Mahari; Mchakato na viwango vyake

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,119
Leo tulikuwa na mjadala kuhusu mahali na hasa viwango vya mahali vinavyotolewa

Mtu mmoja akasema yeye aliomba Mil.3 kama mahari ya kumuoza binti yake. Ikanikumbusha mbali kidogo, nikiwa secondary school nilienda na team iliyokwenda kujadili mahali ya kaka yangu aliyetaka kumuoa binti mmoja wa kisukuma. Nakumbuka mzee mwenye binti alianza na mahari ya Mil 6 lakini ikaishia kuafikiwa laki mbili na nusu.

Sasa nimeona bora tujadili kidogo hapa kitu gani hasa kinaangaliwa wakati wa kutaja mahari, nini hasa maana ya mahari na nani anatakiwa kuchukua mahari?

Wale waliooa na kuolewa tayari, wao walitoa au kutolewa mahari kiasi gani na wale wenye mabinti, wanategemea kutaka mahari kiasi gani?
 
mh!
hapa kwenye mahari hapa partner pagumu ujue!
 
hujambo lakini partner wangu`?
Mi sijambo partner wangu, hofu kwako tu

Mh ni pagumu kweli partner ndio maana nikasema labda niilete jamvini mawazo yapatikane ya wengi
 
Upande wangu c pendi kuolewa kwa mahari kubwa
mil 3 ndo nini kwani nauzwa???
 
Upande wangu c pendi kuolewa kwa mahari kubwa
mil 3 ndo nini kwani nauzwa???
habari ya hapa kimila kwa mfano (unakotokea wewe) Mahari huwa ni ya nani? Nasikia kuna wengine mahari huwa ni ya muolewaji mwenyewe so mara nyingi ye ndiye huwa anaplay sehemu kubwa ya kuamua inakuwa kiasi gani. We unafikiri average mahari inatakiwa kuwa kiasi gani?
 
Last edited by a moderator:
Issue ngumu sana kwa kweli maana kila sehem watu wanatofautiana
Sehemu nyingine utaambiwa leta ng'ombe na mbuzi au fedha yenye thamani na hizo
Issue ya mahari ni mtihani na nakumbuka huwa mama ananiambia hajamaliza kulipa mahari yake mpaka leo japo ameolewa miongo kadhaa imepita snowhite mzima wewe
 
Last edited by a moderator:
mie bukheri!anga la Maulana lanifunika uzuri!
 
Hahahahaa mkuu, hiyo ya kutokamilisha mahari hata baada ya miongo kadhaa imenifurahisha. Nimewahi kusikia stori hizi sana tu
 
mie bukheri!anga la Maulana lanifunika uzuri!

Shukrani sana kwa uzima wako na nafurahi sana kusikia hilo

Hahahahaa mkuu, hiyo ya kutokamilisha mahari hata baada ya miongo kadhaa imenifurahisha. Nimewahi kusikia stori hizi sana tu
Mkuu ni balaa maana ni issue ngumu sana kwa kweli na kila kabila linatofautiana viwango na mahitaji na gharama za mahari yenyewe
 
kitu gani hasa kinaangaliwa wakati wa kutaja mahari, nini hasa maana ya mahari na nani anatakiwa kuchukua mahari?

:: kitu gani hasa kinaangaliwa wakati wa kutaja mahari?

Nadhani mahari hutegemea na mtazamo wa anayepanga ambapo mara nyingi huwa ni wazazi au walezi upande wa mwanamke..

:: nini hasa maana ya mahari na nani anatakiwa kuchukua mahari?

Mahari ni aina ya malipo anayolipwa binti na mchumba wake au ni malipo yanayotolewa kwa binti na upande wa mume anayetaka kuoa. (Ingawaje kuna jamii nyingine mwanaume ndiye hutolewa mahari)
Nadhani utofauti wa mila hupelekea pia utofauti juu ya nani achukuaye mahari, kama ni binti ,mlezi au mzazi.
 
Hilo swali lako linaendeshwa na factors mbili kuu mbali na utashi wa mpangaji mahari: kabila na dini
 
Mkuu, kama anayelipwa ni mmoja wa wale wanaotaka kuingia kwenye ndoa (kulingana na maelezo yako) Je malipo hayo ni ya nini? Kwa ajili ya kitu fulani au for what exactly?
 
Lakini sii makabila yote mwanaume atoe mahari !! Kuna baadhi ya makabila Wanawake hutozwa mahari ili Mwanaume amuoe !! Je utaAmini ?

1.:: nini hasa maana ya mahari na nani anatakiwa kuchukua mahari? Ni bi Harusi achukuwe na ndizo za kumuandaa na matayarisho yake.
Hivi sasa kila siku mfumko wa bei na bidhaa zikipanda juu na MAHARI yanapanda vibaya sana.!!


 
Hilo swali lako linaendeshwa na factors mbili kuu mbali na utashi wa mpangaji mahari: kabila na dini
Kwenye makabila naweza kuelewa kwa mfano
wasukuma; wao akiwa mweupe mahari lazima iende juu maana wenzetu wale wako obsessed na rangi
Wakurya; wao kuoa ni kama kuuza na ndio maana binti akishaolewa hata akitolewa macho ni sawa tu maana anakuwa property ya mume.

Kwenye dini labda ungetusaidia Gaijin, dini inasemaje kuhusu mahari?
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaa kwahiyo Inflation ipo mpaka kwenye mahari eeh? Umenifurahisha mkuu
 
wasukuma; wao akiwa mweupe mahari lazima iende juu maana wenzetu wale wako obsessed na rangi

Wasukuma wa wapi hao ambao hupandisha dau la mahari kulingana na rangi ya ngozi?
 
Mkuu, kama anayelipwa ni mmoja wa wale wanaotaka kuingia kwenye ndoa (kulingana na maelezo yako) Je malipo hayo ni ya nini? Kwa ajili ya kitu fulani au for what exactly?

Mkuu ishu ya mahari ina mkanganyiko mkubwa na ndio maana nilianza kwa kujitetea kuwa namna ya utoaji hutofautiana kulingana na jamii mbalimbali za watu...
Binafsi sijawahi kuona mila ambayo binti ndiye hupewa mzigo wote wa mahari ila nimekuwa tu nikisikia...
Unajua kuwa mahari hutolewa kama ishara ya upande wa mwanaume kuwashukuru wazazi wa upande wa kike.
Katika imani ya ndoa, huwa inaaminika kuwa binti anapoolewa ni kama unamtoa kwenye familia yake na kumleta kwenye familia yako(mwanaume) hapo ndiposa mahari inapoingia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…