Mahakama ya Kadhi: Masheikh wakutana na JK

Angalau Jk katuonyesha njia, kwamba adui wetu sio ccm ni kanisa. kwani ccm ilifata kauli ya kanisa ili mahakama ya kadhi isipate pesa kutoka serekalini(kama nimemnukuu jk nisamehewe)
Badala ya kumlaumu Kikwete aliyewatapeli unalilaumu Kanisa, MIISLAM NDIVYO ILIVYO!
 
Hii kitu inanishangaza sana , waliotoa ahadi ya mahakama ya kadhi ni CCM tena chini ya campaign za JK mwenyewe.
Leo hii JK ameshapata alichokitaka , amewakana mchana mkweupe , mnaanza kuwalalamikia mapadre na CDM,
hivi ni lini jamaa tutaachwa kutumiwa kizembe namna hii ?
Sijui ni kwamba hamjui kudai au nini ?
JK na CCM si wapo , wafuateni mkawaulize wanamaanisha nini ? au ni dharua ? La sivyo mnatalalamika milele
 
Angalau Jk katuonyesha njia, kwamba adui wetu sio ccm ni kanisa. kwani ccm ilifata kauli ya kanisa ili mahakama ya kadhi isipate pesa kutoka serekalini(kama nimemnukuu jk nisamehewe)

Hii kali ndo maana mnatukanwa hamna akili hivi hivi, huyu jamaa si mlimchagua ili awaletee mahakama ya kadhi!
 
Sioni sababu ya kuendelea kujadili suala hili kwa sababu haiwezekani kugeuza masuala ya dini kugharimiwa na Serikali.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
kasema wenzenu waliomba wakapewa. Waislam wanaomba pesa za mahakama ya kadhi . Makanisa hayataki. Sijui udugu wetu unatokea wapi tena hapa. Bora niishi na wakiristo wa kizungu kuliko watz wenzangu
.

hao si ndio watakuchinja na kukuzika baharini ..... bora hawa wa kibongo wanahuruma
 
Mkuu Ivuga hawajaipinga hiyo mahakama ya kadhi bwana.... ila wanachopinga ni GOVERNMENT FUNDING. Endapo Waislam wataiendesha kwa fedha zao wenyewe Christians has nothing to do with it.
wakristo kuipinga mahakama ya kadhi ni kueneza udini...
 
kasema wenzenu waliomba wakapewa. Waislam wanaomba pesa za mahakama ya kadhi . Makanisa hayataki. Sijui udugu wetu unatokea wapi tena hapa. Bora niishi na wakiristo wa kizungu kuliko watz wenzangu
.

Ombeni fedha za kujenga shule, vyuo na hospitali mtapewa. Mahakama jichangisheni wenyewe.
 
unajua kuwa serikali inalipa kanisa fungu kila mwaka? Huu sio udini?
Wake up!!! Hapa serikali imeteleza sana isifikiri kuwa waislamu ni wajinga

Hii ndo Sampuli ya Waislamu tulio nao jamvi hili limejitahidi sana kukuelewesha ila nadhani kuna majibu unayohitahi manake sijui ni kwamba wewe si muelewa au umetumwa humu. Labda nikujibu hivi hayo uyasemayo kwamba Serikali inalipa kanisa weka ushahidi mezani ili watu waweze kuchangia hilo, lakini pili umeshaambiwa serikali haina dini, Leo ninyi mtataka Mahakama ya KADHI, kesho Wakatoliki nao watataka mahakama yao vivyo hivyo kwa Walutheri, Waanglikan, Wapentekoste na wengine wengi hii itakuwa nchi gani??? Embu kaa na wenzio jadilini mambo ya msingi ya nchi hivi mbona mnalalama tuuuu kila kukiwa leo?? Rais wa nchi wenu yeye kesha waambia cha kufanya bado tu.... Kwanza contribution yenu kwa Taifa hili ni nini kama sio uchochezi usio na mantiki.... Wakati wenzenu wanafikiria kuongeza Mahospitali, Vyuo, na Taasisi nyinginezo nyingi nyie endeleeni na Mahakama ya Kadhi na kuunga wali kwa nazi kama hamtabakia hapo mlipo mpaka Mtume anarudi.....
 
