Mahakama Kuu yabatilisha Vifungu vya Sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi

Ni gharama nyingine zinatengenezwa. Suluhisho lilipaswa kuwa watumishi wa umma wasiwe wanachama wa vyama vya siasa

Tatizo kubwa la sheria za nchi yetu kukosa meno ni madaraka makubwa aliyo nayo rais.

Kitendo cha rais kutoshtakiwa akiwa madarakani au akiwa ametoka hilo ni kosa kubwa.

Wakati huohuo rais ndio amelundikiwa madaraka ya kuteua wakuu wengi wa taasisi za umma tena kwa utashi wake na kuwa na nguvu ya kuwaondoa akitaka.

Kama kamisheni ya jeshi ilitumika kupokea wanachama wa ccm huku jeshi likiwa limetengwa na siasa itakuwa watumishi wa umma?
 
Asante Bob Chacha Wangwe kwa kufungua kesi, asante shangazi wa Taifa wakiri msomi Fatma Karume kwa kuisimamia hii kesi ipasavyo mpaka kuishinda jamuhuli.

Hili ni jiwe lililorushwa na mkono wa kushoto na kuhit target baraabara(Jiwe/malaika mkuu) .

Huu ni mwanzo mzuri kwa kuirudisha demokrasia nchini iliyokuwa imeanza kupotea kwa sheria shinikizi zipitishwazo na wagonga meza wa kila kitu ndioooo

Pia hongera mahakama kuu kwa kusimamia haki
 
Kesi nyingine ifunguliwe Mkurugenzi wa TISS akishateuliwa lazima ajadiliwe na ajieleze mbele ya kamati maalum ya wabunge yenye wabunge kutoka vyama vyote, kamati iwe na uwezo wa kumkataa.

Kesi nyingine idai mabadiliko kwenye uteuzi wa IGP asiwe mteule wa Rais, iwe ni kazi ya kuomba miongoni mwa polisi wenyewe na bunge ndio liwe na mamlaka ya kumtengua pale linapoona inafaa na pia kama itapendekezwa na Rais..
 
Back
Top Bottom