Erwin Rommel
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 429
- 115
Leo ni takriban siku ya 12 tangu Zitto na wenzake wavuliwe uongozi Chadema kutokana na usaliti walioukiri.
Hadi leo sijaona mtikisiko wowote (nasema mtikisiko) kwa chama hicho nchini kuhusu kupinga hatua hii ya kamati kuu ya CDM, zaidi ya kelele na matusi humu JF, kelele ambazo naamini kwamba kwa asilimia kubwa zatoka CCM., pamoja na kutoka kwa akina Fyonza na wasaliti wenzake.
Support kubwa anayopata Zitto ni katika magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Daily News, kitu ambacho ilimpaswa kujiuliza vipi?
Nilitarajia katika siku hizo 11 yafuatayo yangetokea:
1. Maandamano makubwa ya wana CDM - hata katika asilimia 40 ya mikoa yote (au aslimia 40 ya wilaya zote) kumsupport Zitto. Hilo halijatokea., na pia Zitto ajiulize kwa nini.
2. Mlolongo wa kujiuzulu kwa viongozi wakuu wa CDM hata kwa silimia 20 tu (kamati kuu, wenyeviti mikoa etc). Hilo pia halijatokea na Zitto inapaswa ajiulize kwa nini.
Ama kweli Zitto kwishney mahesabu yake yamemuumbua sana! Na wanaomtetea CCM wamepatikana kwa hili kwani watu wao katika CDM wametimuliwa na ndiyo maana wanasononeka sana.
___