Haiwi lengo zuri la Mwenye akili KUTUKANA;bali kuelimisha,kufafanua,kutafakari,na kuzingatia,nawmd kuwa tayari kufanyiwa hayo.Mimi ni Muislam(Mungu shahidi).Napenda sie Waislam tuwe na Maendeleo km binadamu wenzetu Wakristo, lakini ni vigumu na zifuatazo ni kwa nini tuko hivyo;

KWa muda mrefu Uislam ulikuwa mbele kwa kila nyanja ya maisha,lakini mapambano kati ya faith na reasoning yaliasisi muanzo wa Waislam kuwa nyuma.Kugundua baadae,kupitia kwa Waislam,kuliwafanya Wakristo(wazungu)waishinde Imani yao(Ukristo) na Logic kushinda(mwanzo mkubwa wa Maendeleo ya kizungu).

Tatizo la sasa la Waislam nchini,na kote duniani ni mlolongo wa Historia hiyo,na hasa Ukoloni uliopendelea upande mmoja wa Ukristo(ni suala la Mjadala mpana hapa,Ukizingatia chuki,ushindani wa imani hizi mbili.

Ingawa wapo wengi wasemao kuwa Ukoloni ulizidi mno ktk Chuki).Kwa Upande wa Waislam,wanazuoni wake wamesema;kuachwa kwa Sunna sahihi ya Mtume(s.a.w) kulikua, na ndio Chanzo cha Matatizo yote;huku Wanazuoni wa kimagharibi wakisema kuwa ni kukataa mabadiliko(Conservatism) kuwa ndo cha matatizo ya Waislam.Ukweli kiasi fulani;Dini ilichangia,kitu ambacho wenzao wa Ulaya baadae walikiepa(Wakafanikiwa).

Matatizo ya sasa ya Waislam ni zao la Umbumbu wa dini yao kwa usafi wake(sunn) na kubaki njid panda na kuendekeza Uhuni,njaa na Maslahi ya Bakwata(Watu ambao hawatafika mbali na hiyo Mahakab ya Kadhi.

Na endapo Waislam hawaamki,tusitaraji lolote kutoka kwetu,Waislam;Allah Yaalam.Tafakarini mchango Angu na nakaribisha maoni.Ahsanteni.
 
Waislam tuchape kazi, malumbano na fikra potofu ndivyo vinaturudisha nyuma. Hata ukiangalia mikoa ya waislam wengi nje ya Dar iko nyuma kimaendeleo. Mfano: Tabora, Lindi, Mtwara na Kigoma.
Sina tatizo na kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ili kukidhi kile wanachoita kuwa ni ibada yao. Tatizo langu ni kuihusisha serikali katika mchakato wa kidini. Kwanini serikali ihusishwe katika mambo ya ibada ya kundi fulani la watu? Ndugu zetu Waislam hupenda sana kulalamika na huku wakijua kuwa wasemalo sio kweli. Sijawahi kusikia serikali imechangia katika kuendesha shughuli za kidini kwa wakristo kama wanavyodai ndugu zetu hawa. Kinachodaiwa kuchangiwa na serikali kwa wakristo ni taasisi za elimu na afya. Elimu na afya ni haki ya kiala mtanzania bila kujali itikadi yake. Wao waislamu wanajenga misikiti, hawajengi mashule na mahospitali ili wapewe ufadhili na serikali kama ilivyo kwa taasisi za kikristo. Kazi ya serikali ni kuhakisha watu wake wanapata elimu na matibabu bila kujali yanatollewa na mtu binafs, taasisi zai dini au serikali yenyewe. Serikali haishirikii katika ibada ya wapagani, wahindu, waislamu au wakristo. Mahakama ya kadhi ni sehemu ya ibada kwao na wamesema wao. Iweje serikali ishiriki katika hilo? Kwanini kodi zetu ziende kuendesha ibada za waislamu pekee? Basi walipa kodi wote watadai hivyo. Wakatoliki wanayo mahakama yao. Anaependa kuifuatlia yuko huru na haigharimiwi na serikali. Labda tuulize chuo cha Kiislamu cha morogoro wanafunzi wake wanabaguliwa katika mikopo na bodi ya Mikopo kwa kuwa tu wanasoma kwenye chuo cha waislamu? Labada watatujibu.
 
