Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Lindi

Mhere Mwita

Verified Member
Jan 24, 2012
235
1,000
c7b322cda5f8c5f5745bf12b80a8f315.jpg
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Suleiman Mathew (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi) na mwenzake Ismail Kupilila (Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara).

Viongozi hawa walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017.

Baadae walikata rufaa Mahakama Kuu na kuomba dhamana kwa hati ya dharua ambayo walipewa tarehe 07.03.2017.

Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili.

Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia.

Aliongeza kusema kwamba ameona mambo kadha katika kesi hii (Observations)

1. Kwa mujibu wa sheria Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa vibali kwa vyama vya siasa kuhusu mikutano au maandamano kama ambavyo aliyekuwa OCD Ngiichi alidai katika ushahidi wake.

2. Warufani wameelekezwa kutoa taarifa Polisi kama sheria inavyotaka na si kwa Mtendaji wa Kijiji au kata kama walivyofanya wao.

3. Mazingira ya kesi na ushahidi uliotolewa, Polisi walitakiwa kitoa onyo la kawaida baada ya kuwatawanya watu. Lengo ni kujenga mahusiano mema kati ya raia na Polisi

4. Polisi wanatakiwa kutoa miongozo ili kazi zao ziweze kwenda sawa katika jamii.

Philbert Ngatunga
Katibu wa Kanda, Kusini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom