Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kutoa hukumu kupinga kuondolewa Wamasai Loliondo Juni 22, 2022

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,272
Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Juni 22/06/2022inatarajia kutoa hukumu dhidi Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania katika kesi ya mwaka 2017 iliyofunguliwa na vijiji vya Loliondo wakipinga kuondolewa katika maeneo yao.

Hukumu hiyo itatolewa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo, Monica Mugenyi.

A61B88AD-C5D9-41BF-899F-AC27610C070D.jpeg
 
Hiyo mahakama haina mamlaka ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya hiyo kesi sababu ni kwamba kesi ya msingi haijasikilizwa kwenye mahakama za ndani kama mahakama kuu na mahakama ya rufaa, jambo la msingi la kuondolewa wananchi wa kimasai mbugani ni kulinda mazingira ya hifadhi yasiharibiwe na kuwa ni kwa manufaa ya umma(Public interests)
 
Eti umma.. ...umma ni nani?
 
Kummilikisha mwarabu ndio kulinda mazingira jinga wew? Uharibifu ulofanywa na mmasai ni upi tuambie
 
Upumbavu mtupu. Wakati wakenya wanawaondoa raia wao kule katika hifadhi yao na kupelekea askari mmoja kupigwa panga la mkono, mahakama hii na hawa watetezi uchwara wa haki za binadam walikuwa wapi?

Usipaniki mkuu. Umetoa taarifa yako bila kusema kama huko Kenya kulikuwa na kesi katika mahakama hii hii ili tuone iliamuaje. Kama hakukuwa na kesi katika mahakama hii, mfano wako hauna maana kwa sababu mahakama hushughulika na mashitaka yaliyofungiliwa katika mamlaka yake!

Hata hivo, sioni mahakama hii ikiamua in favour of wamasai kwa sababu sheria za Tanzania, ardhi haimilikiwi na raia bali serikali na mmiliki ni mamlaka ya Rais.
 
Hiyo mahakama haina mamlaka ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya hiyo kesi sababu ni kwamba kesi ya msingi haijasikilizwa kwenye mahakama za ndani kama mahakama kuu na mahakama ya rufaa, jambo la msingi la kuondolewa wananchi wa kimasai mbugani ni kulinda mazingira ya hifadhi yasiharibiwe na kuwa ni kwa manufaa ya umma(Public interests)

Unadhani EA Court of Justice ni moja ya mahakama za member states zenye appellate jurisdictions?

Hii ina special mandate yake chini ya EAC Treaty. Ina concurrent human rights jurisdiction. Inao uwezo wa kusikiliza human rights disputes hata kama mahakama za member state husika hazijazisikiliza!
 
Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Juni 22/06/2022inatarajia kutoa hukumu dhidi Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Tanzania katika kesi ya mwaka 2017 iliyofunguliwa na vijiji vya Loliondo wakipinga kuondolewa katika maeneo yao.

Hukumu hiyo itatolewa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo, Monica Mugenyi.

View attachment 2266552
Salary la loliondo na ngorongoro siyo suala la kufanyia ushabiki wa kisiasa bila kufanyia uchunguzi wa kina,wanaopinga eneo la km2 za mraba 1500 ambayo inahifadhi kwa ajili ya masalia ya wanyama ni wamasai wa Kenya ambao wamefanya lile pori kama la kwao kwa manufaa ya hawana maumivu yoyote hata likiharibika watanzania wengi hawajaliona hili hata ndugu zangu CHADEMA ambao niliwaamini kuwa wanaweza kuchambua mambo kwa umakini nao wamejiingiza kwenye mtego wa maslahi binafsi
 
Usipaniki mkuu. Umetoa taarifa yako bila kusema kama huko Kenya kulikuwa na kesi katika mahakama hii hii ili tuone iliamuaje. Kama hakukuwa na kesi katika mahakama hii, mfano wako hauna maana kwa sababu mahakama hushughulika na mashitaka yaliyofungiliwa katika mamlaka yake!

Hata hivo, sioni mahakama hii ikiamua in favour of wamasai kwa sababu sheria za Tanzania, ardhi haimilikiwi na raia bali serikali na mmiliki ni mamlaka ya Rais.
Ok mkuu.
 
Back
Top Bottom