Mambo kama haya ndio yanachochea sana matukio kama ya Kibiti
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Seleman Mathew (Mesi) ashinda Kesi ya Rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara leo tarehe 28/06/2017.
Mathew alikata Rufaa baada ya Mahakama kumtia hatiani kwa kufanya Mkusanyiko (Mkutano) na hivyo kufungwa kwa miezi 8.
========
HUKUMU YA RUFAA YA SULEIMAN MATHEW NA MWENZAKE.
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Suleiman Mathew (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi) na mwenzake Ismail Kupilila (Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara).
Viongozi hawa walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017.
Baadae walikata rufaa Mahakama Kuu na kuomba dhamana kwa hati ya dharua ambayo walipewa tarehe 07.03.2017.
Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili.
Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia.
Aliongeza kusema kwamba ameona mambo kadha katika kesi hii (Observations)
1. Kwa mujibu wa sheria Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa vibali kwa vyama vya siasa kuhusu mikutano au maandamano kama ambavyo aliyekuwa OCD Ngiichi alidai katika ushahidi wake.
2. Warufani wameelekezwa kutoa taarifa Polisi kama sheria inavyotaka na si kwa Mtendaji wa Kijiji au kata kama walivyofanya wao.
3. Mazingira ya kesi na ushahidi uliotolewa, Polisi walitakiwa kitoa onyo la kawaida baada ya kuwatawanya watu. Lengo ni kujenga mahusiano mema kati ya raia na Polisi
4. Polisi wanatakiwa kutoa miongozo ili kazi zao ziweze kwenda sawa katika jamii.
Philbert Ngatunga
Katibu wa Kanda, Kusini
Unataka wajitoe ili watumbuliwe?!
!
Sasa kama hazina mashiko kwa nini wasiwe wanajitoa mapema.
Pia yanatuonyesha sisi watanzania ni wapuuzi,unakuwaje kiongozi wa nchi ya kidemokrasia unapiga marufuku kupingwaMambo kama haya ndio yanachochea sana matukio kama ya Kibiti
Magufuli anamuogopa Lowassa vibaya sana !
Hivi kama madaktari wangetibu Malaria kwa dawa zilezile pasipo kutumia hata ujuzi basi pia tungemalizika! Judge angeweza kutumia sheria iliyo kali zaidi ama kutoa adhabu kali zaidi iliyoainishwa kwenye kosa hilo!Hakuna Engineer aliyefundishwa kusanifu jumba lenye ghorofa 200 lakini watu wanajiongeza kulingana na changamoto na mahitaji halisiHayo ni maajabu ya Sheria Zetu.
Hakimu aliyesikiliza shauri tajwa amehukumu kwa Mujibu Wa Sheria ihusuyo "Money laundering" hajahukumu chochote Kwa utashi wake binafsi.
CCM inafanya siasa za kishamba sana !Mambo kama haya ndio yanachochea sana matukio kama ya Kibiti
Mifano yako haina mahusiano hata kidogo.Hivi kama madaktari wangetibu Malaria kwa dawa zilezile pasipo kutumia hata ujuzi basi pia tungemalizika! Judge angeweza kutumia sheria iliyo kali zaidi ama kutoa adhabu kali zaidi iliyoainishwa kwenye kosa hilo!Hakuna Engineer aliyefundishwa kusanifu jumba lenye ghorofa 200 lakini watu wanajiongeza kulingana na changamoto na mahitaji halisi
Nina hakika kuna "au vyote kwa pamoja", kwa nn asitumie hiyo??Mifano yako haina mahusiano hata kidogo.
Hukumu zote ni lazima Ref. Kwenye Sheria Fulani sasa hiyo iliyo "Kali zaidi" ndiyo hiyo inayomtaka anayetiwa hatiani kulipa kiasi hicho cha fedha au kwenda Jela Miaka 7.
Hapo kwenye "vyote kwa pamoja" kuna conditions kadha wa kadha za favour ya kisheria inayomnufaisha Mtuhumiwa/anayetiwa hatiani mathalani mfano hilo ni Kosa lake la kwanza, au ana familia inayomtegemea na mengine mengi mengi.Nina hakika kuna "au vyote kwa pamoja", kwa nn asitumie hiyo??
Lissu Ndio alisimamia kesi hii??Hawa wanasheria wa serikali itakuwa hawakusoma masomo aliyosoma The great Lissu.
Kama ni hivyo kwa nini unajisumbua sumbua kuleta habari zako humu kila sikuAfadhali wakati wa Mkoloni!!