Magufuli ni kama Mwalimu Nyerere

Magufuli ni kama Mwalimu Nyerere

Robethn

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
2,103
Reaction score
354
Watanzania wamehusisha uwezo binafsi alionao mgombea nafasi ya urais kupitia CCM ,kuwa sambamba na wa mwalimu Nyerere kutokana na wote hao kuvunja rekodi za kiutendaji kila sekta waliyopata ongoza.

Hata hivo wote wanasifa za kukemea ufisadi, udini, ukabila na ukanda. Mwalimu Nyerere alichukia sana watu wabinafsi wanaotanguliza udini na ukanda,alichukia watu wente tamaa na kulilia uongozi.

Utendaji na uwezo wa kifikra wa Dr Magufuli umefananishwa kwa kiasi kilubwa na wa mwalimu.
 
unakemea ufisadi na huku unamnadi chenge kama shujaa?
 
Ccm ya leo hakuna wa kumfananisha na nyerere.nani atajali watoto wa masikini wanywe japo uji wa dona shuleni primary wchool.leo migodi kibao.ccm haijali.zaidi kundi kubwa la vijana wanata madawa ya kulevya.
 
mwalimu nyerere aliuza nyumba za serikali??

mwalimu nyerere alifisadi mabillion kwenye wizara ya ujenzi kwa mujibu ya CAG?
 
Magufulia akemea rushwa, udini, ukanda na tamaa ya madaraka kama alivokuwa mwalimu.Jiulizeni huko ukiwa hali ipoje? Kama tu mmeshindwa kugawana majibo,udiwani kesho serikali ndo mtaweza, hampo serious
 
Magufuli ni nyerere wa leo kwa manufaa yangu mimi na wewe,sote tumeona mambo mengi na makubwa aliyoyafanya katika wizara zote alizosimamia,matunda yake sote tunayaona
 
Mtaanza kumfananisha Magufuli na mitume na manabii.

How pathetic.
 
Nadhani tufanye uchambuzi wa kina kuhusu magufuli kabla ya kuja humu jf na kuchangia mada kwakuwa nikitazama ukweli ni kwamba hakuna wakumfananisha na magufuli katika wagombea wote wa kiti cha urais,tuwe wakweli tuache siasa jamani,hivi ninani mchapakazi kama maguFuli,kiongozi aliyeonyesha mfano kwa utendaji mahiri,kiongozi mwenye haiba ya kuongoza,kiongozi anayekubalika na makundi yote ya watanzania,kiongozi anayejua na anayeweza kutuvusha kuelekea nchi ya asali na maziwa,kiongozi tuliyepewa zawadi na mwenyezi mungu, tunataka nini watanzania zaidi ya magufuli,hii ni neema tumepewa kiongozi mwadilifu na mzalendo tumpe nafasi atuvushe kukafurahie nchi ya asali na maziwa, du natumaini hatuhitaji kuongozwa na mafisadi watu wenye uchu wa madaraka kama hawa ukwaaa.
 
Watanzania wamehusisha uwezo binafsi alionao mgombea nafasi ya urais kupitia CCM ,kuwa sambamba na wa mwalimu Nyerere kutokana na wote hao kuvunja rekodi za kiutendaji kila sekta waliyopata ongoza. Hata hivo wote wanasifa za kukemea ufisadi, udini, ukabila na ukanda.Mwalimu Nyerere alichukia sana watu wabinafsi wanaotanguliza udini na ukanda,alichukia watu wente tamaa na kulilia uongozi. Utendaji na uwezo wa kifikra wa Dr Magufuli umefananishwa kwa kiasi kilubwa na wa mwalimu.

Wewe wacha kumvunjia marehemu baba wa taifa heshima,huwezi kumlinganisha Mwl jk na huyo fisadi nakukanya husirudie tena swaini
 
Nyerere alijulikana anasimamia nini hata kabla wakoloni hawjamuachia taifa. huyu mwingine kaibuka hatujui anasimamia nini hadi alivyopewa daftari la ilani.
 
