna sera na sheria za kusaidia ubunifu wa kisayansi. Tatizo ni kwamba Tanzania hatuheshimu sana R&D issues na matokeo yake tumekuwa watumiaji wa ugunduzi wa watu wengine. Kwenye eneo la ICT nimeona vijana wameanzisha The Kinu, tutawasaidia. Hii platform hapa tunayotumia JF imetengenezwa na Mtanzania Maxence, lazima tumsaidie ili iweze kudominate eneo lote la maziwa makuu.Unazionaje shughuli za kisayansi za watanzania? Je, kuna sera yeyote Tanzania inayompa kijana wa kitanzania nafasi ya kuwa mbunifu?
Maswali hayajaisha?
Ni hatua nzuri sana na nadhani mtatoa fursa kama hii kwa watu wengine watakao tayari kujiweka wazi. Wasiwasi wangu ni kwamba maswali ni mengi sana inabidi mtu kukaa siku nzima kwenye KOMPYUTA kujibu maswali. Sio kila mtu atakuwa na muda kiasi hiki. Ninachoshauri ni kuwa na maswali machache muhimu au kuna na maswali na kumwuliza mapema interviewee na yeye ku-paste majibu yake na mjadala uwe kwenye majibu hayo kwa muda maalumu ambapo kila member ataweza kuuliza na MODs kuratibu zoezi hilo. Nitafurahi kuona wanasiasa wengine wakihojiwa hapa. Nafurahi kufungua dimba.Hatuwezi kuwa sahihi katika kila nyanja, vipi umeridhika na namna mdahalo huu ulivyoenda?
Jamiiforums ni mtandao wa kijamii ambao umepata sifa kubwa sana. Kuna watu ambao kila kinachoandikwa JF wao wanaona kweli. Utasikia wanasema, ndio nimeona JF. Kwa hiyo mmepata kuamianiwa sana. Sasa uaminifu huu lazima muutumie vizuri. Kuna watu wanaleta maneno ya uwongo hapa, uwongo mwingine ni wa dhahiri kabisa unaachwa. Kuna watu wanaleta habari za kweli kabisa lakini zinatolewa. Ni lazima Wanachama wa JF wawe makini kwa kile wanachoandika na MODs wawe makini zaidi kuhakikisha masuala ambayo uhakika na yanaharibu reputation za watu yasiruhusiwe.Unaiongeleaje JamiiForums na ungepata nafasi ya kukutana na wahisani ungewashauri waisaidieje?
Yataka moyo sana. Mimi hutumia JF kama kioo hivi. Kuna mambo mengi mazuri sana humu. JF hutusaidia kupata taarifa kwa haraka badala ya kusubiri magazeti siku ya pili. Hata hivyo Najua kuna mengi sana ya uwongo yanasemwa humu lakini kwa kuwa najua ni uwongo hainisumbui sana. Wakati mwingine hata huyo msema uwongo huwa anajijijua kuwa anasema uwongo. Tukikutana mitaani wengine wanaona aibu na hata kuomba radhi. Kuna wakati mpo kwenye kikao na mtu anaandika suala la kikao hicho JF kwa kutwist ukweli na wakati mwingine unamjua na unamwona anavyohangaika. Wakati mwingine mtu ni rafiki yako kabisa lakini ukimpa kisogo tu anapost kitu JF cha uwongo. I don't take anyting personal. Hapana ninakomazwa zaidi maana najua huko mbele criticism zitakuwa nyingi sana. Ninashauri wenzangu wapite katika kikaango hiki. Mimi sina la kuficha ndio maana nipo wazi kabisa kuja hapa na kujibu hoja zinazonihusu. Nitaendelea kushiriki mijadala Jamiiforums.Wewe ni mmoja kati ya wanasiasa wachache wenye 'guts' za kujibu kero za wananchi hata mitandaoni (hasa JF), tunakupongeza kwa hili; unaweza kuwashawishi wanasiasa wengine kufanya hivi?
nashukuru sana kwa kupata fursa hii. Asante sana na hilo lingine nitajipanga tu. Hiki chombo chetu sote