Mahakama Kuu yadai hakuna ushahidi wa Serikali kufungia Mtandao wa Clubhouse

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,515
8,414
1000017977.png

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam iliyosikiliza shauri la kikatiba dhidi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema hakuna uthibitisho kuwa Serikali ndio iliyozuia kupatikana kwa mtandao wa Club House.

Mtandao huo uliojipatia umaarufu mkubwa nchini ukitumika katika mijadala mbalimbali ikiwamo ya kisiasa na matukio mazito, ulianza kutopatikana nchini Agosti 2023 na kumekuwa na hisia kwamba ni Serikali ya Tanzania kupitia TCRA ndio imezuia upatikanaji wake.

Mtandao huo kwa sasa hupatikana tu pale ambapo mtumiaji amepakua programu ya Virtual Private Networks (VPN), programu ambazo nyingi ni za kulipia, sio za bure na kwa sheria za Tanzania, mtumiaji atalazimika kusajili VPN anayoitumia.

Hata hivyo, jopo la majaji watatu, Fredrick Manyanda, Dk Ubena Agatho na Dk Angelo Rumisha katika hukumu yao waliyoitoa Mei 3, 2024, wamesema mikataba ya kimataifa imetoa haki ya upatikanaji wa habari, lakini haki hiyo ina mipaka kwa mujibu wa sheria.

Katika kesi hiyo namba 27860 ya mwaka 2024, mdai Paul Kisabo, alimshitaki Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari kama mdaiwa wa kwanza, TCRA kama mdaiwa wa pili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania (AG) kama mdaiwa namba tatu.

Kisabo ambaye katika shauri hilo alijitambulisha kama mtumiaji mzuri wa mtandao wa Club House, alieleza kuwa kuzuiwa kutumia Club House kunakiuka Katiba ya nchi ya mwaka 1977 na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

Katika hukumu yao kwenye hoja ya kuzuia upatikanaji wa Club House, majaji walisema mdai alisema mdaiwa namba mbili ambaye ni TCRA ndiye mwenye dhamana ya usimamizi wa mitandao, ndiye anayehusika kufanya Club House isipatikane Tanzania.

Mdai aliegemea kwenye ripoti ya OONI inayosema kuwa kuanzia Agosti 13, 2023, TCRA imezuia upatikanaji wa Club House lakini majaji wakasema baada ya kuipitia na kubaini ripoti hiyo sio hitimisho kwa kuwa inazungumzia kushuku kuwa Club House imezuiwa.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom