Mahakama yaamuru Kafulila akamatwe mara moja

Mahakama yaamuru Kafulila akamatwe mara moja

Mahakama yameamuru Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akamatwe na kufikishwa mahakamani mara moja kwa kosa la kumuita Jaji Werema mwizi. Aidha,Kafulila anashtakiwa kwa kuibua tuhuma za ESCROW bungeni kwa namna ambayo haikuwa sahihi kisheria.

MAONI YANGU:

Naona sasa CCM wameanza kuweweseka. Watulie sindano ziingie ili wajipange tena kurejea madarakani mwaka 2020.

========================



Chanzo: Nipashe


Mkuu nashindwa kuelewa kwani maelezo yako yanatofautiana na kiambatanishi ulichoweka toka gazeti NIPASHE.

Sasa hiyo kesi tuelewe ni ya ESCROW au lugha ya matusi.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Nimependa ushauri huu!! .
.
WANA CCM NISIKILIZENI..!!
Nina ushauri kwa wana CCM wenzangu; Lowasa kuhamia CHADEMA msipaniki. Kama kweli tulimaanisha kuwa hafai, ana uchu wa madaraka, alikiuka kanuni na maadili ya chama, ni mwizi na tena ni fisadi basi inabidi tushangilie kuondoka kwake, kwani kuvuja kwa pakacha sio ndio nafuu ya mchukuzi? Ila kama tulimkata kwa maslahi ya watu wachache na ikiwa tulitumia akili ndogo kulikata jina lake basi itabidi tujilaumu wenyewe kwa lolote tusilolitarajia litakalotokea.
Na tukiendelea kutumia akili ndogo za kudhani tutashinda kwa "magoli ya mikono", basi tunakwenda na maji mchana kweupe!
.
Tukijidanganya kuwa matusi, kejeli, mipasho, maneno ya kwenye kanga na nyimbo za Komba kwamba zitabadilisha huu upepo, pia tutajikuta tunakuwa chama cha upinzani bila hata kujiandaa kisaikolojia. Mwana CCM utakuwa unajichanganya kuushambulia uamuzi wa Lowasa kuhamia CHADEMA kwa sababu kimsingi CCM yetu ilishabariki vijana kadhaa wamshambulie majukwaani ili aonekane hafai na hao vijana wakazawadiwa vyeo. Mtu tuliemuona hafai kwetu inatuuma nini akiondoka kwetu? Ukioa mke kisha ukamtuhumu mbele za watu kuwa ni mzinzi na mshirikina; kisha mkaachana na akaolewa na mume mwingine, unaanzaje kuhangaika nae tena huko alikoenda? Tuwaache wapiga kura waamue kama ni sisi CCM ama UKAWA. .
.
Hata Mh. Mwenyekiti JK alishasema kila mtu ana haki kuongoza hii nchi; tunategemea kushinda lakini haitakuwa ajabu UKAWA wakitwaa madaraka kutokana na makosa yetu kimkakati. Wana CCM tusipaniki, kukomaa kisiasa ni pamoja na kuhimili na kukubali usichotarajia!
Wenu,
Mfurukutwa wa Shina.
😂😂👆

Maneno yako ni ya kweli na ya kishujaa lkn wana ccm husishangae wakaja na maneno kuwa wewe ni msaliti
 
unanini cha kufanya nchi isitawalike? huo uhuni wako wa kutembea na sumu mfukoni ndiyo ufanye nchi isitawalike we kiazi kweli.

Ccm mjiandae kukabidhi madaraka kwa lowasa
 
Mkuu nashindwa kuelewa kwani maelezo yako yanatofautiana na kiambatanishi ulichoweka toka gazeti NIPASHE.

Sasa hiyo kesi tuelewe ni ya ESCROW au lugha ya matusi.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Nakuaminia sana Mizambwa kwa uchunguzi
 
Hiyo habari nimeisoma on line,anashitakiwa kwa kosa la kumuita mkuu wa wilaya khadija nyembo kuwa hana maadili,pia hakufika mahakamani kwani wakili hakumjulisha.
Mleta mada ungeweka habari yote si kutunga uongo,make hata jaji welema hakuna alipoandikwa wala ishu ya escrow hakuna ilipoandikwa kwenye hiyo habari.

Kweli mkuu, mleta mada ni mshabiki tu wa upande fulani, maana contents za hiyo post aihusiani na Jaji Werema wala mambo ya tumbili na na nyani wa kuitana mwizi kati ya David na Jaji. Na kosa la kutoonekana mahakamani na kutolewa amri ya kukamatwa mbona si kiivyo inavyoripotiwa kwenye media!
 
Watanzania wamechoka na michezo michafu ya ccm na fisadi kikwete, escrow, richmond, dawasco, na kadhalika
 
Mkuu nashindwa kuelewa kwani maelezo yako yanatofautiana na kiambatanishi ulichoweka toka gazeti NIPASHE.

Sasa hiyo kesi tuelewe ni ya ESCROW au lugha ya matusi.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Mkuu mizambwa hii signature yako ina niacha hoi kinoma "mizambwa ina niuma sana" teh teh teh teh!
 
Last edited by a moderator:
Watanzania tunatia aibu, Hata kuisoma habari hujaisoma unaanza kuandika comments.
Page ya nne hii sasa na bado mnaamini upuuzi mnaoaminishwa?
 
Mizambwa sijui kitu gani, najaribu kusema kwamba watu hata kama utafanyaje wamechoka saiv niwakati wa transition kwahio jambo lolote linalo husu ccm ni mwiba kwa wataka mabadiliko
 
Kabila la nin tena ndugu yangu sindicate ningefurahi kama maisha ya kila mtanzania yangekua kama yangu ila katika utawala wa ccm haiwezekani kabisa
 
Back
Top Bottom