Mahakama Kuu yabatilisha Vifungu vya Sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
1093388

Mahakama Kuu (Dar) imebatilisha vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi.

Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2018, ilifunguliwa na Bob Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo, Bob Chacha Wangwe aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Fatuma Karume, anapinga Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Anadai kuwa hiyo ni kinyume cha Ibara ya 74 (14 ) ya Katiba ya Nchi ambayo inapiga marufuku kwa mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kwamba ana haki ya kupiga kura tu.

Aidha, alidai kuwa wakurugenzi hao ni wateule wa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

SHERIA INASOMEKAJE?

DE71CBBE-4AAF-442B-8789-CB3383387F7B.jpeg



Mwezi Juni 2018, akiwa Bungeni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, alisema Mbunge yeyote anayeona kuwa si sahihi Wakurugenzi wa Halmashauri kutosimamia uchaguzi, apeleke hoja Bungeni ili sheria hiyo ibadilishwe.

Mkuchika aliongeza kwa kusema “Tunayo Mahakama, pale ambapo mtu anaona hakutendewa haki aende Mahakamani,”

Ilikotoka:

Baadhi ya mijadala ndani ya JamiiForums:

2016

Julai 2018:

NEC wenyewe walishaona haya:

2016

2014
 
Habari nzuri sana hii.

Kila siku nawaambia wanasiasa wasiishi kwa mazoea. Wakurugenzi sasa wajipange upya kuchakachua kura.

Asante sana Chacha. Umeleta mabadiliko tunayoyataka. Tunaelekea kwenye tume huru sasa. Asante Mheshimiwa Fatuma Karume. Mumeacha alama kwenye taifa letu.
 
Safi sana!

Kiburi cha Jiwe sasa kitapungua.

Ni imani yangu mahakama itakuwa imetamka kuwa vifungu hivyo ni kinyume na katiba na kuagiza vifutwe/virekebishwe.

Ushauri:
Serikali/Bunge wasipotekeleza amri hii mpaka tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwakani,nashauri wapinzani waiombe Mahakama izuie uchaguzi mkuu unaokuja mpaka pale amri hii halali ya Mahakama Kuu itakapotekelezwa.
 
Mambo yanazidi kuongezeka huku muda ukipungua kwa kasi ya kutisha! Hawa jamaa walijidanganya sana na ile kauli ya "nikulipe mshahara na kukupa gari alafu umtangaze mpizani ....".

Sasa angalia, watu wanajipanga kupora majimbo bila ya kupigiwa kura kwa kutumia nguvu ya dola huku wakisahau huenda hiyo 2020 pesa ya uchaguzi tukasaidiwa na mabeberu na ndio wakashinikiza sheria zifuatwe.

Mungu ni mwema.
 
72 Reactions
Reply
Back
Top Bottom