Magufuli: Wanaogoma wapaki Malori yao Nyumbani na wasiyaweke barabarani

Siku zote ieleweke kuwa busara zinahitajika na ni muhimu sana katika kuongoza na hata kutawala. Huyu Magufuli anaonyesha ni jinsi gani asivyokuwa na karama na busara za uongozi kwani watu kudai madai ni swala la kawaida ila kukaa nao na kuwasikiliza ni swala jingine na la muhimu sana kwani wanaodai na kugoma ni watu wazima na wana umuhimu katika uchumi wa nchi.

Hii inaonyesha jinsi Magufuri asivyokuwa na walau chembe ya uongozi kwani busara kwake si muhimu bali mabavu.
Watanzania kuwa macho na hizi pilika za urais mwaka 2015 kwani mwanzo wa kuwachunguza wagombea ni sasa.

Fuatene sheria acha ujanja ujanja wa kuandika humu huku ukujua na wewe ni mmiliki wa malori,,,,masuala ya kiutendaji unataka kuyaingizia siasa na kusema muda wa kuchunguza wagombea ndoo huu,,,acha ujanja ujanja ucyo na maana,,,,fuateni sheria kila kitu kiwe sawa,,
 
ujinga mtupu

tanzania hatuaendelei kwa sababu kila kitu tunajifanya kuangalia uungwana, blah blah .... walioendelea wote sheria ni msumeno!

tungekua na magufuli 10 tu hii nchi ingenyooka

sielewi tatizo la hawa watu wa malori ni nini .... wewe unapoomba kibali cha usafirishaji unajua kuna sheria za nchi na taratibu za kupata na kukitumia hicho kibali ... kama hutaki acha biashara

ningekua mimi kwanza hayo malori ningehakikisha hakuna lori bovu lolote linalosafiri .... pili kama yamegoma yasionekane yamepaki ovyo barabarani, barabara zetu zenyewe nyembamba watu wanazigeuza parking yard .....

Magufuli kamata hayo malori yote na taifisha (bahati mbaya sidhani kama hii sheria ipo)!

Kwa Kiasi kikubwa naunga mkono wazo la Magufuli na kauli zako hapo juu.

Napenda sana watu wanaosimamia sheria. Tanzania ina sheria nyingi na pamoja na mapungufu yake, zingetufikisha mahali pazuri kama tungekuwa na viongozi Imara wanaosimamia sheria hizo. Ambacho sijakitambua sawa sawa ni kuwa; Waziri alitoa tangazo kuwaarifu wahusika kwamba matumizi lasmi ya sheria hiyo yataanza lini? Kama hilo lilifanyika na wahusika/wamiliki hawakuchukua hatua hadi siku ya mwisho ya utekelezaji wa sheria husika basi Magufuli asirudi nyuma ila kama serikali haikufanya hivyo basi haikuwatendea haki.

Asante.
 
Waziri Magufuri amewataka wenye maloli na mabasi wote wanaogoma wayapaki magari yao nyumbani na wasiyaweke barabarani kwani wanasababoshia watumiaji wengine wa barabara foleni.

Amesema yeye anasimamia sheria na ataendelea kusimamia sheria.

SOURCE: RFA kipindi cha magazeti.

My Take:
Ni vizuri Serikali ikae na Wasafirishaji wafikie muafaka na si kila mtu kuvutia upande wake tu.

Dah huyu waziri kweli nae anaweza kuwa janga.

Yaani yeye anasimamia sheria tu hata kama ni mbovu
 
Siku zote ieleweke kuwa busara zinahitajika na ni muhimu sana katika kuongoza na hata kutawala. Huyu Magufuli anaonyesha ni jinsi gani asivyokuwa na karama na busara za uongozi kwani watu kudai madai ni swala la kawaida ila kukaa nao na kuwasikiliza ni swala jingine na la muhimu sana kwani wanaodai na kugoma ni watu wazima na wana umuhimu katika uchumi wa nchi.

