Mahakama Kuu haina mahabusu ya wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama Kuu haina mahabusu ya wanawake

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, May 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Mahakama Kuu haina mahabusu ya wanawake

  Imeandikwa na Veronica Mheta, Arusha; Tarehe: 29th April 2011 @ 23:47 Imesomwa na watu: 65; Jumla ya maoni: 0
  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa vyumba vya kutosha kumudu kuwahifadhi mahabusu wanawake, wanapokuwa wakisubiri mashauri yao kuitwa mahakamani na kuwakosesha haki ya kunyonyesha vizuri wale wenye watoto wachanga.

  Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere, ameyasema hayo mjini Arusha wakati anazungumza na waandishi wa habari.


  Amesema, tatizo hilo ni kubwa hali inayosababisha mahabusu hao wanawake kuwekwa nje chini ya ulinzi mkali huku baadhi yao wakiwa na watoto wanaostahili kunyonyeshwa au kupata huduma muhimu kwa wazazi wao.


  Jaji huyo amesema, hali hiyo ni hatari kwa kuwa mahabusu wanakosa haki yao ya msingi kama ya kuwanyonyesha watoto wao kwa uhuru na kulazimika kunyonyesha hadharani.


  Ametaja kero mbalimbali kuwa ni ukosefu wa kumbi za kufanyia mashauri, ambapo kwa sasa wana kumbi moja tu kubwa ya wazi na ukumbi mdogo hali ambayo inatatiza usikilizwaji wa mashauri katika kumbi hizo za wazi pindi zinapohitajika kufanya hivyo.


  “Upungufu huu unalazimisha wakati mwingi kupanga zamu za Mahakimu kuingia kazini kwa kupokezana nusu siku, wengine asubuhi na wengine mchana, jambo linalolazimisha kusikiliza kesi chache kwa siku na kusababisha kuzua malalamiko kwa jamii, kuwa tunaandaa mazingira ya rushwa” amesema Jaji Aisha.


  Amesema, matatizo yapo mengi katika Mahakama, lakini mengi yapo nje ya uwezo wao wa kuyatatua, hivyo vema, jamii ikaelewa jinsi ya kukabiliana nayo na kuvumilia.


  Ameiomba serikali na wadau wa Mahakama kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa mahakama ili kuweza kumaliza matatizo waliyonayo na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao bila vikwazo.


  Amemshukuru Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, kwa uamuzi wake wa kuahidi ujenzi wa Mahakama 20 za Mwanzo nchini kote na Arusha ikiwa mojawapo.


  “Hii itatupunguzia mlundikano wa Mahabusu na kesi zisizo na lazima katika Mahakama zetu chache zilizopo, na kuupunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya jamii kuhusu ucheleweshawaji wa kesi zao| alisisitiza Jaji Aisha.


  Aliongeza kuwa mfuko maalum wa Mahakama ulioahidiwa na Rais Kikwete katika kipindi chake, utakuwa suluhisho pekee sio tu kwamba utaifanya Mahakama kujitegemea na kujiendesha kama mhimili thabiti katika mihimili mitatu ya Dola, bali, pia utaipatia Mahakama fedha za kumudu kuendesha shughuli zake kiufanisi na kwa muda muafaka.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  HTML:
  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha,  inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa vyumba vya kutosha kumudu  kuwahifadhi mahabusu wanawake, wanapokuwa wakisubiri mashauri yao kuitwa  mahakamani na kuwakosesha haki ya kunyonyesha vizuri wale wenye watoto wachanga. 
   
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere,  ameyasema hayo mjini Arusha wakati anazungumza na waandishi wa habari.  
  
  SERIKALI HII KATIKA VIPAUMBELE VYAKE UTAOJI WA HAKI HAKIMO ILA KWENYE MAJUKWA TUU YA KUCHAPA DOMO...............
   
Loading...