Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Magufuli na Muhongo, hii sio confusion?

Haya sio mapya hata awamu ya 4 yalikuwa hivi hivi! Mwingine alisema hakuna haja ya katib mpya, mkuu wa kaya akaja akasema kuna haja ya katiba mpya! Kama rais kwanini usimwite waziri husika ukamwambia akabatilishe kauli yake kuliko kujitokeza kwa wananchi na kumpinga!
Magufuli haelewi "collective responsibility". Yeye anachojua ni "serikali ya Magufuli".
 
Mkuu Nguruvi3 bora wewe umetusaidia kuorodhesha madudu haya ya Muhongo
ndani ya siku 100 tu

kinachoshangaza ni kuona why Magufuli hamuondoi haraka?

Amesema amemteua kwa sababu mnamsema sana,wakati Muongo ni Tractor lake.Haoni mabaya kwa aliowachagua.Narudia usemi wa jamaa mmoja kwamba ni RAHISI kumfukuza aliyeteuliwa na mtu mwingine si rahisi kumfukuza uliyemteua
 
Unajua siku Magufuli atakapo badilisha katiba ajiongeze mda kuna watu
watastuka kama vile hawaoni huu mwanzo...
hao mawaziri kina Makamba wanaomsifia kinafiki now huku
wakimsubiri amalize miaka 10 wagombanie kumrithi watabaki mdomo wazi
wakati hili lipo waazi kabisa ukilitazama

Mkuu boss umenifilisi nilichokuwa nataka kusema.Jana nilikuwa mahali natazama mpira katika mazungumzo yetu niligusia hii hoja jamaa wakastuka sana na kuniambia haiwezekani Kikwete,Mkapa & Mwinyi watakuwa wapi.Jibu langu lilikuwa moja tu hao wote hakuna mwenye uwezo wa mwl Nyerere na niliwapa sababu kwanini nafikiri Magufuli anaelekea huko.
Mosi amekuwa akitumia vyombo vya habari sana kila anapofanya maamuzi lakini wakati huo huo amekuwa akifanya kila njia kuwanyima wapinzani nafasi ya kusikilizwa.
Pili Tanzania itakuwa na uchumi wa gas soon ambao utatuletea fedha nyingi na kufungua fura nyingi za kiuchumi nahisi Magufuli atafanya kama alivyofanya Museveni na mafuta ya Uganda.
Tatu waTanzania wengi hawaoni Magufuli anapenda maigizo (sifa za kijinga) na yuko tayari kuvunja sheria na taratibu hii fukuza fukuza imekuwa style yake ambayo sasa Mawaziri ili aonekane anafanya kazi anafukuza rejea Waziri Kariuki anamtimua kiongozi kwenye mkutano mbele ya wanahabari kulikuwa na ugumu gani wa kutumia channel za office.
 
Kama zipo kwa nini rais anahubiri kulia waziri anatenda yake kushoto. Raisi anapiga ndombolo waziri anacheza ngololo!
...Zipo na nimekuwekea uzisome -kwenye maandishi ya blue, bandiko namba 144, ukurasa wa nane wa nyuzi hii- halafu ndio tuendelee kujadiliana. Nikakuuliza kama umezisoma. Nadhani hujazisoma.

...Sasa, inabidi uzisome ili ujue kilichopangwa kufanyika na kinachofanyika. Lakini, nikuhabarishe kidogo, hii nchi inaendeshwa kwa uchumi wa soko na shughuli binafsi za uzalishaji huduma na bidhaa. Serikali inasimamia na kujihusisha kidogo na shughuli hizo.

Hii inadhihirisha Raisi ameona madhifu ya waziri na sera zisizokuwa na maslahi kwa taifa zenye kuwakumbatia madalali na wapiga dili, ndio sababu anakuwa na mtizamo tofauti. Ifike mahala tuwe na uzalendo wa kweli kwa nchi yetu!
...Madhaifu yapi? Pale alimkosoa au alimsifia? Unafahamu vizuri alichoongea, kuhusu Prof. Muhongo?

...Ukizisoma ndio utajua zina au hazina maslahi kwa Taifa. Nakushauri uzisome. Take some few minutes zisome!

...Uzalendo ni vitendo, si maneno! Wazalendo husoma! Zisome utimize jukumu lako kama mzalendo!
 
