Mahakama ya Rufaa yabatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu kesi ya dhamana ya makosa makubwa

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,137
2,000
Katika hukumu iliyotolewa leo tarehe 5 Agosti, 2020, Jopo la Majaji watano wa Mahakama ya Rufani limekubaliana na Serikali kuwa kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai ,Sura ya 20 ya Sheria za Tanzania kinachozuia dhamana kwa makosa makubwa ya jinai yakiwemo mauaji, uhaini, na utakatishaji fedha haramu, unyang’anyi wa kutumia silaha, usafarishaji haramu wa Madawa ya Kulevya nk, hakikinzani na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977kama ambavyo Mahakama Kuu ilivyoamua tarehe 18 Mei, 2020 katika Kesi iliyofunguliwa na Wakili wa kujietegemea Bw. Dickson Paulo Sanga Dhidi ya Mwanasheria Mkuu.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umefutwa na kwa maana nyingine, kifungu hicho kinachozuia dhamana ambacho Mahakama Kuu ilielekeza kifutwe kwenye Sheria husika kitaendelea kubakia na kwa kuwa kinazingatia matakwa kwa kikatiba na hakikinzani na Ibara ya 13(3) wala Ibara ya 15(1)na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama kilivyodaiwa na Wakili Sanga katika kesi yake Mahakama Kuu.

Mahakama ya Rufani ileeleza kuwa, kwa kuzingatia Ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, haki ya mtu ya kulindwa na Katiba haipaswi kuingilia haki na uhuru wa watu wengine. Hivyo, mtu anaponyimwa dhamana haimaanishi kuwa haki yake ya Kikatiba ya kuwa huru imekiukwa bali kwa kuwa anatuhumiwa kwa makosa makubwa yenye kuhatarisha usalama wa nchi na uhai wa watu wengine, ni wajibu wa Serikali pia kuhakikisha kuwa mtu huyo anazuiwa ili asiweze kusababisha madhara kwa jamii.

Mahakama imeona kuwa, hata kama mtu atakosa dhamana, Sheria inatoa haki ya yeye kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana ha hivyo, sio sahihi kuamua kuwa haki ya mtu inakiukwa na kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Mahakama imetahadharisha kuwa, matendo yanayohusu utekelezaji wa shaeria kwa mfano watu kuendelea kuwekwa ndani pasipo kufikishwa Mahakamani yasiusishwe na utekelezaji wa kufungu cha kifungu cha 148(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanya Mahakama Kuu kwa kuwa matendo hayo yanaweza kulalamikiwe kwa utaratibu mwingine wa kisheria badala ya kufuta kufungu cha Sheria.

Uamuzi huo umetolewa na Waheshimiwa Majaji i Jaji . Stella Mugasha, Dr. Gerald Ndika, Jacobs Mwambegele,Mwanaisha Kwariko na Ignas Kitusi.

Mahakama imeeleza kuwa haitakuwa sahihi kwa mtu anayetenda uhalifu wa makosa makubwa kudai haki ya kikatiba bila kuzungatia dhana pana na mahsusi ya Katiba ya kulinda jamii nzima,. Mahaka imesema kuwa Haki za kikatiba ni lazima zitafsiriwe kwa mapana yake na sio kwa kuangalia kifungu kimoja kimoja.

Waliowakilisha Serikali katika kesi hii ya Rufaa Na. 175 ya mwaka 2020, Mwanasheria Mkuu dhidi ya Dickson Paulo Sanga ni aliyekuwa wakili wa Serikali, Dk. Clement Mashamba, Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali bw. Biswalo Mganga, Wakili wa Serikali Mkuu Bw. George Mandepo, Alesia Mbuya, Tumaini Kweka, Faraja Nchimbi, Abubakari Mrisha na wakkli wa Serikali Bi. Narindwa Sekimanga.

Kwa upande Mjibu Rufaa ambaye ni Dickson Sanga, yeye aliwakilishwa na Mawakili Mpale Mpoki, Jonathan Mbuga na Jebra Kambole.

TAZAMA UAMUZI HUO WA MAHAKAMA HAPA CHINI
 

Attachments

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
399
1,000
Mahakama ya rufaa Tanzania imetengua uamuzi wa awali wa mahakama kuu na kusema makosa yaliyo chini ya kifungu cha 148 (5) ya CPA mfano Makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha yaendelee kuwa hayana dhamana.

Rufaa hii inapinga uamuzi wa Mahakama kwenye Shauri la Madai Namba 08 la 2019 ambapo Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam ilimpatia ushindi Bw. Sanga mnamo Tarehe 18 Mei 2020.

Mahakama Kuu iliiagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha kifungu hicho ndani ya miezi 18 kutoka siku ya kutolewa kwa hukumu huku ikiionya Jamhuri kuwa kushindwa kufanya hivyo kutasababishwa kufutwa.

Uhujumu.jpg
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,965
2,000
Sio sahihi kuwapa dhaamana majambazi na wauaji.
Utamtambua vipi mtu ni jambazi kabla mahakama haijamkuta na hatia?

Kumbe ndio maana mnawashikilia mahabusu miaka mingi kwasababu tayari mnaamini hao watuhumiwa ni majambazi!

#Lissu2020.
 

Nsoji go Nvaa

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
381
1,000
CCM wameharibu mifumo ya utoaji haki nchi hii unaeza kuta huyo aliyehukumu hilo shauri anajiandaa kutia Nia uchaguz ujao kupitia ccm
 

stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,481
2,000
Utamtambua vipi mtu ni jambazi kabla mahakama haijamkuta na hatia?

Kumbe ndio maana mnawashikilia mahabusu miaka mingi kwasababu tayari mnaamini hao watuhumiwa ni majambazi!

#Lissu2020.
Wewe unafikiri ambaye anafahamu au kusikia flani ndiye kamuua ndugu yake atamuacha tu jamaa awe anatembea kwa uhuru kusubiri hukumu??

Tumia akili kidogo na sio mihemko uliyonayo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom