Mahakama ya Rufaa mfumo wenu mpya ni kikwazo

activist

Senior Member
Jan 3, 2014
151
178
Tangu jana Mahakama ya rufaa imeanza kutumia mfumo wake mpya wa ku file kesi online. Mfumo huu umekuwa kikwazo na pia unaflchelewesha mashauri. Mfano kwa kesi ambazo ni za rufaa kutoka mahakama kuu mfumo huu haujaanza kuzipokea.

Ukienda pale ku file rufaa yako wanakuambia uache namba ya simu then siku mfumo ukiwa sawa watakupigia ili uweze ku Lodge rufaa yako. Mfumo huu unapokea applications peke yake nazo pia kwa tabu.

Nawashauri mamlaka kama bado mambo hayajakaa sawa tuendelee na mfumo wa zamani watu wasajili rufaa zao na kuzilipia then mfumo ukilaa sawa basi utumike. Kuliko hivi sasa wananchi wanavyoteseka na kucheleweshewa mashauri yao kusajiliwa.
 
20231109_101459.jpg
 
Back
Top Bottom