Mahakama yaamuru Kafulila akamatwe mara moja

Mahakama yaamuru Kafulila akamatwe mara moja

Hiyo itakuwa kesi nzuri zaidi hasa pale magwiji wa sheria wa UKAWA watakapoanza kuyaomba mafaili ya Mgawo wa fedha za Stanbic....'safari moja huanzisha nyingine'...waache wajilete!!

Ccm inabidi wajipange upya kwani kesi hii itawaacha utupu
 
Niliona hadi sura ilikuwa inajionyesha kabisa kuwa hana amani moyoni

Naanza kupata wasiwasi, kuna MTU mkubwa sana anaweza Ku commit suicide kwa hili shinikizo. Ni vema viongozi hawa watafutiwe washauri nasaha
 
acheni uingo mnatuharibia jf yetu imeguka ya wakudaa sio watu wanaotaka mabadiliko
 
Hao washaishiwa mbinu. Unaambiwa Jana Dodoma kwenye kikao cha Kamati kuu JK kachanganyikiwa maana akiangalia wajumbe karibu nusu ni pro Lowasa. Sasa halo mtapanga nini cha siri kisifike kwa walengwa? Kuwafukuza nako hawezi
Awakate tu make hamna nmna
 
Nimependa ushauri huu!! .
.
WANA CCM NISIKILIZENI..!!
Nina ushauri kwa wana CCM wenzangu; Lowasa kuhamia CHADEMA msipaniki. Kama kweli tulimaanisha kuwa hafai, ana uchu wa madaraka, alikiuka kanuni na maadili ya chama, ni mwizi na tena ni fisadi basi inabidi tushangilie kuondoka kwake, kwani kuvuja kwa pakacha sio ndio nafuu ya mchukuzi? Ila kama tulimkata kwa maslahi ya watu wachache na ikiwa tulitumia akili ndogo kulikata jina lake basi itabidi tujilaumu wenyewe kwa lolote tusilolitarajia litakalotokea.
Na tukiendelea kutumia akili ndogo za kudhani tutashinda kwa "magoli ya mikono", basi tunakwenda na maji mchana kweupe!
.
Tukijidanganya kuwa matusi, kejeli, mipasho, maneno ya kwenye kanga na nyimbo za Komba kwamba zitabadilisha huu upepo, pia tutajikuta tunakuwa chama cha upinzani bila hata kujiandaa kisaikolojia. Mwana CCM utakuwa unajichanganya kuushambulia uamuzi wa Lowasa kuhamia CHADEMA kwa sababu kimsingi CCM yetu ilishabariki vijana kadhaa wamshambulie majukwaani ili aonekane hafai na hao vijana wakazawadiwa vyeo. Mtu tuliemuona hafai kwetu inatuuma nini akiondoka kwetu? Ukioa mke kisha ukamtuhumu mbele za watu kuwa ni mzinzi na mshirikina; kisha mkaachana na akaolewa na mume mwingine, unaanzaje kuhangaika nae tena huko alikoenda? Tuwaache wapiga kura waamue kama ni sisi CCM ama UKAWA. .
.
Hata Mh. Mwenyekiti JK alishasema kila mtu ana haki kuongoza hii nchi; tunategemea kushinda lakini haitakuwa ajabu UKAWA wakitwaa madaraka kutokana na makosa yetu kimkakati. Wana CCM tusipaniki, kukomaa kisiasa ni pamoja na kuhimili na kukubali usichotarajia!
Wenu,
Mfurukutwa wa Shina.
😂😂👆
 
inawezekana alikua ktk list ya watu waliokua wanataka kununuliwa sasa akakataa ndio wana mbabaisha ili akubalia!!
 
WAKUU msikurupuke hoja ya msingi ni hii hapa kama ni kweli kwa nini asishtakiwe --->>Mapema, akisoma hati ya mashitaka, Masanja alidai kuwa Agosti mosi, mwaka 2013, katika kata ya Nguruka eneo la Rest House Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, mshtakiwa alitoa lugha ya matusi kwa Nyembo kuwa hana maadili, ana akili finyu na ni kiumbe dhaifu, kitendo ambacho kingeashiria uvunjifu wa amani. Kafulila alipotafutwa na Nipashe kuhusiana na amri hiyo ya mahakama, alisema kuwa hakwenda kortini kutokana na wakili wake kutompa taarifa za kuwapo shauri hilo kwa siku ya jana.
 
Ukiongea chochote bungeni hushtakiwi. Pale pana kinga jamani, kama hamjui msiandike chochote.
 
Hiyo habari nimeisoma on line,anashitakiwa kwa kosa la kumuita mkuu wa wilaya khadija nyembo kuwa hana maadili,pia hakufika mahakamani kwani wakili hakumjulisha.
Mleta mada ungeweka habari yote si kutunga uongo,make hata jaji welema hakuna alipoandikwa wala ishu ya escrow hakuna ilipoandikwa kwenye hiyo habari.

Usishangae inawezekana mleta mada ndiye tumbili mwenyewe!! Ripoti ya gazeti nyingine yeye anaweka ya kwake.
 
Na kwa taarifa yenu wakuu ni kwamba hakuna swhemu yenye upumbaf kama mahakamani.......
 
Back
Top Bottom