Mahakama Kuu yabatilisha Vifungu vya Sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi

Hii iko Kenya
 
Je wewe unashauri je ?!. Kwamba huu utaratibu wenye elements za kikoloni ndiyo uendelee au ?!.

WaTz tumerogwa sehemu si bure !!
 
Mumeacha alama kwenye taifa letu.
Mmeweka "alama kwenye taifa letu," Najua Fatma yupo, huyo Bob bado yupo au alishaondoka?

Hii ni hatua ndogo sana, hata kama ni hatua nzuri kuelekea kwenye chaguzi huru na za haki. Mda unakwenda mbio sana, marekebisho mhimu kwenye taratibu za uchaguzi yanatakiwa yafanyike haraka ili uchaguzi wa 2020 uwe halali.
Sina matumaini sana kuwa hilo litawezekana.
 
Safi sana wangwe na fatuma ...kwa hili mtaingia kwenye Vitabu vya kumbu kumbu

Ni wakati sasa wakufungua kesi mahakamani ya Kudai katiba Mpya
 
Hahaha kweli ni wehu
 
Nimefurahi kwa muda tu lakini nikakumbuka mlolongo wa cases zilizoamuliwa na mahakama na mahakama ikatangaza vifungu Fulani vya Sheria kupingana na katiba na kuitaka serikali kuvirekebisha lakini mpaka Leo vipo na vinaendelea kufanyiwa kazi.mfano ni kesi ya piter ngomango v republic na ile ya Idd mtegule ambazo zilibatirisha kifungu 148 Cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, kupingana na ibara ya 13 ya katiba.mpaka leo hakuna jipya.naomba mungu hili liwe tofauti.
 
Mungu ni mwema kwani hajawahi kuwaacha Waja wake bila ufumbuzi. Hongereni sana Wangwe na Shangazi Karume na wote walioshiriki ktk tafsiri ya vifungu sana
Amina
 
Ni gharama nyingine zinatengenezwa. Suluhisho lilipaswa kuwa watumishi wa umma wasiwe wanachama wa vyama vya siasa
Hii haifanyi kazi. Tumeona hata vyeo visovyostahili wanasiasa katika civil service wanateuliwa wanasiasa! Kiburi kilifikia impala makamisheni wa Tume ya Uchaguzi wanachaguliwa viongozi au yalikuwa viongozi wa vyama vya siasa!
 
Hii ni habari njema kwa wapenda mabadiliko. Ccm mbinu 1 imetolewa. Bado 17. Tutapambana na nyie mwanzo mwisho.
 
Sasa hivi hizo nafasi watapitishwa watu wa Tiss ndio watakwiba kura hadi tushangae..
 
W Watakata rufaa
 
Sio wa kuwaamini hata hao mahakama...wanaweza amka kesho na kusema uchaguzi usimamiwe na wakuu wa mikoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…