Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Lindi

Mi natamani kama hizo observation alizoziona kwenye kesi hiyo zingewekwa wazi. Naamini ingetupa kitu zaidi cha kujifunza
 
Huyu anasema sitaki mikusanyiko wala maandamano, mwingine anatangaza mkusanyiko na maandamano ya kumpongeza Mafuligu. Ni kama wale wajenzi wa mnara wa Babeli waliogongana lugha hadi kushindwa kufanya chochote katika ujenzi wa mnara. maana huyu akiagiza tofali analetewa mwiko. Akiagiza udongo analetewa rangi.
 
c7b322cda5f8c5f5745bf12b80a8f315.jpg


Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Seleman Mathew (Mesi) ashinda Kesi ya Rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara leo tarehe 28/06/2017.

Mathew alikata Rufaa baada ya Mahakama kumtia hatiani kwa kufanya Mkusanyiko (Mkutano) na hivyo kufungwa kwa miezi 8.

========

HUKUMU YA RUFAA YA SULEIMAN MATHEW NA MWENZAKE.

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Suleiman Mathew (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi) na mwenzake Ismail Kupilila (Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara).

Viongozi hawa walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017.

Baadae walikata rufaa Mahakama Kuu na kuomba dhamana kwa hati ya dharua ambayo walipewa tarehe 07.03.2017.

Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili.

Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia.

Aliongeza kusema kwamba ameona mambo kadha katika kesi hii (Observations)

1. Kwa mujibu wa sheria Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa vibali kwa vyama vya siasa kuhusu mikutano au maandamano kama ambavyo aliyekuwa OCD Ngiichi alidai katika ushahidi wake.

2. Warufani wameelekezwa kutoa taarifa Polisi kama sheria inavyotaka na si kwa Mtendaji wa Kijiji au kata kama walivyofanya wao.

3. Mazingira ya kesi na ushahidi uliotolewa, Polisi walitakiwa kitoa onyo la kawaida baada ya kuwatawanya watu. Lengo ni kujenga mahusiano mema kati ya raia na Polisi

4. Polisi wanatakiwa kutoa miongozo ili kazi zao ziweze kwenda sawa katika jamii.

Philbert Ngatunga
Katibu wa Kanda, Kusini
Mambo kama haya ndio yanachochea sana matukio kama ya Kibiti
 
!
!
Sasa kama hazina mashiko kwa nini wasiwe wanajitoa mapema.
Unataka wajitoe ili watumbuliwe?

Kwani wewe hujui hizo kesi za akina Lijuakali, Suleiman Mathew, Godbless Lema, hazikuamuliwa kwa hao majaji na mahakimu kutumia taaluma zao, bali ilikuwa maelekezo toka juu?

Na wao hao Majaji/Mahakinu 'wakaafiki' maelekezo hayo, kwa kuwa taaluma zao walikuwa wameziweka 'rehani' Magogoni......

Hata hivyo Majaji hao na Mahakimu, wanapofanyaga maamuzi ya upendeleo wa wazi kwa Sisiem, huwa wanasahau kale kamsemo kanachosema, MWISHO WA UBAYA AIBU....
 
Siasa za kishamba za ccm zinadhalilisha Taifa , kesi za kizushi zinawadhalilisha vibaya mno
 
Hayo ni maajabu ya Sheria Zetu.



Hakimu aliyesikiliza shauri tajwa amehukumu kwa Mujibu Wa Sheria ihusuyo "Money laundering" hajahukumu chochote Kwa utashi wake binafsi.
Hivi kama madaktari wangetibu Malaria kwa dawa zilezile pasipo kutumia hata ujuzi basi pia tungemalizika! Judge angeweza kutumia sheria iliyo kali zaidi ama kutoa adhabu kali zaidi iliyoainishwa kwenye kosa hilo!Hakuna Engineer aliyefundishwa kusanifu jumba lenye ghorofa 200 lakini watu wanajiongeza kulingana na changamoto na mahitaji halisi
 
Hivi kama madaktari wangetibu Malaria kwa dawa zilezile pasipo kutumia hata ujuzi basi pia tungemalizika! Judge angeweza kutumia sheria iliyo kali zaidi ama kutoa adhabu kali zaidi iliyoainishwa kwenye kosa hilo!Hakuna Engineer aliyefundishwa kusanifu jumba lenye ghorofa 200 lakini watu wanajiongeza kulingana na changamoto na mahitaji halisi
Mifano yako haina mahusiano hata kidogo.

Hukumu zote ni lazima Ref. Kwenye Sheria Fulani sasa hiyo iliyo "Kali zaidi" ndiyo hiyo inayomtaka anayetiwa hatiani kulipa kiasi hicho cha fedha au kwenda Jela Miaka 7.
 
Namuomba wakili msomi Tundu Lissu afuate taratibu muafaka kuipata nakala ya hukumu hiyo kisha ampelekee IGP na wakuu wa vituo vya polisi.
Maana mahakama kuu imetoa mwongozo wa kisheria kwenye "Observations"

Ili atakayepingana na mahakama kwa mujibu wa Precedence basi kesi za hao vichwa ngumu ziwe rahisi.
 
Mifano yako haina mahusiano hata kidogo.

Hukumu zote ni lazima Ref. Kwenye Sheria Fulani sasa hiyo iliyo "Kali zaidi" ndiyo hiyo inayomtaka anayetiwa hatiani kulipa kiasi hicho cha fedha au kwenda Jela Miaka 7.
Nina hakika kuna "au vyote kwa pamoja", kwa nn asitumie hiyo??
 
Nina hakika kuna "au vyote kwa pamoja", kwa nn asitumie hiyo??
Hapo kwenye "vyote kwa pamoja" kuna conditions kadha wa kadha za favour ya kisheria inayomnufaisha Mtuhumiwa/anayetiwa hatiani mathalani mfano hilo ni Kosa lake la kwanza, au ana familia inayomtegemea na mengine mengi mengi.

Lakini kwa case husika mtuhumiwa alikubali kosa la kutakatisha fedha jambo ambalo linamuweka kwenye nafasi nzuri zaidi kunufaika na ahueni za adhabu kisheria kulingana na kosa husika.
 
Ccm huwa hawana uelewa wowote juu ya sheria wao ni kuagiza tu wale vijana wa nguo za KAKI
 
Back
Top Bottom