Mahakama Kuu yabatilisha Vifungu vya Sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi

Safi sana!

Kiburi cha Jiwe sasa kitapungua.

Ni imani yangu mahakama itakuwa imetamka kuwa vifungu hivyo ni kinyume na katiba na kuagiza vifutwe/virekebishwe.

Ushauri:
Serikali/Bunge wasipotekeleza amri hii mpaka tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwakani,nashauri wapinzani waiombe Mahakama izuie uchaguzi mkuu unaokuja mpaka pale amri hii halali ya Mahakama Kuu itakapotekelezwa.
AG ataenda court of appeal kama alivyofanya kwa Nondo!
 
Itawapa nafuu wakurugenzi....maana kuna maeneo walikuwa wanapata tabu sana kubebe mizigo isiyobebeka....plus mkwara juu kutoka kwa J.we
Sio Jiwe tu. Hata Katibu Mkuu wa Chama au wale wanaojiita "wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa" nao these days wamejipa mamlaka ya kumshurutisha Mkurugenzi apindue matokeo kwa ahadi ya kulindwa kwa gharama yoyote
 
View attachment 1093388
Mahakama Kuu (Dar) imebatilisha vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi.

Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2018, ilifunguliwa na Bob Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo, Bob Chacha Wangwe aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Fatuma Karume, anapinga Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Anadai kuwa hiyo ni kinyume cha Ibara ya 74 (14 ) ya Katiba ya Nchi ambayo inapiga marufuku kwa mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kwamba ana haki ya kupiga kura tu.

Aidha, alidai kuwa wakurugenzi hao ni wateule wa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

SHERIA INASOMEKAJE?

View attachment 1093398

Mwezi Juni 2018, akiwa Bungeni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, alisema Mbunge yeyote anayeona kuwa si sahihi Wakurugenzi wa Halmashauri kutosimamia uchaguzi, apeleke hoja Bungeni ili sheria hiyo ibadilishwe.

Mkuchika aliongeza kwa kusema “Tunayo Mahakama, pale ambapo mtu anaona hakutendewa haki aende Mahakamani,”

Ilikotoka:

Baadhi ya mijadala ndani ya JamiiForums:

2016

Julai 2018:

NEC wenyewe walishaona haya:

2016

2014
Rais yuko juu ya sheria mahakama kaiweka mfukoni wala hatajali hukumu hiyo
 
Sasa wameula kwa chuya na uchaguzi ndiyo huuuooo wa serikali za mitaa
Sio Jiwe tu. Hata Katibu Mkuu wa Chama au wale wanaojiita "wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa" nao these days wamejipa mamlaka ya kumshurutisha Mkurugenzi apindue matokeo kwa ahadi ya kulindwa kwa gharama yoyote
 
MaCCM yatatokwa mapovu kama yametafuna majani ya magimbi
Daudi Mchambuzi hebu kuwa na busara kidogo. Hivi unadhani wale wabunge wote wa upinzani waliopita kwa kura nyingi nani alikuwa msimamizi wa uchaguzi na ni nani alitangaza matokeo?? Hapo ndiyo ujue kuwa suala si kusema eti kura zinaibiwa. Ukweli utabaki pale pale kuwa CCM inakubalika sana tena sana hata akija nani kusimamia uchaguzi CCM lazima ishinde kwa kishindo, na kishindo hicho chaja tena 2020 na 2025, 2030, 2035, 2040, 2045, 2050, 2055, 2060, 2065, 2070, 2075, 2080, 2085, 2090, 2095, 2100 ...... ni CCM tu!
 
Hakuna kitu kama hicho

Tanzania hakuna Judicial Review, yani nguvu ya mahakama kubatilisha sheria, ikafa hapo hapo. Ambacho ndio maana ya neno la Kiswahili "batilisha."

Katiba inasema mahakama nguvu yake inaishia kulinasihi bunge hii sheria imevunja katiba, do something ( rekebisha, futa, fanya ufanyavyo...)

Na haitakiwi kuzidisha: hakuna kutoa time frame (nakupa siku saba to do something) wala kutahadharisha madhara yake (usipo do something itakuwa hivi na vile).

Kwa hiyo, hivi tunavyoongea ukitokea uchaguzi kesho asubuhi ni hii sheria ndio itatumika.

Nchi ambazo zina Judicial Review, mahakama ikisema sheria hii ni batili sheria hiyo inakufa papo hapo!

Ukibisha njoo na vifungu na vipengele vya sura na ibara
Ondoeni Fikra Kwamba Mahakama Kuu Imewaondolea Sifa Ya Wakurugenzi Kuwa Wasimamizi Wa Uchaguzi Bali Mahakama Chini Ya Ngwala J, Haijabatilisha Hivyo Vifungu Vinavyosemwa Bali HC imesema Kwamba vifungu vya sheria ya uchaguzi No. 7(1) na 7(3) ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) viko kinyume ya Katiba ya Nchi Basi, Ikaishia Hapo.
 
Kamuogeshe mwana wa kichina ndiyo kazi utakayo iweza pale ilala
Daudi Mchambuzi hebu kuwa na busara kidogo. Hivi unadhani wale wabunge wote wa upinzani waliopita kwa kura nyingi nani alikuwa msimamizi wa uchaguzi na ni nani alitangaza matokeo?? Hapo ndiyo ujue kuwa suala si kusema eti kura zinaibiwa. Ukweli utabaki pale pale kuwa CCM inakubalika sana tena sana hata akija nani kusimamia uchaguzi CCM lazima ishinde kwa kishindo, na kishindo hicho chaja tena 2020 na 2025, 2030, 2035, 2040, 2045, 2050, 2055, 2060, 2065, 2070, 2075, 2080, 2085, 2090, 2095, 2100 ...... ni CCM tu!
 
Nimefurahi sana. Hongereni majaji. Uzuri wa kesi za kikatiba wanakaa majaji watatu, hivyo vitisho vya watawala vinakuwa weak at least.

Aibu yenu mahakama ya rufaa na Jaji Mkuu wenu ambae anashinda kula mapochopocho ya ikulu kila dhifa/shughuli, tuje tushangae mmepindua hii hukumu
 
Ondoeni Fikra Kwamba Mahakama Kuu Imewaondolea Sifa Ya Wakurugenzi Kuwa Wasimamizi Wa Uchaguzi Bali Mahakama Chini Ya Ngwala J, Haijabatilisha Hivyo Vifungu Vinavyosemwa Bali HC imesema Kwamba vifungu vya sheria ya uchaguzi No. 7(1) na 7(3) ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) viko kinyume ya Katiba ya Nchi Basi, Ikaishia Hapo.
Mahakama haiwezi kuhukumu alafu ikaishia hapo lazima hivyo vifungu vibadilishwe
 
SSM hamtujui vyema sisi amri hii haitekelezeki kama ahadi ya kutiririsha maziwa nchi nzima
 
Serikali ndio Yenye Mamlaka Ya Kupeleka Jambo Lolote Bungeni, Mahakama Haina Mamlaka Ya ku- enforce Serikali Kupeleka Mswada Bungeni, Vifungu Vitaendelea Kutumika Kama Awali, Then Mahakama Haijabatilisha Bali Mahakama Imesema Ambao Ni Wanachama Wa Chama Fulani Hawapashwi Kuwa Wasimamizi Wa Uchaguzi
eti na wewe ni wakili/mwanasheria!
 
Back
Top Bottom