Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,879
Naomba swali hili aulizwe Msemaji wa Chama Bungeni ambaye ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Mimi ninajisemea binafsi. Ninatekeleza msimamo huu kivitendo. Sipokei posho za vikao Bungeni na mahala popote ambapo ninahudhuria vikao kama sehemu ya kazi yangu. ( huu ni mfano wa namna ninavyokataa posho #1 Say NO to Posho! « Zitto na Demokrasia)Najua msimamo wa Chama chako juu ya posho ni kuzipinga, je Chama chako kinatekelezaje msimamo huo kwa vitendo?
Posho za vikao ni wizi wa fedha za umma. Posho za vikao ni moja ya dalili za mfumo unaoitwa ‘rent seeking ' au Pato-nyemelea. Huu ni mfumo wa kujipatia kipato bila kufanyia kazi. Wabunge wamechaguliwa kwa kazi maalumu na tunalipwa mshahara na marurupu mengine kwa kazi hii. Kulipwa posho ya kukaa kitako ni kujipatia kipato bila kufanyia kazi. Wabunge wanakuwa kama genge la majambazi yanayovamia benki na kuiba! Kwa kuwa mfumo unatoa nguvu kwa wabunge, basi hawatumii silaha, bali wanatumia mfumo kujilimbikizia mali. Sitting allowances ni uporaji.
Ndio maana tulikaa kikao na kuamua kuandika barua kwa Spika ili atupe fomu nyingine za mahudhurio na nyingine za posho. Hajafanya hivyo na mimi siandiki mahudhurio. Mimi kama Waziri kivuli wa Fedha nilikuwa nazungumzia na kutekeleza msimamo wa kukataa posho kama sehemu ya kazi yangu. Ndio mandate yangu. I walked the talk. Wengine watajisemea wenyewe maana mimi sio msemaji wao na wala sio msemaji wa Wabunge wa upinzani.Je, katika suala hili ulipata ushirikiano wa kutosha toka kwa wapinzani wenzako bungeni?
Mbunge pekee wa CCM aliyekuwa na msimamo kama wangu ni ndugu Januari Makamba. Alishambuliwa sana kwenye chama chake lakini alisimama kidete. Nafurahi kuona wabunge vijana kama hawa ambao wanaleta aina mpya ya siasa. Ninamtakia kila la kheri. Ndugu Filikunjombe alinipa moyo sana kuhusu suala hili lakini sikumbuki kama naye aliacha kuchukua posho. But he was on my side all the time. January najua alikataa kuchukua posho. Wengine sijui.Je, ulipata ushirikiano wa kiwango gani toka kwa Wabunge wa CCM?
Sipokei posho ya kikao (sitting allowances) na sitapokea posho hiyo katika kipindi chote ambacho mimi ni Mbunge. Nikiwa Rais moja wa uamuzi wangu wa kwanza utakuwa ni kufuta posho za aina hii kwenye Serikali nzima. Nisipokuwa Rais nitamshawishi Rais atakayekuja afute posho hizi na kuelekeza fedha tutakazookoa kwenye kuondoa umasikini vijijini.Je, hadi sasa hupokei posho za vikao?