Nafikiri hili swala lipo wazi kwamba ili kuweka usawa, serikali haitakiwi kujiingiza kugharimia au kuendesha mambo yanayohusu ibada za kidini. Ndiyo maana wakristo wanajenga makanisa yao na kugharimia mafundisho kwa waumini wao kwa pesa zao wenyewe, hali kadhalika, waisilamu wanajenga misikiti na kugharimia mafundisho kwa waumini wao kwa pesa yao wenyewe. Sasa kama suala la mahakama ya kadhi ni ibada kwa ajili ya waisilamu, inakuwaje serikali ilazimishwe kuianzisha na kuigharimia. Hapa kuna walakini.
 
Kimsingi serikali haina dini hili Suala la mahakama ya kadhi walishughulikie waislamu wenyewe, Pia Serikali lazima ikae na mashekh kujadili na kujua sheria watakazoweka ili kuona kama zinaendana na utaratibu wa nchi yetu vinginevyo isije kuwa kama wenzetu waarabu wanapojitoa muhanga kwani ile ni imani ya dini ya Kiislam
 
kama haina dini kwa nini -Katoliki wanapewa fungu na serikali? Kwa nini kama wanatoa huduma za jamii wasitoe tu kama kanisa? Kwa nini wameingia gentlemen mkataba na serikali ambayo haina dini? Serikali na maaskofu hapa wameteleza kuwanyima waislamu mahakama ya kadhi kama walivyotaka na huu udini wakristo ndio wanauanzisha wenyewe

Pumba tu. Hamna mengine ya kujadili????
 
Waislam ndivyo walivyo waonyeshe hata kimoja walichofanya kikafanikiwa,nasubiri hizo hukumu za mahakama kadhi,kuchapwa viboko 8
pale mwenge au posta hakuna kuvaa suruali kwa wanawake,ni vituko vitupu!uwezo wa kuchanganua mambo kwa ndugu zetu waislam una walakini.
 
Mimi ni mkristo, pilipili hii inaniwasha kwa kuinunua (kutumia kodi yangu) na si kuila (hainihusu)! National Bank of Commerce walipoingiza upuuzi wa Islamic Banking nilifunga account yangu instantly na kuelekea Mkombozi.


lol... kwani walitoa tamko kwamba wateja wote watatakiwa wa switich account zao ziwe kama za waislamu..

tehetehetehe....
 
Solution is simple mzee subiria waislamu waanze kugoma kulipa kodi kwa madai wanataka kodi yao ijulikane inaenda wapi ndio mtalijua jiji kama hamjatokwa na macho maana mmezoea vya bure.
Kodi mtatoa kama kawaida bwana mdondoaji. mtabaki kulalama kiila siku badala ya kuwapeleka watoto wenu shule.
 
kama haina dini kwa nini -Katoliki wanapewa fungu na serikali? Kwa nini kama wanatoa huduma za jamii wasitoe tu kama kanisa? Kwa nini wameingia gentlemen mkataba na serikali ambayo haina dini? Serikali na maaskofu hapa wameteleza kuwanyima waislamu mahakama ya kadhi kama walivyotaka na huu udini wakristo ndio wanauanzisha wenyewe
Linganisheni tu!! Lakini tunataka vile vile mahakama ya kadhi ihudumie watanzania wote kama huduma za mashule na mahospitali ya wakatoliki serikali inavyochangia kwa ajili ya raia wote.!!!
 
Tunarudi kule tulikotoka zamani sana

Jina Lako____________
Umri wako___________
Kabila lako___________
Dini yako____________
 
ok
..nimekubali ..je na hii mahakama itakupunguzia kitu gani?
ofcourse hiyo mahakama haitapunguza jambo lolote kwa hayo yaliyotajwa hapo juu. wakristo hatuna tatizo na nyie waislamu kuanzisha hiyo mahakama kwa sababu ni suala la imani yenu kwa faida yenu. tatizo ni pale mnapoishinikiza serikali hilo suala liwe kwenye katiba ya nchi, hapo ndipo panapozua utata!! kwa nini suala la kiimani kama hilo liwekwe kwenye katiba, bila ridhaa yetu sote??
 
Back
Top Bottom