Magufuli turns Mnangagwa into a translator

Magufuli turns Mnangagwa into a translator

Ukute hapo unalala njaa pamoja na kuwa unakijua kingereza
giphy.gif
 
anayeongea kiswahili ni RAISI WA NCHI unayejua KIZUNGU ni JF KEYBOARD WARIOR

MAISHA YETU tunapenda kujisifia vitu ambavyo haviongezi idadi ya sifuri yoyote ile kwenye bank accounts zetu
 
Kaka Kiingereza cha Mbowe ni level nyingine

Unajua mtoto wa tajiri hata akiwa mchafu watu humuita msafi na kumpigia magoti

Kaka mtoto wa tajiri huongea Kiingereza tofauti na maskini

Endelea kujilinganisha familia ya Mbowe na Babu yako mvaa kandambili zilizotoboka katikati

Mbowe ni next level kwenye lugha ya malkia

Tangu lini maskini akaongea lugha ya kueleweka mbele ya tajiri, Tajiri hata akikosea watu huzalisha msamiati aliotamka tajiri na kuingiza kwenye kamusi
Ha ha
 
Kujua kiingereza sio ndio kuwa na akili au uwezo mkubwa wa kiuongozi, nafahamu rais wa China hajui kabisa kiingereza, Chancellor wa ujerumani hajui kiingereza , hao ni viongozi wa nchi kubwa duniani na wanaheshimika Sana .
Jamani tuache kumbeza kiongozi wetu kwa suala la lugha ya kiingereza,
Merkel alizungumza na Rais kwa simu kwa lugha ipi mpaka akaahidi kutujengea kiwanda cha mbolea nambari wani Afrika kwa ukubwa? Walielewana vizuri sana.
 
Mswahili hasa utamjua tu mjuaji lakini hajui mjanja mjanja mwisho hujiumbua mwenyewe.
 
Wewe, Babako na Ukoo wenu wote wa panya hata kwa miaka 5000 hamtafikia mafanikio Raisi Magufuli alioyafikia katika maisha yake kwa muda mfupi aloishi hapa Duniani.

Hivyo funga kopo lako, wache Wanaume waliobarikiwa wafanye yale walioteuliwa kuyafanya.
Mafanikio yanaweza kuwa NEGATIVE pia...Magufuli hajafanikiwa chochote...sanasana kaharibu tu kila kitu
 
Tunafanana kwamba sio lazima kwa kiongozi mkuu wa nchi kujua sana kiingereza ndio uthibitisho kwamba huyo ni kiongozi mzuri.
Sasa watu wanaombeza kiongozi wetu kwamba eti hafahamu kiingereza vizuri siwaelewi mantiki yao,
Sio lazima mtu kufahamu lugha ya kiingereza vizuri ndio uthibitisho kwamba ni kiongozi mzuri
Kiongozi mzuri anapokwenda nchi ya kigeni anakuwa amejiandaa at akavyo wasiliana na wenyeji wake. Kweli huko Ikulu hakuna mkalimani hata mmoja? Nchi zote alizotembelea zinazungumza kingereza kwa mini hakujiandaa. Bad image for country.
 
Mafanikio yanaweza kuwa NEGATIVE pia...Magufuli hajafanikiwa chochote...sanasana kaharibu tu kila kitu

Magufuli ni Raisi wa JMTZ, wewe na Familia yako mmefanikiwa nini? Au kuna mahali popote pale Dunia hii ukoo wako unajulikana kwa chochote kile?
Magufuli amefanikisha mengi na hata akiondoka kesho Jina lake litabakia Dunia nzima kwamba alikuwa Raisi wa V wa JMTZ, wewe na familia yako yote mna nini cha kuonyesha na wapi?

Hivyo hata mumcheke hadi mpasuke lkn ukweli ni kwamba ameishi maisha yake vizuri na kutumia muda hapa Duniani ipasavyo na wengi wenu na ukoo wenu hata miaka 10 000 ijayo hamuwezi kufanikisha Magufuli aliyofanikisha kwa miaka 50 tu hapa Duniani.

Hivyo kumcheka mtu kama huyo ambaye amekuzidi kila kitu, mnaonekana ni kituko!
 
