KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Je wewe unashauri je ?!. Kwamba huu utaratibu wenye elements za kikoloni ndiyo uendelee au ?!.
WaTz tumerogwa sehemu si bure !!
Hapana.
Nadhani hujamuelewa alichosema, unamlaumu bure na kumbe yeye kasema tu ukweli ulivyo. Mahakama haiwezi kubadilisha sheria kama mleta mada alivyosema. Baada ya uamzi huu wa mahakama inatakiwa bunge lipitishe mabadiliko ili sheria mpya itakayokuwa imepitishwa na bunge iweze kutumika. Na ukiangalia kwa makini, toka sasa hadi 2020 kwenye uchaguzi unaofuata, ukiacha hizi chaguzi za mitaa, mda wa bunge kufanya hivyo haupo, hasa ukichukulia kwamba hili ni jambo wasilolitaka wanaotawala.
Njia inayowezekana ni kwa vyama vya upinzani kukomalia kufanyika uchaguzi wowote bila marekebisho kufanyika na wafanye hivyo kwa kuwaelimisha wananchi, na kuomba msaada toka kwenye Jumuia za Kimataifa.
Hii ni kazi inayotakiwa waifanye kwa nguvu zote tokea sasa hivi na kuendelea mbele.