Hii inaonyesha jinsi Magufuri asivyokuwa na walau chembe ya uongozi kwani busara kwake si muhimu bali mabavu.
Watanzania kuwa macho na hizi pilika za urais mwaka 2015 kwani mwanzo wa kuwachunguza wagombea ni sasa.

magufuli yuko sahihi kwa hili...tumeona waswahili kila wakiambiwa kutii sheria wanakuwa wabishi kisa wakigoma wabongo wa kwaida wanapata shida..................tufike wakati tuwajibike kile kilichosahihi kisimamiwe..mabasi ya mikoani yanazidisha abiria wakifika kwenye mizani wanashushwa..waswahili wanakubali usumbufu huo wakibanwa kwa manufaa ya umma....wanagoma..eti wananchi wareact
 
Waziri Magufuri amewataka wenye maloli na mabasi wote wanaogoma wayapaki magari yao nyumbani na wasiyaweke barabarani kwani wanasababoshia watumiaji wengine wa barabara foleni.

Amesema yeye anasimamia sheria na ataendelea kusimamia sheria.

SOURCE: RFA kipindi cha magazeti.

My Take:
Ni vizuri Serikali ikae na Wasafirishaji wafikie muafaka na si kila mtu kuvutia upande wake tu.

Dr.Magufuli ni kiboko na jana katika kikao na waandishi wa habari aliyataja makampuni 13 ambayo yana rekodi ya miaka kumi (10) ya kutozidisha mizigo na hayajawahi kukamatwa katika mizani yeyote Tanzania na Afrika ya Mashariki:

1. Dar Express (Passenger Coaches)

2. Cargo Star (Haulage Lorries)

3. Hood Bus Service (Passenger Coaches)

4. Coca Cola (Haulage Lorries)

5. BM Bus Service (Passenger Coaches)

6. Bakhresa Group (Haulage Lorries)

7. TBL (Haulage Lorries)

8. Golden Bus Services (Passenger Coaches)

9.[FONT=verdana,geneva][/FONT]Kanji Lalji Limited ,KL Ltd. (Haulage Lorries)

10. Tawaqal (Passenger Coaches & Haulage Lorries)

11. Consolidated Logistics (Haulage Lorries)

12. Lamada Transport (Haulage Lorries)

13. British Petroleum/PUMA (Haulage Lorries)

TATOA wasome sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya usalama barabarani iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2001 inayohusu kiwango cha mwisho cha uzito wa magari.

Dr.Magufuli kiboko cha wavunja sheria! Watanzani tumuungeni mkono.
 
tatizo letu sisi watz tumezoea kubembelezana na pia hatuwezi kutii sheria bila shuruti hawa wamiliki wa malori na mabasi ndo hao hao ambao wamesababisha kufa kwa reli kwa sababu zao binafsi na pia wanafanya biashara ya usafirishaji kwa manufaa yao binafsi kwa mfano lori la tani 7 linatengenezwa ili libebe tani 17 mpaka 20 hiyo ni sawa na pia wanatumia mapungufu ya watumishi wa waserekali ktk mizani kufanya ushenzi wao kwani wakipima mfano mizani ya kibaha na lori kukutwa limezidi wanatoa kitu kidogo ili wavuke then wakienda mizani inayofuata lazima mizani utakuwa juu na pia hawa wamiliki hawajui kitu gani watumishi wao wanafanya huko njiani mbona zipo kampuni hata cku moja hawajazidisha uzito mfano azam na dar express kwa maoni yangu ni kwamba watanzania kama tunataka maendeleo ya kweli tusimamie sheria na tuwape nguvu viongozi kama mwakyembe,magufuli,kagasheki kwa mustakabali wa nchi yetu tuache ubabaishaji na kama mtu hataki hajalazimishwa buni biashara nyingine kwani zipo nyingi tu sio usafirishaji peke yake.
 
Nampongeza Magufuli kwa kauli hii, watza tunapenda super profit na hatuendeshi biashara kitaaluma; walipaswa kutafuta njia mpadala ya kupunguza operation cost, kusafirisha mzigo kuna midle mans zaidi ya watatu, kukata tiketi ya basi ndio usiseme yaani basi la kwenda morogoro kwa nauli ya sh 5000 kuna midlle mans zaidi ya watatu. Tunapaswa kutumia akili katika kuendesha biashara, kuna graduates wengi wa mambo ya biashara lakini hawa wafanyabiashara wetu wanashindwa kuwatumia na badala yake wanazidi kuwaumiza walaji.
 
