Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Mahakama Kuu ya Zanzibar imeyatupa maombi madogo ya dharura yaliyowasilishwa na wagombea wa ACT Wazalendo wa Uwakilishi kutoka Majimbo17, yaliyolenga kuzuia Wasimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu kuchomaaukuharibu nyaraka za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Uamuzi huo umetokana na hoja ya upande wa Serikali kuwa Viapo(Affidavits)vilivyotumika vilikuwa na kasoro ya kiufundi, kwa madai kuwa MkuuwaViapo(Commissioner for Oaths) Wakili Ussi Khamis Haji, hakuwa amehuishaleseni yake ya mwaka 2026.
Akieleza masikitiko ya ACT Wazalendo katika taarifa aliyoitoa leo 13 Februari, 2026, Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma Salim A. Bimani, amesema kuna haki dhidi ya ufundi (Technicalities).
“ACT- Wazalendo inasikitishwa na mchezo wa "paka na panya" unaofanywa naupandewa Serikali. Ni dhahiri kuwa, Serikali inatumia nguvu kubwakupataushindi wa kiufundi (technicalities) badala ya kuruhusu Mahakamakusikiliza kiini cha hoja (merits) za maombi yetu.
“Jitihada za kuzuia usikilizwaji wa mashauri hayazinaashiria hofu kubwa juu ya kile ambacho nyaraka hizozitafichuakuhusu uadilifu wa Uchaguzi wa 2025. Sheria haipaswi kutumika kama kichaka chakuficha ukweli. Tunasisitiza kuwa haki ya wananchi kujua ukweli,” amesema.
Kutokana na hali hiyo, Bimani amesema wamemerudi Mahakamani kwa kasi Zaidi na hawaruhusu wapinzani wao kupumua wala kudhani wameshinda.
“Dakikachache baada ya maombi hayo kuondolewa, tayari tumeshafungua upyamaombi hayo (Fresh Application) kwa Hati ya Dharura katika Mahakama Kuu yaZanzibar, yakisajiliwa kama Maombi Madogo nambari 19 ya Mwaka 2026tukiwatumerekebisha kasoro zote zilizodaiwa.”
Wamewatoa hofu wanachama wao, akisema chama hicho kimejipanga kuvuka kila kizingiti cha kisheria kitakachowekwa mbele yao.
“Hatutaruhusu hata karatasi moja ya kura ipotee au kuchomwa moto mpakapalehaki itakapopatikana. Tumejipanga kisheria, tumejipanga kisiasa. Hatuishii kwenye makaratasi, tunalinda heshima ya mpiga kura wa Zanzibar,” amesema.