Magufuli yupo wapi

Status
Not open for further replies.
Kuna mambo ya kimkakati yalikuwa yanakamilishwa. Katikati ya wiki ijayo atakuwa Zanzibar kufunga kazi. Pia akina Ben Mkapa na Kikwete wanaanza ziara za kuzunguka nchi nzima kumnadi Tingatinga

Wakati mnaanda tingatinga lenu, wenzenu wanaandaa dereva/opereta wa tingatinga!
Dereva wa tingatinga lenu mnamjua?
 
Inaonekana mtoa mada hafuatilii matangazo ya biashara, sasa hivi Magufuri anawazidi hata cocacola, tigo na voda kwa matangazo ya biashara yake na kwenye mabango ndio usiseme mpaka kinyaa.

Wanampigia promo utafikiri hatujawahi kumuona au kumsikia.
 
Kama ingelikua Lowasa yupo kimya ungelisikia kelele za Magamba ooh yupo Germany Mara moja hahaaahaa
 
Kama ingelikua Lowasa yupo kimya ungelisikia kelele za Magamba ooh yupo Germany Mara moja hahaaahaa

Hatuna shaka na Magufuli hata akipotea wiki nzima ila UKAWA pamoja na ushabiki walio nao wanajijua kabisa wanafanya majaribio tu ya kuitoa CCM waone itakuaje na si kujikita kwenye kuwaza uhalisia wa maisha.
 
Atakuwa alikosea masharti kwahiyo madoctor watakuwa wamemuita embu fikiria mtu mwenye matatizo ya moyo uanze kupiga push up kishamba mara ululuke mara wakuzomee unafikiri humo ndani utabaki ni moyo tena?
Mtu kama anashindwa kuujali moyo wake kwa kuzingatia ushauri wa madoctor moyo ulio fanyiwa operesheni anaanza kululusha. Je ataweza kuwajali watanzania kwenye shida zao?
 
Kumbe wanamsikiliza sana Magufuli anavyomwaga sera zake. Wamemmiss sana

Tumemmisi mkuu, UKAWA tunataka Ushindi usiokuwa na visingizio. Mwangalieni mkapa asije kutukana tena muwe mnamwandalia vya kusema, Kikwete apite mikoa ya CCM na mwambie asikanyage Arusha, Mara, Mbeya, Iringi labda aende mikoa ya pwani na ngoma ya mdundiko atawapata wanawake wengi. Tunamtaka Magufuli maana anafurahisha sana Jukwaani kama Comedy
 
Vipi Magufuli alikuwepo mkutano wa CCM mwembe yanga Jana?
 
nasikia mnyika ataongea na waandishi wa habari,kuihoji tume alipo mgombea wa ccm,kwani ukawa wanahisi kuna mbinu inatengenezwa....
 
nimekuwa nikifuatilia taarifa za habari kupitia vituo mbalimbali tangu jana tarehe 10/10 nimeona zinarushwa za Edward Lowassa, Samia Suluhu, Maalim Seif, Babu Duni na Dr Shein. Wadau kwa anayejua Magufuli yupo wapi atujuze.........


Labda Push up zimemzidi kapata maumivu tehtehtehhh
 

Kitu usichokijua ni sawa na usiku wa giza, ccm bado itaendelea kushinda katika chaguzi zake zote, kwani upinzani na wana JF mnachofanya ni propoganda tu, hata chaguzi za serikali za vijiji/mitaa kelele hizi zilikuwepo pia, naamini siku ya ushindi wa upinzani hakutakuwa na vitisho wala kelele kama hizi zilizopo, ccm bado ni taasisi kubwa sana tofauti na uelewa wa watu wachache wanavoelewa, kushindwa kwa Lowasa kuibomoa ccm, ndo sasa imekuwa imara sana, na ushindi utakuwa wa kishindo.
 

Mbona povu jingi? ccm ni nani adi isitoke safari hii? mbona nchi nyingine zimefanikiwa kwanini isiwe tz? tunajua ccm mnategemea nguvu za giza ukiwemo mwenge ili mfanikiwe JE KUNA WA KUMSHINDA MUNGU? naona umetoa kisingizio cha serikali sijui za mitaa AMKA ZEZETA WEWE HUU NI MWAKA WA MABADILIKO NA HAKUNA WA KUZUIA, NAONA UNATEGEMEA NGUVU YA MABWANA ZAKO WAKULETEE USHINDI BADALA YA KUBISHA KWA HOJA. Lowassa kawashika pabaya mbweha nyie.
VIVA UKAWA!!!!!
 
Kwasiku 2. sasa sijaona ripoti ya kampeni ya ndugu Magufuli kwenye vyombo vya habari.amepotelea wapi?

Yupo Lumumba na jopo wanaandaa upya ilani ya uchaguzi ya CCM.
mambo yamewaendea kombo CCM wamepagawa.
 
Definition BURNOUT: Exhaustion of physical or emotional strength or motivation usually as a result of prolonged stress or FRUSTRATION .
 

Utamsikia leo akiwa zanzibar.
 
Tushajua Tumeshinda Magufuli Yupo Mezani Na Wataalamu Kujadili Na Kupanga Mipango Madhubuti Ya Kuendesha Serikali....!!
 
Tushajua Tumeshinda Magufuli Yupo Mezani Na Wataalamu Kujadili Na Kupanga Mipango Madhubuti Ya Kuendesha Serikali....!!

Heri Mungu akupe hekima na akunyime nguvu. Hilo nalo ni la kujisifia?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…