Jagermaster
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 654
- 321
sasa kwa mfano akiwa Rais Magufuli atatuongozaje?
Nchi ilishavulundwa muda mrefu na watendaji wabovu, ili kuweka mambo sawa kwa nchi iliyovulugwa kama hii tunahitaji viongozi wenye vulugu, kwa hili Magufuli anafaa. Watu wanahitaji maamuzi magumu, maamuzi magumu yakianza kutekelezwa tena tunakuwa watu wa kwanza kulalamika. Katika lundo la vigogo wote wanaong'ang'ania kuongoza mzoga huu (Tanzania), at least Pombe ndio anafaa. Mtoa maada umeonyesha bias kwenye topic hii. Kamwe sitaweza support eti Magufuli ajiuzuru kwa kuwa tu anasimamia bomoabomoa au kwa kuwa tu kawaambia watu wapige mbizi. Au kwa kuwa tu maamuzi yake huwa nayapingana na Rais na PM, I don't see any rationality on this , Unless utwambie kuwa hao viongozi walio juu yake ni watendaji wazuri kuliko yeye, then anawavuruga. Lakini kama Magufuli anafanya kwa manufaa ya Tanzania, na akiwa kati ya watu wachache ambao walisomeshwa bure enzi za Mwalimu ili waje walipe fadhira kwa taifa kwa kulitumikia, Magufuri hana haja ya kujiudhuru unless tuaminishwe kuwa JK, PM and others are doing well for this poor nation. Wapo watu wakujizuru wengi tu huko kwenye system wachafu kuliko Magufuli. Kama sheria zilikosewa watu walipwe na nyumba zibomolewe na hayo ndio wanaita maamuzi magumu. Magufuri anahitaji blending ndogo tu ila kazi anaiweza kwa watu wapenda soga kama sisi watanzania.
Katika kipindi hiki mpaka 2015 tutayasikia mengi sana na waandishi uchwara wanaotumia kalamu kuchumia tumbo wataonekana.
Watu kama Magufuli ambao hawajatumia muda wao kisiasa kujijenga Kichama wala hawajishughurishi kuwapa visenti waandishi wa habari ili waandikwe vizuri kwenye magazeti bali kutegemea utendaji wao kujijenga kisiasa wanapata shida sana kwenye mazingira ya Tanzania ambayo yamejaa waandishi wachumia tumbo.
Sasa nimeanza kuamini ni kwa nini Mpaka alimpa ulinzi wa ziada Magufuli, kweli mazingira ya Tanzania yamejaa predetors kwa watu wa aina ya Magufuli. Tunakoenda kazi iko
Kwa mfano kama ni kweli Magufuli alitaka Jengo la TANESCO-UBUNGO libomolewe, ilibidi afikirie kua lile jengo limejengwa kwa pesa yetu na ujenzi uliidhinishwa na Mawaziri husika walikokuwepo kabla yake Magufuli kwenye wizara hiyo. Likibomolewa leo, kesho kuna uwezekano atakuja waziri mwingine anayembadili Magufuli na akaidhinisha ujenzi tena katika sehemu hiyo - sasa utaona kua sisi ndio tunaliwa tokana na maamuzi ya kibabe toka kwa hao mawaziri wa CCM.
Magufuli angetufaa sana kama angesimamia na kuwakaba walioidhinisha ujenzi wa hilo jengo. Pia atatufaa kama atadhibiti ujenzi holela unaoendelea kukua na hapo hapo kupigania raia kupata viwanja vilivyopimwa haraka - bomoa bomoa is too easy kumpa sifa Magufuli. Vilivyofanywa kwa makosa na wenzake kabla yake, basi na waadhibiwe kwanza ili makosa yasirudiwe.
Kimsingi Magufuli si kiongozi mzuri, anafanya mambo kama kuruta - utafikiri amekatazwa kufikiri. Ni kweli tunaweweza kumlaumu magufuli kwa kutaka kubomoa jengo la TANESCO kwa kigezo cha kula hasara walipa kodi wa tanzania. Sasa tujiulize ni kifanyike ili barabara iweze kutanuliwa?
Mkuu ilo unalo dai ni sawa lakini ukumbuke magufuli sio wazimwenye dhamana na hiyo mipango miji au ujenzi holela mwenye dhamana hiyo ni wazili tibaijuka
. Suala la je, anapokuwa hana madaraka yukoje, to me is irrelevant. Kwani kuna mijitu ndani ya serikali ya kifisadi ya ccm imepewa madaraka yote lakini imekaa kimya na kuacha nchi inachezewa kama haina mwenyewe. Kikwete anamweka magufuli madarakani kwa kinyongo.Magufuli bado namfagilia kwa ushupavu wake wa kusimamia sheria kwa vitendo
Anachoogopa ni kunyoshewa vidole na watanzania endapo ataamua kumwacha kwa sababu utendaji wake wa kazi hakuna mtanzania asiyeujua. Aliwahi hata kumtia ndani kiongozi mmoja wa ccm kwa kukutwa na kokolo ya kuvulia samaki kwenye bwawa la nyumba ya Mungu.
