Magufuli ni kama Mwalimu Nyerere

Magufuli ni kama Mwalimu Nyerere

upo sahihi mtoa post.
rais wetu hana longolongo
nimempenda sana japo sikupiga kura.
Kuna sura zipo serikalini kiurithiurithi halafu majivuno kibao hakuna maendeleo yoyote.
Mwaka huu wataisoma
 
Nashauri Pombe angeanza kujenga ile Mahakama ya kushughulikia Mafisadi na Majizi kama alivyoahidi mara kwa mara.
 
Kuanza ameisha anza, napenda aendelee na majukumu yake na kuipeleka nchi yetu kwenye Neema na hata ifikapo siku zake 100 za kwanza shilingi ipande thamani
 
Nashauri Pombe angeanza kujenga ile Mahakama ya kushughulikia jMafisadi na Majizi kama alivyoahidi mara kwa mara.
kwani mahakama zilizopo hazijitoshelezi?
Kama uhalifu umetokea ni kuripot polise wahalifu hao wakamatwe wafunguliwe mashtaka ushahidi upelekwe mahakamani then hukumu itolewe.
Mahakama zipo Tu.hilo akitaka hata Leo issue ni je ushahidi upo? Au ataanzisha mahakama mpya isiyotumia ushahidi kutoa hukumu?
Mijizi ilijipanga haijaacha trace za ushahidi wowote na ndo maana huwa inajivuna eti ishtakiwe
 
watanzania ni watu wa kujisahau sana na kupenda kua na imani kubwa sana kwa vitu ambavyo kiuhalisia havihitaji kua na imani iliyopitiliza.Si vibaya kuamini hisia zako ila ni vizuri kua na kiasi na kamwe usiruhusu hisia zikaitawala akili.Naamini bado tunao muda wa kumpima raisi wetu na kumuombea pia atimize aliyoahidi kinyume na hapo tutabaki pale pale na Uhuru wetu ni miaka 54 sasa
 
Ni kama kachukua nchi mkononi mwa mkoloni
Tunaanza upya kuijenga nchi

Nasikia RAISI Wetu hapendi upendeleo Wa familia
Hata mtoto wake anasoma Shule ya kata.
Hili nitaamini Tu endapo yule February
Atapigwa chini kwenye uwaziri.kwanini yule jamaa ni WAZIRI?
Raisi amesema hachanganyi serikali na siasa.Namuombea kwa mungu approve hapo kwa kuanzia na hyo jamaa.
Wewe unapenda aanzie wapi?

cc FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
akiendelea na staili hii...basi upinzani wana kazi sana uchaguzi ujao...

hata waliokata tamaa wanaanza kuona mwangaza wa nchi yao
Hata hivyo ngoja tusubiri baraza jipya la mawaziri ndipo tutakapopata picha halisi kama kweli Nyerere na Sokoine 'wamefufuka' au bado tunaendeleza kwa vitendo kale ka-slogan kanakosema CCM NI ILE ILE na CCM INA WENYEWE na hao wenyewe ni watawala wetu na familia zao.
 
Nashauri Pombe angeanza kujenga ile Mahakama ya kushughulikia Mafisadi na Majizi kama alivyoahidi mara kwa mara.
Na watu wa kwanza kutinga kwenye mahakama hiyo wawe wale jamaa waliobeba manoti ya shilingi bilioni 73 za Escrow, kwenye viroba na magunia ya lumbesa pale Stanbic na kuyapakiza kwenye malori bila kuguswa na chombo chochote cha usalama hapa nchini.
 
Mh.Rais......mimi binafsi sipendi hawa waweko kwenye baraza lako la mawaziri; Mwingulu..arudi CCM ajiandae kumrithi Kinana.
Makamba..arudi CCM achukuwe nafasi ya Nape.
Prof Muhongo..huyu angekuwa Katibu mkuu wa waizara ya Nishati madini na Maji.atoke ubunge afanye kazi stahiki.anafaa saana huko kuliko kwenye siasa
Lukuvi...aliharibu hali ya hewa wakati wa bunge la katiba.Watu bado wanayo moyoni aliyoyasema.
Hawa Ghasia,Ummy Mwalimu na Angela Kairuki wabakai ubunge tu.
 
