Mahakama Kuu Zanzibar yaamuru Cryprian Musiba kumlipa Fatma Karume Tzs 7.5 bilioni

Huyo Misiba angekuwa mpinzani hiyo hukumu ingekuwa na maana, na kesi iwe imefanyikia huku Bara. Hakuna mwanaccm anatii amri ya mahakama, hasa mwenye haki anapokuwa mkosoaji wa serikali.
Na tusubiri tuone. Muda ndio muamuzi wa mwisho.
 
Pacha, Cyprian Musiba akishindwa kulipa hio hela yatapelekwa maombi mahakamani ya;

1) kukamata mali zote za Gazeti na za kwake binafsi ziuzwe ili alipwe Fatma Karume.

2) Kufungiwa account zake na za Gazetti zote za bank, pesa zilizomo kulipwa kwa Fatma Karume.

Deni lisipowezekana kulipwa kabisa kutokana na mali kutofikia kiasi anacho daiwa, basi maombi ya kumfunga yanaweza kufanywa mahakamani (Civil Jail Term, sio Criminal Jail) na kama maombi yatakubaliwa na mahakama basi itapigwa hesabu ya deni na kifungo atakachotakiwa kufungwa kwa gharama za Fatma Karume (Yani Fatma Karume atakua akimhudumia lishe yake Cyprian Musiba kwa kipindi chote atakachofungwa).

In short, Cyprian Musiba safari hii anaweza akatolewa marinda.
Lihove2
 
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Wakili msomi, Fatma Karume aka Shangazi, ameandika hivi;

Hamjambo? Mnaomjua Cyprian Musiba mwambieni Mahakama Kuu ya Zanzibar, ndio pale VUGA, yametoa HUKUMU leo. Yamesema ni yeye na GAZETI lake wameandika UONGO dhidi yangu.
Sasa anatafute 7.5 billion za kunilipa!. Namshukuru sana Advocate Wangu!.

Billion 7.5 ilihali sponsor ameshakufa na kwa upande mwingine biashara zake zimemuendea kombo hadi kushindwa kuwalipa Wafanyakazi mbona atajua hajui!.

Watu wa karibu wa Musiba mnaweza kumpa hizi habari maana ni kitambo hatujamuona huko Twitter republican huyo aliyekuwa "Mwanaharakati huru" wa kumtetea hayati Magufuli.
😂😂🤣🤣🤣
 
Hivi mtu kama Musiba ni wa kumfungulia kesi nadhani ni wa kuupzwa ! Ukichaa wake ni wa hali ya juu tu!
 
Ile ya Mdude na akina Mbowe kurudishiwa hela ilikuwa ya nini?

Fuatilia kama kuna popote wamerudishwa hiyo hela. Hakuna mahali wapinzani wanatekelezewa Hizo haki kwa maana ya haki kutokana na sheria inavyotaka.
 
Fuatilia kama kuna popote wamerudishwa hiyo hela. Hakuna mahali wapinzani wanatekelezewa Hizo haki kwa maana ya haki kutokana na sheria inavyotaka.
Ya Mdude vipi? Kwani hiyo hela ikirudishwa huwa inatangazwa kwa kila mtu? Sidhani kama sheria za fedha zinataka hivyo
 
Ya Mdude vipi? Kwani hiyo hela ikirudishwa huwa inatangazwa kwa kila mtu? Sidhani kama sheria za fedha zinataka hivyo

Narudia tena, hakuna popote serikali inatekeleza hukumu za hivyo, labda uwe na uwezo wa kukamata mali za serikali, kama yule mzungu aliyekamata ndege huko nje.
 
Narudia tena, hakuna popote serikali inatekeleza hukumu za hivyo, labda uwe na uwezo wa kukamata mali za serikali, kama yule mzungu aliyekamata ndege huko nje.
Haupo sawa Mkuu, endelea kujitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom