Magufuli na ndege, siri nyuma ya pazia?

Magufuli na ndege, siri nyuma ya pazia?

Raisi ana mshahara Na marupurupu ya mamilioni ya shilingi kila mwezi, Na ana kiinua mgongo Na pension ya mabilioni, yet analishwa, kuvishwa, kutibiwa, Na kulazwa kwa kodi ya watanzania Na familia yake yote kwa maisha yake yote. Sina hakika kama anajua kuna watu wana shida!
Hajui kabisa, wala haelewi.

Wala hajui nini nchi inataka.
 
Fedha alizozitumia kununua ndege angezitumia kujengwa daraja la kigongo busisi linalounganisha mkoa wa mwanza na Geita lingekuwa na faida kubwa kuliko hizo ndege na ungekuwa tayari alisharudisha fedha zake mapema. Ila ashauriki na hajui aanzie wapi na aishie wapi. Hata akichaguliwa Tena SGR kwa kipindi Cha miaka mitano itakuwa haijafika mwanza kutokea dar. Utakuwa mradi kiporo. Bila katiba mpya anakusumbua yote anayoyafanya CCM utakuja kuviuza Tena na kuvitapanya upya
 
Sisi kwetu ukipata hela jambo la mwanzo ni kujenga nyumba ya ghorofa. Hiyo iko akilini tokea utotoni. Labda kwa yeye aliweka akilini akipata uwezo atanunuwa ndege.

Ukienda upande wa pili wa sarafu, kuna ukweli katika manunuzi, "the bigger the spending the bigger the commission" I hope you have gotten my gist!
 
kwan umelazimishwa c ukamchague chiba atakuwa anawagawia hela mitaan
 
Masuala ya afya na maji ni masuala ya lazima sio ahadi.. yeye anaongelea ya ahadi
 
Mkuu labda kama haufatilii mada za ndege au miradi ya magufuli,tulishaeleza sana humu,miradi mingi ya JIWE ni ya kupiga pesa kwa mfano hizo ndege anakula cha juu karibu 40% inaenda kwakwe ,terrible teen tulinunua kwa usd 200m wakati bei halisi ni sd 98m kwahio kaweka kibindoni 102m USD ,kwenye hiyo miradi JIWE ndio anapiga pesa ndio maana kutwa kufanya miradi mikubwa ambayo kwasasa sio hata kipaumbele chetu....Midege yenyewe hasara tupu.
 
Raisi ana mshahara Na marupurupu ya mamilioni ya shilingi kila mwezi, Na ana kiinua mgongo Na pension ya mabilioni, yet analishwa, kuvishwa, kutibiwa, Na kulazwa kwa kodi ya watanzania Na familia yake yote kwa maisha yake yote. Sina hakika kama anajua kuna watu wana shida!
Tatizo wapiga kura wengi hawajui wanataka nini zaidi ya ushabiki tu wa vyama
FB_IMG_15980951277964266.jpg
 
Fedha alizozitumia kununua ndege angezitumia kujengwa daraja la kigongo busisi linalounganisha mkoa wa mwanza na Geita lingekuwa na faida kubwa kuliko hizo ndege na ungekuwa tayari alisharudisha fedha zake mapema. Ila ashauriki na hajui aanzie wapi na aishie wapi. Hata akichaguliwa Tena SGR kwa kipindi Cha miaka mitano itakuwa haijafika mwanza kutokea dar. Utakuwa mradi kiporo. Bila katiba mpya anakusumbua yote anayoyafanya CCM utakuja kuviuza Tena na kuvitapanya upya

ndege zitanunuliwa na hilo daraja litajengwa, unalingine?
 
Raisi ana mshahara Na marupurupu ya mamilioni ya shilingi kila mwezi, Na ana kiinua mgongo Na pension ya mabilioni, yet analishwa, kuvishwa, kutibiwa, Na kulazwa kwa kodi ya watanzania Na familia yake yote kwa maisha yake yote. Sina hakika kama anajua kuna watu wana shida!
Kuna jamaa kule Geita walimwambia Magu "baba njaa kali".

Nae akawajibu mnataka mimi nije kuwapikia?
 
Haina shida mchagueni Lisu na akipata huo uraisi mwambieni jambo la kwanza auze ndege zote alizo nunua Magu

Pia nilikuwa sijui kama ndege sio chanzo cha kuongeza ajira nchini
 
Kwani hizo ndege zinjiendesha zenyewehazina watu ndani?
Zikikubebea mizigo yako kwenda nje ya nchi sio ajira?
 
ndege zitanunuliwa na hilo daraja litajengwa, unalingine?
Kingine Ni kujengwa kwa kiwango Cha lami barabara kutoka Geita mjini, kupitia nyarugusu kwenda kahama mjini, barabara kutoka katoro kwenda ushirombo, barabara kutoka Geita mjini kwenda nzera , Barabara kutoka Geita kwenda bulhyankulu kutokea kahama mjini,barabara kutoka sengerema kupitia ntobo kwenda nyangwale kutokea kahama, barabara kutoka nzera kwenda sengerema , barabara kutoka bulyankyulu kwenda msasi kutokea misungwi, Kijiji Cha Kamwanga kilichopo mjini geita kupatiwa barabara ya moramu ,maji na nishati ya umeme.
 
Katika vipaumbele vyote vya taifa, je, ndege ndicho hasa watanzania wanachohitaji?

Hizi ndege za magufuli zina malengo ya dhati ya kuinua maisha ya watanzania ama kuna ajenda nyingine isiyojulikana?

Watu wetu wanalia na umasikini, ajira, mifuko ya hifadhi ya jamii, mikopo, afya, maji, umeme, makazi duni, elimu duni, kilimo duni, mishahara kiduchu na mengine mengi, hayo yote hayana umuhimu kwake isipokuwa ndege tu?

Tunahitaji sera za magufuli ziguse watu. Miaka sita sasa ajira hakuna vijana wanahangaika tu mitaani kama yatima lakini yeye hana habari. Ati nendeni mkajiajiri!

Hizo ndege zina msaada gani kama haziweza kuinua maisha ya watu?? au ni kutafuta ujiko tu na kulimbuka?
Mbona watu wanaajiriwa kila siku? Kuna kazi za Dr. zimetangazwa kaombe mkuu kama ulisomea Udakitari.
 
Kuongoza nchi si jambo rahisi hata kidogo.
 
Back
Top Bottom