Mahakama yatupilia mbali ombi la Lulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yatupilia mbali ombi la Lulu

Discussion in 'Celebrities Forum' started by MwanaFalsafa1, May 7, 2012.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu', leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
  [​IMG]Kamera zikimfuata kwa shauku.

  Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.

  (PICHA: RICHARD BUKOS / GPL)


   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Du hatareeeeeeeeeeeeee!!
   
 3. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  du! huyu mtoto kesi inamnukia asubuhi yote hii??? wangeweka swala la mimba, kesi iwe inasikilizwa muhimbili, labda lingekuwa na uzito! pole lulu, sali rozari kwa bidii, itakusaidia!
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Inaelekea walikua wana jaribu kufoji cheti ili aonekane underage.
   
 5. Nish

  Nish JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 732
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hiyo ya muhimbili umenivunja mbavu lol!
   
 6. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mhhhh....... Uwongo utatucost wabongo...... Alishajiachia kitambo kuwa Ana 18.
   
 7. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  wamesha foji vyeti,polisi na takukuru wapo wspi?
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,135
  Likes Received: 6,630
  Trophy Points: 280
  Hata mimi namwonea huruma sasa,
  chango la uzazi linaniuma kwa kweli.
   
 9. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,224
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa sheria za nchi hii, kughushi kitu chochote kile ni kosa la jinai, inatakiwa mahakama ianzie hapo kuwashikisha adabu walioghushi cheti cha kuzaliwa cha binti huyu
   
 10. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  usicheke my dear! ndivyo serikali ya magamba inavyoendesha mambo yake, waeza sikia kesi imehamishiwa muhimbili!
   
 11. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  unaongelea serikali hii ya magamba, au ijayo 2015 chini ya gwanda!??? kama ni hii utasubiri sanaaaaaa, wakubwa wenyewe ndio walikuwa wanamega, sasa unategemea nini???
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Siku zote hajawahi kusali hiyo kitu inayohusiana na Vatican,,leo ndo atasikilizwa? achana nae!
   
 13. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135

  Mamndenyi chango la uzazi?...kumbe na ww mkongwe eeh?au ndo zile mimba za utotoni...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  rozali na baibui...nimeipenda iyo.
   
 15. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Si kazi ya Mdee hiyo na Hawara wake Z.
   
 16. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwani mtoto anapata mimba? sasa hivi anaonekana kabisa mjamzito! sasa sijui watasema ni mtoto ana mimba ya mtoto! binafsi namuonea huruma kwa yaliyomkuta, maana yanaweza mkuta mtu yeyote. sheria tu ichukue mkondo ke na haki itendeke.
   
 17. Type

  Type JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mawakili wenyew wali nazi, hapo tayar wanakes iweje mtu m1 anvyet viwli vya kuzliw, wakajipange upya la sivyo wamkosa hy bich
   
 18. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mdomo uliponza kichwa.
   
 19. senior citizen

  senior citizen Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhan tuiache mahakama ifanye kazi yake kabla hajapata hayo matatizo hatukuona hata mwanaharakati mmoja aliyejitokeza kumuonya huyo binti sanasana mlikuwa mnamshangilia na hata alivyohojiwa na katika kipindi cha eatv channel 5 na mtangazaji Salama Jabiri sote tulikubali na kuelewa kuwa ametimiza the age of majority yaani utu uzima iweje leo aseme kuwa ni under 18??? Asiyefunzwa na wazazi hufunzwa na ulimwengu alikimbilia mambo makubwa ndio hayo sasa!!! Na hili nadhan imekuwa funzo kwa vijana wetu ambao hukimbilia mambo kabla ya umri wao! Asanteni.
   
 20. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  UMRI wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba jana ulizua utata katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mawakili wanaomtetea kutaka kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo ili akashtakiwe kwenye Mahakama ya Watoto.

