Bahati mbaya sana unasahau hoja na kumtetea mtu. Sina tatizo na Magufuli, nina tatizo na utekelezaji ambao unaashiria kutofuata taratibu na kanuni za nchi. Ukipitia posts zangu hapo nyuma utaona nimeorodhesha vipaumbele vya nchi yetu. Kipaumbele kwenye bajeti ya sasa hivi si elimu bure kutoka nursery mpaka sekondari au chuo kikuu. Haya mambo yanahitaji mipango. Ahadi hii ni endelevu ambayo anatakiwa aitekeleze miaka yote atakapokuwa madarakani. Si barabara kama ukijenga na kumaliza gharama zimekwisha. Inahitaji wadau wa elimu waweze kutambua mahitaji halisi ni kiasi gani. Tukumbuke shule zinatofautiana Kijiografia na kimahitaji pia. Wengine wanapata maji ya bomba na wengine hawapati. Maji yatawafikia vipi kama watapewa bajeti yenye kufanana. Lini amefanya uchambuzi? Amefuta ada peke yake au na michango? Ninafaham kipato cha nchi na bajeti ya elimu naifaham fika. Kufanya maamuzi kwa kukurupuka kutatugharimu. Hata kama tulimchagua tusiogope kuongea yale yenye kuitakia nchi yetu mema.Nanona umeongelea negative Points, sasa unadhani angefanyeje ili elimu iwe bora? Je unfahmu badget ya elimu kwa mwezi hapa TZ? na je unafahamu incomes ya Tanzania kwa siku, chukulia tu hapo badari unadhani panapatikana kiasi gani kwa siku?
Ufisadi ukikomeshwa mambo mengi tu yatafunguka ingawa ni kazi ngumu sana.
Cha muhimu nikuona ahadi zake zitafika wapi. Ndio maana siasa si kama mpira ukiwa simba basi utakua simba milele hata kama wachezaji wakihama lakini siasa ni kitu kingine, Sera ndio zinazo fuatwa kama zinatekelezwa na pia kuangali uchapakizi wa huyo mtoa sera. Binafsi Magufuli nimemkubali lakini ningependa kuona viti vingi vya upinzani hapo bungeni.
Hapo nime mention short term na long term solutions kwa faida ya wengine.Ila naomba tumuachie,kwa kuwa sisi hatuko kwenye chungu.Ila nikuhakishishie kwamba kwenye short term solutions peke yake tutapata pesa nzuri tu.
Hata hivyo labda na washauri wake walipo-spread costs over four quaters,wameona they can manage with what they will get and what they have, kwa kuwa tunatumia a quarter system, hulipi kila kitu mara moja kama nilivyo kwisha sema.
Rais ana nia nzuri,lets be patient and see what he can do.At most tumtie moyo.
kuna watu hawana kumbukumbu kabisa, sijui akili yao ikoje? mara hii mmesahau kuwa bajeti ya 2015/16 wizara ya elimu ilisema shule ya msingi hadi sekondari bure? rejea kwenye kumbukumbu za bunge na wizara ya elimu utapata majibu yote hayo.
Si ameshafuta Safari zote za nje! Makongamano! Think this despot J kikwete used 50 million USD by only himself plying the world; doing his business! The money is enough to educate our boys and girls!!
By the way Mr. JPM remove this ambassador at the Beijing Embassy!
kuna watu hawana kumbukumbu kabisa, sijui akili yao ikoje? mara hii mmesahau kuwa bajeti ya 2015/16 wizara ya elimu ilisema shule ya msingi hadi sekondari bure? rejea kwenye kumbukumbu za bunge na wizara ya elimu utapata majibu yote hayo.
Ame dist111 Rolandi BabuM hoja kuu hapa siyo wapi zitoka hizo hela bali mfumo wa kiserikali (Kama utafuatwa) fedha zote zinazotumika zinatakiwa ziwe zimepitishwa na Bunge wakati wa kikao chake cha Bajeti. Sasa kwenye Bunge la bajeti lililopita lilipitisha na bajeti hiyo ya kulipia ada wanafunzi watakao kuwa wanaingia kidato cha kwanza?
Mkuu acha dharau unauliza fedha zinatoka wapi??????!!!!!!! Serikali ina vyanzo vingi vya pesa tofauti na tunavyoelewa sisi kwa hiyo kitu cha msingi hapo ni kupokea utekelezaji wa ahadi zake na usihoji fedha imetoka wapi unadhani itakuwa imetoka wapi?????? Wakati wa kampeni alijua fedha zitatoka wapi na ndiyo maana alisema, Yule wa mazingaombwe ya kumaliza matembe nchi nzima naye alijua atapata wapi wakandarasi wa kujenga na kulipwa ili kumaliza matembe yote jamhuri nzima ya Tanzania. Ushauri wangu tumhoji anaposhindwa kutekeleza ahadi na tusihoji anapotimiza ahadi.
Nchi ya bila kuhoji si nchi ya Kidemokrasia. Tunatambua Serikali ina vyanzo vingi na hivyo vyanzo vilishapangiwa matumizi na Bunge tukufu la JMT. Wakati wa Kampeni si wakati wa utekelezaji. Kutekeleza ni suala jema, atuambie anatoa hizo fedha kwenye mipango ipi? Na kama anasema anatoa kwenye kubana matumizi atuambie atabana matumizi kwa kiasi na kiasi gani kitapatikana. Lakini kumbuka kuandaa mfumo wa makusanyo na kusambaza pesa kwenye shule zote ndani ya miezi miwili, inawezekana? Halafu deni lililoachwa na watangulizi wake si deni la familia za watangulizi bali ni deni la Watanzania. Lazima tulipe ili tuweze kukopesheka. Tunazitengenezea shule matatizo ifikapo mwezi January.
Mkuu shule haiwezi kuendeshwa kwa ada ya 20, 000/= hata kama zitalipwa kama unavyotaka, bado serikali ilikuwa inatuma fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shule kama huamini naomba umuulize headmaster wa shule iliyoko jirani yako hasa yule mwenye ndevu nyingi atakupa ufafanuzi A level nako ilkuwa 70,000/= lakini michango kibao kwahiyo ada itafutwa michango iko palepale ambayo kwa mwanafunzi wa A level inafikia laki sita mpaka saba upo hapo???? Kama hilo hulijui tuulize sisi tunaosomesha tutakuambia na mfano wa hiyo shule nenda SENGEREMA SEC SCHOOL HUO NI MFANO WA SHULE ZOTE ZA SERIKALI ADA NI NDOGO SANA ILA MAHITAJI YA MWANAFUNZI UTAKOMA NI BORA ULIPE ADA MAHITAJI YA MWANAFUNZI WAKULIPIE.
Mkuu why balozi wa Beijing hahhh? Anakula raha hatumikii wanaomlipa mshahara au?Si ameshafuta Safari zote za nje! Makongamano! Think this despot J kikwete used 50 million USD by only himself plying the world; doing his business! The money is enough to educate our boys and girls!!
By the way Mr. JPM remove this ambassador at the Beijing Embassy!