Mara kadhaa katika jukwa hili na majukwaa mengine, nilisema kwamba Kenya inahitaji Rais Kama Magufuli. Nakumbuka hata kuna wakati tulipingana sana na MK254 kuhusu systems vs personalities. MK254 alimsifu Magufuli kwa nia yake, lakini alikuwa very cautious kuhusu mtindo wake wa kufanya mambo. Mimi naye, nilikuwa upande ule mwingine wa kutaka ule mtindo wa Magufuli. Siku ya leo, nakubali kuwa nilikuwa nimekosea. Ingawa taifa linahitaji kiongozi mwenye mamlaka kama vile Kagame, kiongozi huyu yafaa awe na nia ya kuweka taasisi zitakazodumu kuliko madaraka yake mwenyewe.
Magufuli ni kiongozi ambaye anatakia taifa lake mema. Tatizo lake ni kukurupuka na kuwafanya wote ambao wako upande wake kuwa adui ikiwa hawatakubaliana naye kwa vitu vyote. Juzi amekurupuka kwa hili la kuibiwa mali ya taifa, na vile ninavyoona, kuna vile kamati imemdanganya hata kwa mambo ya kiupuzi. Kwa mfano; kamati yamuambia kuwa Kampuni ya Acacia, haijasajiliwa Kule Tanzania; itakuwaje basi kampuni hii iwe inalipa Ushuru, PAYE na mengine yote? Huu sio upuuzi tu? Wakati anapokea ripoti hii, Rais alisema kuwa anakubaliana na mapendekezo yote 100%. Hii ni ripoti amabyo hata hajasoma na ndio anapokea tu. Hata hujawauliza civil servants walio ndani for second opinion?
Upuuzi huu huu ndio alioufanya kule kwenye bandari. Sasa hivi, vitu vinavyopita kwa bandari ya Dar vimepunguwa kwa asilimia 13%. Vitu vinavyopitia bandari ya Mombasa na kuingia Tanzania vimeongezeka kutoka 1% hadi 2.7%. Ni kitu gani kinafanyika huku? Kwa kweli uongozi unahitaji busara. Ndiposa wazungu walinena: "The road to hell is paved with good intentions."
Ukitazama video hii ya mbunge wa CCM, utaona kuanzia dakika 7, akiongelea ya bandari