Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Lindi

HUKUMU YA RUFAA YA SULEIMAN MATHEW NA MWENZAKE.

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewaachia huru Suleiman Mathew (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi) na mwenzake Ismail Kupilila (Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyangamara).

Viongozi hawa walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifungo miezi nane jela bila faini na Mahakama ya Wilaya ya Lindi mnamo 18.01.2017.

Baadae walikata rufaa Mahakama Kuu na kuomba dhamana kwa hati ya dharua ambayo walipewa tarehe 07.03.2017.

Wakati anasoma hukumu hiyo Jaji Mlacha alisema kwamba kosa la kusanyiko lisilo halali linatakiwa kufanywa na watu watatu au zaidi sio wawili.

Akasema pia kwamba vifungo vyao vimefutwa. Wako huru kwa sababu hawana hatia.

Aliongeza kusema kwamba ameona mambo kadha katika kesi hii (Observations)

1. Kwa mujibu wa sheria Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa vibali kwa vyama vya siasa kuhusu mikutano au maandamano kama ambavyo aliyekuwa OCD Ngiichi alidai katika ushahidi wake.

2. Warufani wameelekezwa kutoa taarifa Polisi kama sheria inavyotaka na si kwa Mtendaji wa Kijiji au kata kama walivyofanya wao.

3. Mazingira ya kesi na ushahidi uliotolewa, Polisi walitakiwa kitoa onyo la kawaida baada ya kuwatawanya watu. Lengo ni kujenga mahusiano mema kati ya raia na Polisi

4. Polisi wanatakiwa kutoa miongozo ili kazi zao ziweze kwenda sawa katika jamii.

Philbert Ngatunga
Katibu wa Kanda, Kusini
 
c7b322cda5f8c5f5745bf12b80a8f315.jpg


Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Seleman Mathew (Mesi) ashinda Kesi ya Rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara leo tarehe 28/06/2017.
Mathew alikata Rufaa baada ya Mahakama kumtia hatiani kwa kufanya Mkusanyiko (Mkutano) na hivyo kufungwa kwa miezi 8.
Ndio huyo pichani?
 
CCM ni sawa na kale kamdudu mtu kanakosumbua katika mboga za majani. Kazi ya hako kamdudu ni kutoa hofu kwa watu. Hiki ndio chama ovu Afrika
 
Pole sana Mathew,mlioamua kufanya siasa upande wa upinzani mnapitia matatizo mengi sana lkn msirudi nyuma kama si leo ni kesho au kesho kutwa
 
Yawezekana tatizo likawa kwa mahakimu na majaji! Papaa ndama katakatisha 1.3 bill kahukumiwa faini ya mil 200!Maajabu ya mahakama zetu
Hayo ni maajabu ya Sheria Zetu.



Hakimu aliyesikiliza shauri tajwa amehukumu kwa Mujibu Wa Sheria ihusuyo "Money laundering" hajahukumu chochote Kwa utashi wake binafsi.
 
Back
Top Bottom