Hapa tunaleta ushabiki usio na maana lakini ukweli ni kwamba MAGUFURI yuko sawa mno.Hii nchi inahitaji viongozi wababe kama MAGUFURI.Bila ubabe wa magufuri,barabara zetu zitakuwa nyang'anyang'a muda si mrefu.Tutakao umia zaidi baada ya barabara kuharibika ni sisi wananzengo sanasana na siyo hao wamiliki wa maroli sababu wao wanaweza kukwepa KODI lakini sisi wavuja jasho ni vigumu mno kuukwepa mkondo wa KODI.
 
mi nadhani tatizo siyo Magufuli kama wengi mnavyodhani, Magufuli anatekeleza sheria, na sheria ni msumeno,

inawezekana sheria ina mapungufu yake, kwa mantiki hiyo Magufuli anatekeleza sheria yenye mapungufu,

lakini Magufuli hatungi wala kusaini miswada ya sheria mbovu! je ni nani? anahusika na sheria mbovu?? jibu ni "Bunge la kichovu lenye wabunge wengi Maccm"

wewe unaye lalamika je ulichagua mbunge wa chama gani ili atetee maslahi yako ya kuzidisha mizigo barabarani, alafu mbona huilalamikii serikali chovu ya Maccm unamlalamikia waziri mmoja tu. unajua kitu inaitwa "collective responsibility" usideal na mtu deal na mfumo

tafakari chukua hatua

Waziri Magufuri amewataka wenye maloli na mabasi wote wanaogoma wayapaki magari yao nyumbani na wasiyaweke barabarani kwani wanasababoshia watumiaji wengine wa barabara foleni.

Amesema yeye anasimamia sheria na ataendelea kusimamia sheria.

SOURCE: RFA kipindi cha magazeti.

My Take:
Ni vizuri Serikali ikae na Wasafirishaji wafikie muafaka na si kila mtu kuvutia upande wake tu.
 
Serikali ingejikita kwenye kuimarisha reli ugomvi huu wa malari wala usingekuwepo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Ndugu yangu wanaogopa kuboresha reli kwakuwa maroli na mabasi yenyewe ni mafisadi ambao 100% wapo ndani ya serikali kazi tunayo kweli.
 
Mawazo mazuri sana,sasa nenda pale wizara ya uchukuzi mchukue Magufuli nenda naye ubungo ukawasiadie wale abiria walokwama usafiri,
hilo la ubungo ni "administrative issue" maana hata wkt wa xmas abiria huwa wanakwama. wala magufuli hatakiwi kwenda, wanaweza malizana na sumatra/ vyombo vya dola tu. ila la kutuharibia barabara zetu ni policy issue, pesa za kodi zetu zinaishia kukarabati barabara, hapo hatu-wasupport wa mabasi wala malori.
 
mi nadhani tatizo siyo Magufuli kama wengi mnavyodhani, Magufuli anatekeleza sheria, na sheria ni msumeno,

inawezekana sheria ina mapungufu yake, kwa mantiki hiyo Magufuli anatekeleza sheria yenye mapungufu
,

lakini Magufuli hatungi wala kusaini miswada ya sheria mbovu! je ni nani? anahusika na sheria mbovu?? jibu ni "Bunge la kichovu lenye wabunge wengi Maccm"

wewe unaye lalamika je ulichagua mbunge wa chama gani ili atetee maslahi yako ya kuzidisha mizigo barabarani, alafu mbona huilalamikii serikali chovu ya Maccm unamlalamikia waziri mmoja tu. unajua kitu inaitwa "collective responsibility" usideal na mtu deal na mfumo

tafakari chukua hatua
mfano mzuri ni sasa hivi wanavyoshabikia presidaa asaini sheria ya katiba mpya kisa yeye ni raisi na ana madaraka, wanasahau upresidaa unahitaji hekima za hali ya juu... 3 yrs frm nw watakuja mlalamikia waziri mwenye mamlaka atakapoanza ku-implement hiyo sheria.
tatizo letu wa-tz hatutaki kuelewa mambo kabla ya kuamua kuonyesha feelings zetu, wengi wanafata mkumbo na ushabiki. magufuli alishasema sheria aibadilishwi na barua bali ni kurudi mjengoni na kurekebisha sheria. go magufuli go...
 
Very pertinent observation in deed. The fact is if you have a good railway system with a network covering all key cities and towns then you don't need all these inter-city monster trucks weighing over 50 tons which do more harm to our roads and environment than the benefits they produce. You will need only medium range trucks (the size of Fuso) to move freight from the main railway stations to their points of destinations within the regions. For instance, with a good and functioning railway system in Tanzania you may not need a truck to transport your cargo from Dar to Mwanza, Mbeya, Songea, Arusha, Moshi, Tanga, Kigoma etc. This will save not only our roads from wear and tear but will also preserve the environment from polution.
a reason i support constructions of railways and not a port. the port will come later, the priority should be the good railway network
 
Mkuu naona amechelewa kutoa amri hiyo, waya-park majumbani/magereji yao - Taifa aliwezi kutekwa nyara na ma-cartel wa usafirishaji wachache, kwanza wanapashwa kuburuzwa mahakamani kwa kujaribu kuhujumu uchumi. Taifa kwa nini alijiulizi hivi kwa nini watu hawa wachache wamekomalia lupitia excess ya tani tano, hii excess ina nini ndani yake zaidi ya kutuharibia barabara zilizo jengwa kwa gharama kubwa, hisije ikawa excess ikiwa Mega Excess; nilikuwa nawafatilia fatilia sana hawapendi kabisa mizani iliyo wekwa kwenye vitua maalumu wanataka ikiwezekan vibaki viwili tu ili njiani wafanye madudu yao - wakikaribia mizani wafanye usanii wao. Swali ni je Uzalendo huko wapi - si vizuri kila wakati kufikiria faida tu bila ya kutimiza wajibu.
 
Serikali ingejikita kwenye kuimarisha reli ugomvi huu wa malari wala usingekuwepo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Reli wametupia mbali. Hivi kweli kuna sababu ya serikali kuachia sekta ya reli kwa mwekezaji? Hona sasa hakuna cha safari za uakika za treni kutoka bara. Haya sasa huyu waziri hanatumia ubabe wakati watanzania wanakosa usafiri. Tunashindwa kufikilia muda tunaopoteza wakati nchi zingine zikisonga mbele na kazi. Tanzania tubadilike hawa viongozi wanakatisha tamaa na kauli zao kila kukicha.

Tunaitaji uwajibikaji sio kiongozi anakuja na kusema kwamba sheria hipo, je mwaka 2006 kwanini walifikia makubaliano na wasafirishaji? Je kutengua makubaliano hayo walishirikishwa au?
 
Waziri Magufuri amewataka wenye maloli na mabasi wote wanaogoma wayapaki magari yao nyumbani na wasiyaweke barabarani kwani wanasababoshia watumiaji wengine wa barabara foleni.

Amesema yeye anasimamia sheria na ataendelea kusimamia sheria.

SOURCE: RFA kipindi cha magazeti.

My Take:
Ni vizuri Serikali ikae na Wasafirishaji wafikie muafaka na si kila mtu kuvutia upande wake tu.

sawa waongee, lakini kama wamegoma... wanfanya barabarani??? wakayaweke magari yao gereji sie kupunguziwe majasho ya foleni

dawa ya hawa trasnporter ni kuweka mfumo mzuri wa reli tu......... kwisha habari yao
 
Sheria ni msumeno na lazima kuwepo na utawala wa sheria.

Mbona kuna makampuni ya usafirishaji mengine hayajawahi kuzidisha mizigo kwa zaidi ya miaka tisa kama tatizo ni mizani?.

Hawa wamiliki wa magari ya usafirishaji wanatingisha kiberiti nila kujua kama Kiberiti cha Mh. Magufuli kimejaa.
 
Serikali ya MACCM haina uwezo wa kufanya maamuzi yoyote yenye maslahi kwa Tanzania na Watanzania, na rekodi yao ya utendaji haisemi uongo.

Serikali ingejikita kwenye kuimarisha reli ugomvi huu wa malari wala usingekuwepo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom