Mahitaji ya watanzania ni yaleyale Makonda ukiyatimiza haya kijiji unachukua, Hayati Magufuli alipendwa kwa Haya

Upekuzi101

Senior Member
Aug 28, 2020
134
348
Sina mengi ya kusema ila Makonda ukiweza kutatua kero za wananchi on spot, kurudisha uwajibikaji kwenye ofisi za umma maana waajiriwa wote na watumishi wote wapo kwa udhamini wa CCM so unaweza kuvimba nao, huduma muhimu ziboreshwe, ikiwemo shule, hospitali, miundombinu ya maji, barabara na umeme nchi nzima, bila kusahau ukamilishaji wa bwawa la Nyerere ili tupate umeme wa kutosha, miradi mipya ubuniwe na ya zamani ikamilishwe ili kuleta tija kwa wananchi.

Pambana na rushwa, wizi wa Mali ya umma na uonevu Kati ya raia au dhidi ya raia. Ukiweza kuyafanya haya kwa uamnifu mkubwa na watanzania wakaona matoke, mbona wabongo hawana baya hata nchi wanakupa. By the way mfumo wa Chama chenu na nafasi ulonayo, wewe ni kama free player unaweza kuamrisha mifumo ikianza kufanya kazi in that direction na ukaeneza Chama kwa namna yoteyote inayofaa.

Majukumu mema kiongozi.
 
Leo Dodoma alitaka kujaribu style ya jiwe ya kutatua changamoto za wananchi lkn yakamshinda.

Ajue zama zimebadilika.
 
Kuna kila sababu ya kupiga vita ujanjaujanja wengine wanawaita Wahuni.

Kinacho kera katika nchi hii ni wazee wa dili hawa jamaa wapo serious na kazi yao hata ikitokea mkondo wa sheria ufuatwe lakini utashuhudia jinsi vifungu vya sheria vinavyo wekewa mbwembwe za kuokoa muhalifu.

Leo hii Raia wa kigeni wamejiwekea mtandao mrefu hakuna mamlaka ya kuwahoji.

Muhimu hapa ni kuwa Wazalendo katika nchi yetu
 
Kesi aliyofungua Kubenea dhidi ya Makonda iko inapikwa upya. Wanamsubiri Makonda ajichanganye ili wamkamate na kumfunga
 
Back
Top Bottom