Nashauri Pombe angeanza kujenga ile Mahakama ya kushughulikia Mafisadi na Majizi kama alivyoahidi mara kwa mara.
Hata hivyo kuanzisha mahakama maalum za mafisadi sidhani kama lina umuhimu sana.
Cha muhimu kuliko jambo lolote ni watawala wetu kuwa na utashi wa kuweza kuwashughulikia wale wote 'wanaokwapua' rasilimali zetu.
Hebu tujiulize swali moja tu jepesi, kwani Basil Mramba na Daniel Yona walifungwa jela na mahakama za ufisadi?
Kiuhalisia ingawa mashitaka yao yalikuwa ya uhujumu nchini ambayo inaangukia kwenye kesi ya mafisadi, bado tuliwaona wakihukumiwa na mahakama ya kawaida ya pale Kisutu.
Kwa hiyo tatizo kubwa ninaloliona hapa nchini ni kutokana na mfumo wetu wa kisheria kuweka ulazima wa majalada yote ya ufisadi baada ya uchunguzi kupelekwa kwa DPP ambaye ni yeye pekee hapa nchini mwenye mamlaka ya kumfungulia mashitaka mtuhumiwa yeyote wa ufisadi.
Kutokana na mazingara hayo hata zitaundwa mahakama za ufisadi, kama tutaendelea na mtindo wa hivi sasa kumfanya DPP kuwa ndiye 'chujio' basi tutaendelea kuona vijadagaa pekee wakifikishwa kwenye mahakama hizo za ufisadi na wale mafisadi mapapa tutaendelea kuwaona 'wakitesa' mitaani bila kuguswa na chombo chochote cha usalama hapa nchini.
 
Mh.Rais......mimi binafsi sipendi hawa waweko kwenye baraza lako la mawaziri; Mwingulu..arudi CCM ajiandae kumrithi Kinana.
Makamba..arudi CCM achukuwe nafasi ya Nape.
Prof Muhongo..huyu angekuwa Katibu mkuu wa waizara ya Nishati madini na Maji.atoke ubunge afanye kazi stahiki.anafaa saana huko kuliko kwenye siasa
Lukuvi...aliharibu hali ya hewa wakati wa bunge la katiba.Watu bado wanayo moyoni aliyoyasema.
Hawa Ghasia,Ummy Mwalimu na Angela Kairuki wabakai ubunge tu.

ni kwabahati mbaya wachapakazi huwapendi lakin hakuna namna mwingulu ni Wazir wa fedha, muhongo nishat na madin
 
ni kwabahati mbaya wachapakazi huwapendi lakin hakuna namna mwingulu ni Wazir wa fedha, muhongo nishat na madin

Niheshimu mawazo yako.Niko tayari kurekebishwa...huku kwetu naona katibu mkuu ndiyo mtendaji na asatahili kuwa mtaalamu kwenye hiyo wizara.Uwaziri ni political figure....Hebu angalia hapo kenya.haya mazoea tuyaache..tuwatumie wajuzi kwenye fani zao..Dr Tulia ...mfano mzuri
 
Ni kama kachukua nchi mkononi mwa mkoloni
Tunaanza upya kuijenga nchi

Nasikia RAISI Wetu hapendi upendeleo Wa familia
Hata mtoto wake anasoma Shule ya kata.
Hili nitaamini Tu endapo yule February
Atapigwa chini kwenye uwaziri.kwanini yule jamaa ni WAZIRI?
Raisi amesema hachanganyi serikali na siasa.Namuombea kwa mungu approve hapo kwa kuanzia na hyo jamaa.
Wewe unapenda aanzie wapi?

Mkuu, utaniwia radhi kama nimeelewa vibaya...kwani huyo kijana kama anafanya kazi vizuri kuna tatizo gani??..hatuwezi kumnyima mtu cheo kama sifa anazo eti kwasababu baba yake alikuwa mtu fulani!!
 
Back
Top Bottom