Lakini, zaidi ya hapo, mh. Raisi anahamasishwa na dhamira yake ya dhati mfano kuweza kushurutisha makusanyo ya kodi, tozo na mapato ya serikali kwa ujumla wake, tena ya ndani kwa mamlaka husika na kupata fedha za kugharamia uwekezaji huo mkubwa.
...Hizo fedha -the current collections- hazitoshi hata kuendesha shughuli za kila siku za Serikali. Achilia mbali kugharamia miradi mikubwa ya uwekezaji.

...Hela ya kodi haitumiki -na wala si lengo lake- katika kugharamia uwekezaji mkubwa! Fedha kwa ajili hiyo hutafutwa toka maeneo mengine ya kupata fedha, kama kuuza hisa maalum za serikali, kukopa, n.k.
 
...Zipo na nimekuwekea uzisome -kwenye maandishi ya blue, bandiko namba 144, ukurasa wa nane wa nyuzi hii- halafu ndio tuendelee kujadiliana. Nikakuuliza kama umezisoma. Nadhani hujazisoma.

...Sasa, inabidi uzisome ili ujue kilichopangwa kufanyika na kinachofanyika. Lakini, nikuhabarishe kidogo, hii nchi inaendeshwa kwa uchumi wa soko na shughuli binafsi za uzalishaji huduma na bidhaa. Serikali inasimamia na kujihusisha kidogo na shughuli hizo.


...Madhaifu yapi? Pale alimkosoa au alimsifia? Unafahamu vizuri alichoongea, kuhusu Prof. Muhongo?

...Ukizisoma ndio utajua zina au hazina maslahi kwa Taifa. Nakushauri uzisome. Take some few minutes zisome!

...Uzalendo ni vitendo, si maneno! Wazalendo husoma! Zisome utimize jukumu lako kama mzalendo!
Ninasikitika sana kusoma mambo yaliyopitwa na wakati na kukosa uhalali timilifu kwa wananchi Hii ni kwa sababu yaliandaliwa kukidhi maslahi ya kikundi cha watu wachache wenye nia mbaya na nchi yetu.
Sote ni mashuhuda wa mambo ya ajabu yanayotia kinyaa katika bunge letu la serikali ya awamu ya nne. Bado kuna watu bado wanataka kumrudisha Mheshiwa Rais kule asikotaka kwa kivuli cha sera mbovu na zisizo na chembe ya uzalendo. Hii inajionyesha kwamba wapo watu kama huyo waziri ambao ni majipu yanayosubiri kutumbuliwa. Bado waziri ana akili ileee ya kukosa uzalendo, kufikiri kwamba serikali ni masikini na inahitaji matapeli.
Hapa tulipo tunahitaji viongozi wenye kufikiri na kukidhi matakwa ya wananchi. Wenye kuangalia jinsi tukavyoweza kujitegemea na kutumia vyema raslimali za nchi. Viongozi kama huyo bwana hawatufai.
 
Pili Tanzania itakuwa na uchumi wa gas soon ambao utatuletea fedha nyingi na kufungua fursa nyingi za kiuchumi nahisi Magufuli atafanya kama alivyofanya Museveni na mafuta ya Uganda.
...Ngongo, kwa rhetoric hizi, wawekezaji wata shy away, na hizo fursa nyingi tutaishia kuziongelea kwenye vikao!

...Tukumbuke, kuna ushindani mkubwa hivi sasa katika eneo hili -indian ocean- kwenye sekta hii. Mozambique tayari wameshaenda hatua kadhaa. Actually, kilichotokea Mozambique kinatuweka katika kona ngumu ya kuingia mikataba yenye faida zaidi. Jamaa watabana kona. I don't know how we will respond to that. Worse enough, we may react!

...We need to send a clear signal, and avoid making noise.
 
Sisi tunahitaji umeme wa uhakika, utapatikana vipi watajua wenyewe.

Hayo mambo ya sera nimeanza kuyasikia tokea mwishoni mwa miaka ya themanini.
Ni muhimu kujua umeme unapatikanaje. Vinginevyo, wapiga dili wanaingizwa kwenye uzalishaji na umeme tunauziwa kwa gharama ambayo ni mara tano ya uhalisia
 
Ninasikitika sana kusoma mambo yaliyopitwa na wakati na kukosa uhalali timilifu kwa wananchi Hii ni kwa sababu yaliandaliwa kukidhi maslahi ya kikundi cha watu wachache wenye nia mbaya na nchi yetu.

