Mahitaji maalumu kwa wanawake wanapokuwa jela

Mahitaji maalumu kwa wanawake wanapokuwa jela

Kiujumla wanawake wana mahitaji ya tofauti hasa hasa katika vipindi viwili ambavyo ni unique to women only.

1. Wakati wa hedhi
2. Wakati wa ujauzito.

Swali langu ni je, katika jela[prison service] zetu Tanzania, wanawake wakiwa kwenye hivi vipindi, wanapata huduma zipi za ziada. Kwa walio mwenye periods, wanapewa sanitary pads na pain killers etc. Kwa wajawazito, swala la lishe, kupumzika etc je yanaangaliwaje?

Najua kuna watu wanaweza sema mimi mwanaume nataka nijue nini kuhusu mambo ya wanawake? You never really know, kesho anaweza kuwa your beloved wife behind bars.

Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !

Near by Iwambi Mbeya.
 
Jera hakuna utu,kama unataka utu ungebaki uraiani usingekuja jera

Ndugu,

Kwenye jela zetu kuna watu wa aina mbili, wafungwa waliohukumiwa na mahabusu wanaosubiri hukumu zao. So kila aliyeko huko amekwenda kwa sababu anastahili.

Binafsi niliumia sana siku moja dada yangu amelala ndani kwa kosa la kusingiziwa kabisa, I was with her huo muda huo wanaosema alikosa... I witnessed injustice first hand... Alitoka baada ya siku kadhaa, lakini nikasema what if angekaa huko muda mrefu.

Kuna mambo inabidi tuyaangalie kwa utofauti.
 
Hii thread imeniumiza sana,kuna vitu tunavichukulia kawaida tu na tunasahau wenzetu ambao hawana.....Nimewahi kwenda sehemu nikaambiwa wasichana wakiwa hedhi hawaendi shule mpaka iishe kwa kuwa kujisitiri inakuwa shida kwa vitambaa yale masaa wanayokaa shule. Sasa leo sipati picha hao kina mama,complication zote za utu uzima,maradhi haya,mlo usio mzuri....wanavyoteseka.....najua kuna namna wanaweza saidika....pamoja na makosa yao wao bado ni binadamu na wanastahili huduma ambazo wanawake wengine tunazipata.....asante kwa hii thread....research idea!

Me naamini ni muhimu kuyaangalia haya.

I would want my woman to through a difficult time in jail, halafu akapata hadi time hasa hasa na periods. Sijui ni nani anacheck hizi mambo lakini we need to check
 
Wanasema ukiwa jela we ni mali ya serikali..hatari sana.
 
jela ni jela tu mbona mahabusu tu wanajisaidia kwenye ndoo mnazani ile harufu ni nzuri,, shida ni nyingi,, watu walisha zungumzia sana hii ishu na kwa baadhi ya magereza huwa wanacare kidogo ila shida kubwa ipo mahabusu kule ndio hakuna utu kabisa

mmmmmmh.. siamini katika hili labda uweke picha
 
Tukipaza sauti zetu kwa pamoja twaweza leta mabadiliko, hawa ni binadamu wenzetu.
 
haki za kibinadamu zipo ulaya tu
afirika bado sana
 
Tuliopo huru huku uraiani tunataabika kiasi hiki na serikali haitujali kabisa.Sembuse waliopo jela
Afrika Jela ni Mbaya, Jela ni mateso, jela ni utumwa. Waulizen waliotoka jela watakwambien ukwel.
 
Back
Top Bottom