Wewe ndo umetumwa na usiowajua pia hujitambui. Dr. Magufuli hakamatiki

Teeeeeh,teeeeeh,eti hakamatiki?atakamatwa kupelekwa kwa pilato kwa kununua kivuko cha MV dsm kwa bei mbaya
 
Watanzania wamehusisha uwezo binafsi alionao mgombea nafasi ya urais kupitia CCM ,kuwa sambamba na wa mwalimu Nyerere kutokana na wote hao kuvunja rekodi za kiutendaji kila sekta waliyopata ongoza. Hata hivo wote wanasifa za kukemea ufisadi, udini, ukabila na ukanda.Mwalimu Nyerere alichukia sana watu wabinafsi wanaotanguliza udini na ukanda,alichukia watu wente tamaa na kulilia uongozi. Utendaji na uwezo wa kifikra wa Dr Magufuli umefananishwa kwa kiasi kilubwa na wa mwalimu.

Nyerere aliwachukia sana wauza nyumba za serikali kwa wasiohusika
 
Magufuli ni nyerere wa leo kwa manufaa yangu mimi na wewe,sote tumeona mambo mengi na makubwa aliyoyafanya katika wizara zote alizosimamia,matunda yake sote tunayaona

Wewe nenda kashindie mihogo yako ya kuchoma ukabebe zege
 
Watanzania wamehusisha uwezo binafsi alionao mgombea nafasi ya urais kupitia CCM ,kuwa sambamba na wa mwalimu Nyerere kutokana na wote hao kuvunja rekodi za kiutendaji kila sekta waliyopata ongoza. Hata hivo wote wanasifa za kukemea ufisadi, udini, ukabila na ukanda.Mwalimu Nyerere alichukia sana watu wabinafsi wanaotanguliza udini na ukanda,alichukia watu wente tamaa na kulilia uongozi. Utendaji na uwezo wa kifikra wa Dr Magufuli umefananishwa kwa kiasi kilubwa na wa mwalimu.

Magufuli hana sifa ya kuwa hata katibu kata kutokana na silika za udikteta alizonazo. Si mtu anayezingatia sheria, haki za binadamu na wala hana karama ya kuwa msikivu (listening skills) ambayo ni moja ya sifa za kiongozi. Ni mshiriki wa dili za ufisadi zilizofanyika ndani ya miongo miwili aliyokuwa waziri ndani ya serikali mbali mbali za ccm hadi sasa.

Mwalimu Nyerere asingeweza kukaa karibu na uchafu wa EPA, MEREMETA, RADA, NETGROUP SOLUTION, UUZWAJI WA NBC, UUZWAJI WA MIGODI YETU KWA BEI YA KUTUPA KWA WAWEKEZAJI, FAMILIA YA UKAPA KUJIMILIKISHA MAJUMBA YA SHIRIKA LA POSTA NA SIMU, UUZWAJI NA KUJIMILIKISHA VIWANJA NA MAJENGO YA SERIKALI, ESCROW N.K
 
Nadhani hata yesu akirudi leo na mtume muhammad wakaulizwa nani anafaa kuongoza tanzania hawawezi kutuchagulia ukwaa kwa sababu wataleta uharibifu katika nchi kwani dalili tumeziona kwa matendo na maneno yao ya hadaa hivi kweli unaweza ukachagua ukawa watuongoze,ukifanya hivyo hata manabii isa na na muhamaad watatushangaa,tusidanganywe na mafisadi wa ukawa wanatafuta namna ya kuongeza ultajiri wao waliojilimbikizia kwa njia haramu badala ya kuwatumikia watanzania,hatudanganyiki,chaguo letu ni magufuli hapa kazi tu
 
Mwalimu Ñî Mwalimu , magufuli Ñî magufuli. Watu wawili tofauti.

Kwa utumishi uliotukuka wa Mwalimu, magufuli hatoweza kuufikia hata atakaporudi mwana wa adam.

Ccm haina jipya.
 
Back
Top Bottom