Mahari na kufunga ndoa ndio sababu inayofanya vijana wasioe

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Prakatatumba etumba etumba abaabaabaabaa, nimekaa nimefikiria kitu kimoja, maisha yenyewe yalivyo magumu hivi unaambiwa mahari ya milion 2, hivi hiyo million 2 si naweza invest ikanipatia hela nyingine?..

Just imagine hauko stable then vijana wanaambiwa mahari million 2/3, na bado huyo mwanamke ukimuingiza ndani aje atumie hela yako kwenye mambo yake.
Tusiwalaumu vijana tuwaache watafute hela.

Nikawaza tena, makanisani kuna makundi mengi ya vijana 27-35 hawajaoa kwa sababu wengine hulka yao hawapendi sherehe/harusi (kama Mimi) . vijana wanakua wanafikiria sasa nikiweka mwanamke ndani na sijafunga ndoa basi nitafutwa usharika,nitaonekanaje kanisani? N.k

Mimi prakatatumba nawaagiza vijana woote ambao hamjaoa na hamna mahari, chukua Mwanamke ishi nae huku unaendelea kutafuta hiyo mahari mdogo mdogo ukipata peleka, ukisema ujichange ukamilishe mahari miaka 30 inafika unaiyona.

Mimi babu yenu Leo nimetimiza miaka 67 ndio nimeenda kukamilisha mahari kwa bibi yenu.
 
Ndiyo maana single mothers bado wapo kwenye chart pamoja na kejeli wanazopewa.

Hawana complications kwenye "Sogea tuishi", wazazi wake wenyewe wanaona heri kapata wa "kumstiri" na hakuna mahari za kukomoana.

Huyo mwanamke wa kuishi naye huku unadunduliza mahari lazima ameshafeli mahali sasa kaona bora yaishe na ndiyo hao SMs.
 
Back
Top Bottom