Wanawake wapo njema kitambo tu, provided wanapata mazingira mazuri!!Wanawake kwasasa wapo juu sana ,imagine dada amepiga GPA 4.7 Bsc in Chemical processing.
Hata sisi class kwetu wakati tupo chuo, ingawaje wanaume ndio walikuwa wanakaa juu lakini by average wanawake walikuwa wanafanya vizuri kuliko wanaume!
Akina chige ilikuwa tukipata boom tu, hatuonekani chuo wala hostel, hadi upigiwe simu kwamba kesho kuna paper! Sasa unaanzaje kushindana na mtoto wa kike ambae ame-settle!!
Huu ujinga ujinga sitasahau mwaka wa pili ulisababisha karibu term mzima lunch yangu iwe chai na chapati lakini ndio mwaka ambao nilifaulu zaidi kwa sababu nilikuwa nabaki chuo!!