Masheikh sita walioshinda tuhuma za Ugaidi, wanashikiliwa na Polisi tena

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MASHEIKH WALIOACHWA HURU NA MAHAKAMA KUU JANA IJUMAA IMEFAHAMIKA WANASHIKILIWA NA POLISI

Masheikh sita walioshinda tuhuma za Ugaidi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana tarehe 01/12/2023, wako mikononi mwa Jeshi la Polisi.

Jana walichukuliwa Mahakamani na kulazwa mahabusu ya kituo cha Kati jijini Dar es Salaam.

Taarifa za uhakika leo pia na kesho watalazwa katika mahabusu za Jeshi hilo.

Shura ya Maimamu ilipo mhoji mmoja wa Askari katika kituo hicho kuhusu kosa la watu hao alisema yeye hafahamu na kukiri kuwa watu hao amewaona katika kituo hicho.

Tukio hili linathibitisha mfumo wa sheria usio eleweka Tanzania ambao unatoa fursa kwa askari kutoa adhabu kwa raia bila ya kuwepo hukumu ya Mahakama iliyomtia hatiani raia huyo.

Watu hawa ambao jana wameanza kutumikia adhabu hiyo (ya mahabusu za Polisi), wamekaa gerezani zaidi ya miaka tisa na hatimaye jana walishinda tuhuma za ugaidi dhidi yao Mahakamani.

Shura ya Maimamu Tanzania inaendelea kufuatilia kushikiliwa watu hao na Polisi na itatoa taarifa ya kinachoendelea.

KATIBU MKUU SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
 
Swali, je wameacha kuunga mkono jitihada za magaidi?
 
Back
Top Bottom