...I get it, hujazisoma. Siku njema ndugu!
 
Haha, kuna watu wanaona haya matamko na maagizo ni mapya ...

TANESCO Leo haina hata chuo cha kuzalisha wataalamu wake......
Si kilikuwepo siku za nyuma kikabadilishiwa matumizi? Labda itabidi wajenge kingine.
 
Haya mambo ya serikali na namna inavyopaswa kuwa na kujiendesha ni tatizo kubwa sana, Tusilaumiane tutafute namna nzuri zaidi ya kusaidiana, Nchi inatakiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa, Ni kazi ngumu sana, tusaidiane, tusihukumiane, tunaweza kuitengeneza nchi yetu kama tutashirikiana kwa pamoja na kusaidiana. Magufuli ana maono nadhani kuna tatizo kidogo kwenye kuyatafsiri kwa vitendo - tumsaidie, ndio wajipu wetu kumsaidia kiongozi wetu. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Tatizo la mambo yote hayo limesababishwa na pale nchi ilipoamua kuuza au kubinafsisha viwanda na mashirika yote ya umma. TANESCO ilikaa kwa zaidi ya miaka kumi ikisubiri iuzwe hivyo pakawa hakuna uwekezaji na mambo yote kuwa ya hovyo. Baada ya kuonekana kuwa haiuziki tena ndipo hapo watawala wakaanza kuja na sera za mitambo ya kukodi kwa gharama kubwa na kuliumiza sana shirika mpaka linashindwa namna ya kujikwamua. Kinachotakiwa kwa sasa ni kusonga mbele kwa kufanya uwekezaji mhimu na tuepuke kueudi tulipotoka.
 
Shida ya nchi hii iko hapo
mtu hana team ya wataalam na kama anayo haisikilizi

Sasa Magufuli hotuba tu ya kuandikiwa haisomi
anazungumza yake...jiulize team ya washauri ya uchumi ataisikiliza?

nimewahi toa mfano humu
Makamu wa Rais wa Marekani sio mtendaji..hafanyi maamuzi
lakini still ana washauri wa kila sekta
unakuta Makamu wa Rais ana mshauri wa uchumi...
Rais ana mshauri wa uchumi na kuna mawaziri husika nao wana washauri...

Sisi Rais anaibuka tu na kusema kitu hata washauri hawana taarifa nacho

Yes, you are right mkuu.

Na labda mimi nitofautiane kidogo na wachangiaji wengi humu.

Nionavyo mimi tatizo liko kwa Mr President na sio kwa waziri wake. Sema tu kwa sbb yeye ndiye mkubwa na ile dhana ya "the boss is always right" ndiyo tatizo.

Muhongo ukiachilia mbali udhaifu wake ule mwingine wa kimaadili (rejea skandali la Tegeta - Escrow Account) pamoja na chuki za kisiasa, kichwani ni mzima zaidi kuliko Magufuli!!

So long as yeye ni Rais (the boss) na kishatamka in a contradicting way, hakuna namna, a mere minister bila kujali weledi wake ataonekana takataka tu!

Otherwise, mimi Profesa Muhongo namkubali sana. Nakumbuka sana, ktk awamu ya nne aliopokuwa waziri wa hii wizara na kabla hajakutwa na dhahama ya Escrrow scandal, upatikanaji wa nishati ya umeme ulikuwa bora kabisa (sijui alikuwa anafanya nini)

Alipoondoka tu, scarcity ya nishati ya umeme ilirudi kwa kasi hadi leo ni mgawo mtindo mmoja!!!

Vinginevyo tunakubaliana kuwa kwa mparanganyiko huu wa misimamo ya viongozi wa serikali ktk sera zozote zile, hakika ni kuchanganya watu wasijue wanaelekea wapi!

Na pia tukumbuke kauli yoyote ya Rais kiongozi mkuu wa nchi iwe nzuri au mbaya, basi, matokeo ni kumwathiri kila mmoja wetu.

Muhongo is better than Magufuli upstairs. Hakurupuki ktk matendo na kauli zake though ana udhaifu wake.....he's too arrogant sometimes!!
 
Back
Top Bottom