Ohh that is my president, yaani nafurahi sana anaposimamia msimamo wa lugha yetu. Mungu ambariki sana Dr Magufuli!!
Ni kweli.Lugha ni kwa ajili ya mawasiliano tu.kama mawasiliano yalikuwepo kati ya hao viongozi,na mambo ya maana na msingi yakakubalika kati yao,hilo ndilo twalihitaji.Sio kutuuzia kingereza,lugha ya watu.
Hizi silka za kuona kingereza ni kitu cha maana sana,nadhani ni kilema na kasumba fulani hivi ya hovyo tu.Hata Nyerere tu,ambaye kwenye lugha kila mtu amjua alikuwa mahiri,alishawahi kukebehi waabuduo kingereza na kuwasema kuwa "...kuna watu kwa namna wanavyokitukuza kingereza,hata wakitukanwa,ilimradi ni kwa kingereza,watafurahi na kucheka tu...".
Hakuna sababu kukomalia lugha kama haikai sawa mdomoni.Tumekuwa na mabingwa wa kuongea hiyo lugha ya kingereza,wababe wa jukwaa katika lugha,lakini sioni kama ilitusaidia sana kama nchi katika ulinganisho wa tija kiuongozi.Sana sana tulipigwa tu kama nchi.
Lakini zaidi,kukuza Kiswahili na kukitangaza huko,nako kuna faida zaidi na kapata maombi ya waalimu wa hii lugha.Sasa sijui hao mahiri wetu wa kingereza waliopita,walituletea faida kama hii?
Binafsi,kosa pekee ninalohisi lilifanyika,ni kutoandaa mtu wa kutafsiri toka hapa hapa Tz wakaambatana naye,na wamejaa tu.
Wachina wakija wanakuja na wakalimani.Sisi ifike mahala,hata kiongozi akiwa aijua lugha,ili kuongeza msisitizo na kujiainisha kiufasaha zaidi,wakati huo huo hata wananchi wake karibia wote wajue kiongozi wao alisema nini,vema mwendo uwe huu huu....KISWAHILI!
Uongozi si lazima mpaka mtu kujua kingereza sana.
 
Haina shida maana sijawahi kumsikia Putin ama rais wa china akiongea lugha ya kigeni
Putin na Rais wa China wamesoma kwa lugha gani? Atleast wanazimudu lugha walizojifunzia na kusomea masomo yao kuanzia elimu ya awali hadi ya chuo kikuu lakini kwa huyu bwana ni jambo tofauti kabisa lugha kaisomea lakini haiwezi kabisa
 
Magufuli ni Raisi wa JMTZ, wewe na Familia yako mmefanikiwa nini? Au kuna mahali popote pale Dunia hii ukoo wako unajulikana kwa chochote kile?
Magufuli amefanikisha mengi na hata akiondoka kesho Jina lake litabakia Dunia nzima kwamba alikuwa Raisi wa V wa JMTZ, wewe na familia yako yote mna nini cha kuonyesha na wapi?

Hivyo hata mumcheke hadi mpasuke lkn ukweli ni kwamba kwa ameishi maisha yake vizuri na kutumia muda hapa Duniani vizuri na wengi wenu na ukoo wenu hataa miaka 10 000 ijayo hamuwezi kufanikisha!
Nadhani wewe utakua umeacha legacy ya Lumumba 7,000 mkuu au sio hahahahaah 😁😁😁
 
Wabongo wengi hata wanaojiita wasomi yai limewapita pembeni, huwezi kuwa mahiri wa kuongea lugha kama huitumii katika mawasiliano yako ya kila siku. Hapa bongo asilimia kubwa ya mawasiliano ni kwa lugha ya kiswahili, hivyo ni jambo la kustaabisha kufikiri kwamba watanzania wanaweza kuongea kiingereza fluently. Kama wapo ni wachache sana hawafiki hata asilimia moja, ukweli lazima usemwe
 
Magufuli ni Raisi wa JMTZ, wewe na Familia yako mmefanikiwa nini? Au kuna mahali popote pale Dunia hii ukoo wako unajulikana kwa chochote kile?
Magufuli amefanikisha mengi na hata akiondoka kesho Jina lake litabakia Dunia nzima kwamba alikuwa Raisi wa V wa JMTZ, wewe na familia yako yote mna nini cha kuonyesha na wapi?

Hivyo hata mumcheke hadi mpasuke lkn ukweli ni kwamba kwa ameishi maisha yake vizuri na kutumia muda hapa Duniani vizuri na wengi wenu na ukoo wenu hataa miaka 10 000 ijayo hamuwezi kufanikisha!
Hata idd Amin, Osama bin Laden, Bokassa wote hao majina yao yamebakia...same to huyo MAGUFULI wako aliyeharibu kila kitu

Rais wa ajabu kabisa kuwahi kutokea. Ni AIBU kwa kila mtanzania
 
Magufuli ni Raisi wa JMTZ, wewe na Familia yako mmefanikiwa nini? Au kuna mahali popote pale Dunia hii ukoo wako unajulikana kwa chochote kile?
Magufuli amefanikisha mengi na hata akiondoka kesho Jina lake litabakia Dunia nzima kwamba alikuwa Raisi wa V wa JMTZ, wewe na familia yako yote mna nini cha kuonyesha na wapi?

Hivyo hata mumcheke hadi mpasuke lkn ukweli ni kwamba kwa ameishi maisha yake vizuri na kutumia muda hapa Duniani ipasavyo na wengi wenu na ukoo wenu hata miaka 10 000 ijayo hamuwezi kufanikisha Magufuli aliyofanikisha kwa miaka 50 tu!
Kila mtu na mkate wake,kama kila mtu akitaka kuwa Rais,mambo mengine atafanya nani?
Mtu yeyote mwenye sifa anaweza kuwa Rais,ni game tu!Hata IDD Amin alikuwa Rais!!!!Kuwa Rais sio kwamba umebarikiwa sana kuliko binadamu wengine!
 
Back
Top Bottom