YphNet
Member
- Sep 3, 2022
- 62
- 103
Hii ni offline app niliyoitengeneza kwa ajili ya matumizi binafsi kwa lengo la kukokotoa jumla ya mauzo ya siku katika fremu yetu ndogo. Nimeiweka Playstore ili kushare na wengine wanaohitaji. Kwa kifupi unavyoanza siku mpya ya biashara unagusa button [J] ili kufungua jalada mpya na utaona tarehe ya jalada. Akija mteja unagusa button [d] ili kurekodi ulichouza yaani jina la bidhaa na bei. Mwisho wa siku unagusa button [+=] kulia kwa chini ili kukokotoa jumla ya mauzo yote. Hapo chini ni screenshot ya hii app. Kuedit ulichorekodi utabadili mode button [1] hapo juu kuwa [2] kisha unagusa neno ili kuedit, ukimaliza utachange mode kuwa [1] (default mode). Licha tu ya kurekodi mauzo unaweza pia kurekodi mambo mengine mbalimbali na kutafuta jumla au wastani.
NB: Sio lazima urekodi kitu kimoja kimoja, mfano mteja amekuja kununua pipi 8 za tsh 50 kwa mara moja, sio lazima urekodi pipi moja moja mara 8, unaweza kuandika, mfano kwenye bidhaa "Pipi8" kwenye kiwango/kiasi (bei) utaandika "50*8" hivyo app itazidisha yenyewe wakati wa kutafuta jumla. Gusa nenio "Mahesabu" for more options. Very small app, about 98 KB only!!
Link: Install toka Playstore.
UPDATE:
Kitabu (PDF) cha muongozo jinsi ya kutumia Mahesabu app
kipakue hapa: mahesabu muongozo.