Mahakama Kuu Zanzibar yaamuru Cryprian Musiba kumlipa Fatma Karume Tzs 7.5 bilioni

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
242
450
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Wakili msomi, Fatma Karume aka Shangazi, ameandika hivi;

Hamjambo? Mnaomjua Cyprian Musiba mwambieni Mahakama Kuu ya Zanzibar, ndio pale VUGA, yametoa HUKUMU leo. Yamesema ni yeye na GAZETI lake wameandika UONGO dhidi yangu. Sasa anatafute 7.5 billion za kunilipa!. Namshukuru sana Advocate Wangu!.

Billion 7.5 ilihali sponsor ameshakufa na kwa upande mwingine biashara zake zimemuendea kombo hadi kushindwa kuwalipa Wafanyakazi mbona atajua hajui!.

Watu wa karibu wa Musiba mnaweza kumpa hizi habari maana ni kitambo hatujamuona huko Twitter republican huyo aliyekuwa "Mwanaharakati huru" wa kumtetea hayati Magufuli.
 
Back
Top Bottom