  Kesi hiyo ilitajwa jana huku mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Keneth Fungamtama, wakiwasilisha maombi kuhusu suala hilo la umri wa mteja wao wakitaka asishtakiwe mahakamani hapo kama ilivyo sasa. Fungamtama ambaye alikuwa akisaidiana na Mawakili Peter Kibatala na Fulgence Masawe, alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 17 hivyo, kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika Mahakama ya Watoto. "Mshtakiwa ana umri wa miaka 17 na tuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa ambacho kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa," alidai Fungamtama.

  Fungamtama alisema Kifungu cha 4 cha Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 Kipengele namba 21, kinatamka wazi kuwa mtoto ni yule aliye na umri chini ya miaka 18. Wakili huyo aliendelea kunukuu vifungu mbalimbali vya Sheria ya Mtoto kama 98 (i) na 114 (ii), ambavyo alidai kuwa vyote vinawapa nguvu ya kuwasilisha maombi yao hayo ya kuihamisha kesi hiyo. "Hata katika suala la Mahakama, vifungu vyote vya sheria hii vimefafanua, hivyo tunawasilisha maombi yetu kwamba mteja wetu ana umri wa miaka 17 na shauri hili lingepaswa kusikilizwa Mahakama ya Watoto," alidai.

  Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda aliomba wapewe muda zaidi kwa sababu bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo. "Kesi hii imekuja mahakamani hapa kama ya mauaji na upelelezi bado haujakamilika. Tunaposema haujakamilika, tunapeleleza kila kitu, likiwamo suala la umri," alieleza Kaganda. Alisema hata jina linaloonekana katika cheti cha kuzaliwa kilichowasilishwa mahakamani hapo, linasomeka Diana Elizabeth wakati mshtakiwa ametajwa mahakamani hapo, kwa jina la Elizabeth Michael. "Tunaomba muda tuweze kuchunguza kuhusu umri wa mshtakiwa kwa sababu aliwaeleza polisi kwamba ana umri wa miaka 18 halafu mawakili wake wanakuja kueleza hapa mahakamani kwamba ana umri wa miaka 17," alidai Kaganda. Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa kutokana na mvuto wa kesi hiyo katika jamii, wanaomba wapewe muda zaidi kufanya upelelezi ili kumtendea haki mshtakiwa huyo.

  Kuhusu cheti hicho kusomeka Diana Elizabeth, Wakili Fungamtama alikiri na kudai kuwa ni jambo la kawaida hasa kwa Wakristo kuwa na majina mawili. Fungamtama alidai kuwa hawana pingamizi na maombi ya upande wa mashtaka kwamba wapewe muda zaidi wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa cha mshtakiwa, ingawa alidai kuwa suala hilo halina ugumu. Akitoa uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mkazi Augustina Mbando alisema: "Mahakama imesikiliza maombi yaliyoletwa na Fungamtama na Kaganda na imeona kesi iliyopo hapa ni ya mauaji na jinsi kesi hii ilivyo, hatuwezi kufanya hoja yoyote hadi upelelezi utakapokamilika."

  "Kama defence (upande wa utetezi) wana maombi yoyote wanaweza kufanya hivyo kupitia Mahakama Kuu,"
  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 21, mwaka huu itakapotajwa tena. Inadaiwa kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam msanii huyo wa kike, alimuua Kanumba. Jana Lulu alifikishwa mahakamani hapo saa 2:50 asubuhi akiwa peke yake kwenye gari linalobeba mahabusu, huku akisindikizwa na magari mengine mawili.

  Alipoingia mahakamani alikuwa amezingirwa na askari Magereza na Polisi zaidi ya 10 na kuufanya umati mkubwa wa watu uliofurika mahakamani hapo kushindwa kumwona. Miongoni mwa watu waliofika mahakamani hapo jana ni baba mzazi wa msanii huyo, Michael Kimemeta na ndugu zake wengine kadhaa.
   
Loading...