Magufuli kumfilisi Lowassa

Magufuli kumfilisi Lowassa

DSC00825.jpg

Lowassa Kuifilisi ccm ! Ihi imekaa Vizuri Sana.
 
Albart marwa riz na said lugum pamoja na maboss wa home shoping centre said pamoja na gharib wenye ma trilion ya masikini wa tz atawafanyaje?
MAGUFURI HAO HAPO JUU NDIYO WALIOIWEKA FISIEM MIFUKONI KTK KILA SEKTA,UTATHUBUTU KUWAGUSA?teh,teh,teh
 
Ndugu Pasco, nashukuru kwa mchango wako, natambua umeshafanya maamuzi yako ya kumchagua Lowasa na Chadema, hongera kwa kufanya maamuzi. Binafsi sijafanya maamuzi sababu sikurupuki, sina chama, naendelea kuwapima wagombea wote kutokana na vigezo ambavyo nitavianisha hapo chini baadaye:
Sitegemei uanze na mihemko ya CCM out bila kupata vigezo nitakavyojirizisha navyo kwamba ninayemchagua anatosha kuniongoza kwa miaka mitano ijayo.
Lengo la kuanisha muda wa uanachama wangu humu JF ni kuonesha kutoyumbayumba na ushabiki maandazi wa vyama na misimamo kama wewe na wengineo mnavyofanya humu.

Vipimo vyangu;
- Usikivu ( Ntamchagua kiongozi anayesikiliza shida za watanzania, ushauri wa wataalamu na wanasheria)

- Maono(Vision)- Kiongozi anayeitazama Tanzania ya kimaendeleo kwa mikakati inayotekelezeka na ufahamu kwamba maendeleo ni hatua(steps) not an event.

- Afanyaje maamuzi inapobidi(decisiveness).

- Mtatua matatizo( problem solver)- sifa hii inashabihiiana na ya juu hapo.

-Mwaminifu(honesty)- Kiongozi ambaye nikimtazama najiridhisha na uaminifu wake bila shaka yeyote.

-Mbunifu( Creative)

-Mwenye ari na uchu wa kuwainua waTanzania, asiyependa uonevu.

Pamoja na sifa nyingine, hizi kwangu ni muhimu kwa kiongozi nitakayemchagua.

Nilitegemea wewe mwanaUkawa unielimishe kwanini nimchague mgombea wako kwa kutanabaisha mifano na hatua za mgombea wako na sio kunishambulia as if mimi ni mwanaCCM.

Yapo mengi yaliyonivutia Ukawa ilipoanzishwa( Umuhimu wa Katiba mpya), sasa imekuwa ya kina Sumaye, watu ambao mimi binafsi siwaamini; Nina haki ya kuhoji uhalali wake kwenye haya so called Mabadiliko.

Tatizo wana Ukawa hamshauriki kama mgombea wenu; sifa yangu ya kwanza hapo juu ni USIKIVU

Wiki njema ndugu
 
Last edited by a moderator:
Baada ya Lowasa kuapishwa kuwa raisi wa tanzania.
Aliyeuza nyumba za serikali kwa hawara zake ajiandae kwenda segerea.
Ripoti ya CAG mwaka huu inaonyesha upotevu wa bilioni.262 kwenye wizara ya ujenzi waziri husika ajiandae kwenda segerea.
 
NATABIRI CCM itazikwa na MAGUFULI
watu tunamwamin sana MAGUFULI na kihalisia sijui ataanzia wapi kupambana na kinachoitwa ufisadi kwani na yeye ni zao na ana vimeo vyake vya kifisadi.

CHAGUA hashim rungwe au dovutwa kama tunataka mtu wa kupambana na ufisadi na sio hawa wafanya maigizo.
hivi kivuko, nyumba kwa mahawara then ataanzia wapi kumhoji mkapa, mwinyi , jakaya, lowaassa, pinda????
 
Zile billion 1.7 za magufuri zimepatikana?
 
Sikusema hakuna wasiomuunga mkono. Kanda ya ziwa anapendwa sana. Migodi zaidi ya 25 iliyokuwa imechukuliwa imerudishwa kwa wananchi katika awamu hii, ameahidi kuirudisha zaidi na kuwapa wachimbaji wadogo teknolojia ya kuwasaidia katika uchimbaji. Kwetu tunaoujua uchimbaji wa madini hilo ni jambo kubwa kwa mchimbaji wa dhahabu. Ina maana watapata mpaka concentration equipment ambazo unaenda kuipata gold ikiwa nyingi na ikiwa na impurities chache sana baada ya kuprocess ore nyingi tofauti na kutumia karai. Unategema watataka kipi tena?

Miaka 54 yote mlokaa madarakani mbona hamkufanya hayo bado mwataka kudanganya Watz
 
Wuh, thank God kwa kukunyima jicho la ndani, uko sahihi sana unavyoamini, usije ukadanganyika kusikiliza propaganda tofauti na za chama kikuu

Mkuu, tatizo kubwa mlilonalo mnazungumza kwa kutegemea taarifa nyepesi. Jiulize Lowassa ameanza kuchangia lini kwenye Makanisa huku akiwaacha wapiga kura wake wakiwa hawana maji? Angekuwa na fungu la kutosha si angewapatia maji kwanza watu wa Monduli? Badala yake wakati akitoa misaada yenye sura ya kampeni Makanisani amewaacha wakitaabika na ukosefu wa maji mpaka Kikwete alipoyafikisha mwaka jana tu. Bwawa la lekeni limekuwa huko kwa miaka ingapi na yeye amekuwa ofisini kwa muda gani? Hilo ni moja, tangu akiwa CCM amewashinikiza sana wafanyabiashara wa kihindi waichangie kampeni yake ya kuingia ikulu, kama fungu lilikuwa bado lipo angefanya hilo? Badala yake aliwekeza katika nyumba nje ya nchi na biashara zake ambazo zimechukua hela yake nyingi. Kama unamjua vizuri, mtafute mwanae anaeitwa Bob umuulize ni biashara gani ambayo iko sokoni anayoisimamia, kama angekuwa ana pesa asingekuwa ameiweka biashara yake sokoni.
 
Yeye na wenzake mafisadi watafilisiwa. Magufuli yupo siliace na kazi yake.
Kumbe ndio wale wale mjinga ndio m
taji?siliace ndio kitu gani ndugu?go back to school utakuja kujigundua ulikua mtu wa aina gani
 
Miaka 54 yote mlokaa madarakani mbona hamkufanya hayo bado mwataka kudanganya Watz

CCM imefanya mengi ila haimaanishi kuwa hakuna mapungufu, ndio maana kwanza tukamkataa Lowassa kuwa mgombea wetu ili tuubadili mfumo wa kuwa na watu kama yeye, Tukamuweka Magufuli ambae ana rekodi nzuri ya utumishi wenye mafanikio na ambae mpaka sasa ameweka wazi kuwa haridhishwi na utendaji wa waliomtangulia pamoja na kuainisha vipaumbele kadhaa ambavyo ukiviangalia vina kila sababu ya kuleta mabadiliko ya kweli kwetu Watanzania.
Kwa historia yake ilivyo na kwa ushahidi ulio wazi, atatekeleza hayo yote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom