Safari za nje kwani zilitengewa kiasi gani na bunge? Si kwamba nyingine zilikuwa zina-infringe bajeti ya maeneo mengine?Safari za nje.
Si ameshafuta Safari zote za nje! Makongamano! Think this despot J kikwete used 50 million USD by only himself plying the world; doing his business! The money is enough to educate our boys and girls!!
By the way Mr. JPM remove this ambassador at the Beijing Embassy!
Your a great thinker ?Tusiongee kinadharia hapa, aseme gharama ya shule zote za serikali ni kiasi gani na kiasi anachotarajia kupata ni kiasi gani kutokana na kubana matumizi. Kufanya kazi kwa headlines hakutatusaidia.
Wakati wa Lowassa kujibu maswali haya umekwisha. Hatutekelezi sera zake. Tunatekeleza ilani ya CCM.Kwani Lowasa pia si alisema hayo.. Yeye angezitoa wapi hizo hela??
Elimu ni kitu cha muhimu sana ndio maana leo hii w?tanzania wengi wanashabikia vyama vya siasa kama wanavyo shabikia mpira, Na hatuwezi kupata maendeleo kama hatuna elimu nzuri.
Afya pia ni muhimu sana kwani umaskini unasababishwa na magonja na kukosekana huduma nzuri mahospitalini. Ukiwa mgonjwa leo hii utamaliza akiba yote uliojiwekea na kurudi kwenye umaskini.
Hela zipo nyigi saaaana lakini asilikia kubwa zinaishia kwa mafisadi kwa hiyo kazi ya kwanza inabidi abane na kutokomeza ufisadi. Sasa ndio amenza kazi tuone.
Pesa yenyewe usifikiri ni nyingi iliyokuwa inapatikana kama ada. Kumbuka kila mwanafunzi alikuwa analipa elfu 20 tu. Piga hesabu kama wanafunzi wako milioni moja kwa mwaka watalipa ngapi.
Mjomba yenu Mamvi Lowasa alipokuwa anawaingiza chaka kwamba elimu mpaka chuo kikuu bure mbona hamkuwahi kumuuliza hizo pesa atazitoa wapi?
Mwacheni Hon President afanye yake.
Home shopping center
Kuna umuhimu gani kuwa na vikao vya bajeti vya kupanga pesa za maendeleo na pesa za matumizi ya serikali?
Pesa za kulipia elimu ya bure amempa nani au ni mamlaka ipi imeidhinisha pesa hizo zitumike ?
Naomba ieleweke sina tatizo kwa watoto kusoma bure. Hii ni November na January elimu ni bure. Hayo makusanyo yote uliyotaja mengine yanahitaji mipango na hata kubadilishwa kwa sheria. Mf suala la misamaha ya kodi. Tatizo amekurupuka kudhani ukiahidi leo lazima kesho uanze kutekeleza bila kujua pesa anatoa wapi. Unazungumzia madini, kuna kampuni zinatangaza kupunguza wafanyakazi kutokana na kupungua kwa bei ya dhahabu, kubuni vyanzo vipya; si suala la miezi miwili. Angekuja na hesabu hapa kwa hiyo mipango yake mipya atakusanya kiasi gani na mahitaji ya shule ni kiasi gani. Tumechoka kusikiliza porojo zisizokuwa na evidence. Hizi shule, mambo yatakuwa magumu zaidi. Hao walimu watapata hizo fedha kufidia umbwe litakalojitokeza?
Tuwe wakweli nchi ni ya kwetu na ccm ni ya kwangu na magufuli ni rahisi wetu mamvi alisema pesa itatokana na kuondoa safari za nje na kuondoa mashangingi/gari ambazo serikali inagharamia pesa ndefu.Leo tumeona raisi wetu anapita mulemule banyani mbaya lkn tukubali sisi tulikukuwa wa maisha club kidumu chama chetu.Mjomba yenu Mamvi Lowasa alipokuwa anawaingiza chaka kwamba elimu mpaka chuo kikuu bure mbona hamkuwahi kumuuliza hizo pesa atazitoa wapi?
Mwacheni Hon President afanye yake.
Wakati wa Lowassa kujibu maswali haya umekwisha. Hatutekelezi sera zake. Tunatekeleza ilani ya CCM.
Elimu bora ni muhimu, lakini kufuta michango bila maelezo ya kina kwamba zile pesa walizokuwa wanachangia wanafunzi za Maabara nani atapeleka. Madawati na afya, je Magufuli kajipanga? Anatoa wapi? Huwezi kuleta hadithi ya kuwa watu wakakusanye pesa, wanaenda kukusanya wapi? Ni asilimia ngapi ya safari zitafutwa. Safari km za ofisi ya CAG kukagua balozi huwezi kufuta. Safari za UN na AU za kiusalama huwezi kufuta. Amefuta safari zipi? Hizi porojo za kwenye vyombo
vya habari si mahitaji ya Watanzania