Wakati naandika makala ambayo itatoka kwenye gazeti moja la leo kuhusu Magufuli na kwanini hana chaguo jingine lolote isipokuwa kujiuzulu nilijadiliana na ndugu yangu mmoja na tukajikuta tunakabiliwa na swali ambalo hatukuweza kulipatia jibu: Hivi nje ya madaraka Dr. Magufuli anaweza kukumbukwa vipi katika kusimamia sheria nchini na kupigania maslahi ya wananchi?
Hapa sizungumzii mambo ambayo alikuwa anauliza kama mbunge kwa ajili ya jimbo lake tu nazungumzia kitaifa ana jambo lolote ambalo tunaweza kusema alilisimamia kitaifa nje ya yale ambayo amewahi kuyafanya akiwa na madaraka?
Yawezekana ujasiri wa Magufuli hautokani na msimamo au mtazamo uliosahihi bali unatokana na kuwa na madaraka kwamba kwake madaraka na siyo kanuni ya kuongozwa na uadilifu ni chombo kwake cha kutimiza mambo mbalimbali?
Je amewahi kusimama akiwa Mbunge kuhoji na kutaja uwajibikaji wa serikali kwenye jambo gani ambalo lilikuwa na taswira au matokeo ya kitaifa?
Ni wazi kwamba amekuwa Waziri toka wakati wa Mkapa na wakati wote wa Kikwete yawezekana madaraka yamemjengea pazia ambalo ni kwa hilo tu anaweza kuonekana? Je Magufuli bila ya madaraka ni nani? Bila kuwa na cheo - yaani akiwa Mbunge wa kawaida anaweza kupigania sheria isimamiwe Bungeni bila kucompromise? Je akiwa MBunge wa kawaida yuko tayari kubanwa na mawaziri na wabunge wengine?
Katika kujitahidi kupata majibu binafsi nilifikia mahitimisho yafuatayo - mengine nimeandika kwenye makala hiyo:
a. Dr. Magufulu hawezi kuwa mpiganaji wa raslimali za taifa bila ya madaraka. Madaraka ni kinga kwake ya kuweza kufanya mambo mbalimbali.
b. Dr. Magufuli hana historia ya kujivunia ya kujitofautisha kuwa ni mtetezi wa raslimali za wananchi nje ya ofisi yake. Kwa kiasi kikubwa anakumbukwa kwa mamboa ambayo yamemjengea sifa ya kuwa ni "askari wa mwamvuli" wakati wa Mkapa lakini bila kuwa na uwaziri ni mtu ambaye yuko very docile.
Haya mawili yanajibu maswali mawili - kwa uzuri na kwa ubaya:
a. Itakuwa vigumu sana kwa Magufuli kujiuzulu on principle hasa baada ya kutofautiana na RAis na Waziri Mkuu wake na vile vile kwa viongozi hao wawili kuonesha wazi kuwa hawana imani na uwezo, nia na sababu ya maamuzi ya waziri wao. Kwa vile hawezi kukaa bila ya madaraka na kupigania anachoamini ataendelea kuwa waziri na tushangae akiwa mkimya mno kwani alichofanyiwa juzi si kidogo kwa kipimo chochote.
b. Endapo atakuja kutaka kupewa madaraka makubwa zaidi nchini; kuna watu wanaweza kujikuta wanakimbia nchi kwani ni wazi kuwa anaweza kutumia madaraka aliyonayo kufikitia masuluhisho ya mambo kadha wa kadha kuliko baadhi ya viongozi wengine ambao wamebakia kuja na sura za huruma na upole wakikwepa kusimamia sheria.
my two cents plus the other fifty
Mhe John magufuli amekuwa kwenye barza la Mawaziri toka awmu ya kwanza ya Benjamin Mkapa hadi sasa. Ni katika kipindi hicho hicho taifa limeshuhudia wizi na ubadhirifu mkubwa wa raslimali na fedha za taifa ukitekelezwa na viongozi wakuu wa nchi hii k.m RAD, EPA, MEREMETA, TANGOLD, kuuzwa kwa mashirika ya umma kama vile NBC, TTCL n.k kwa be za kutupwa; Seikali ambayo yeye ni mmojawapo kufanya maamuzi kuitia baraza la mawaziri kutengua maelekezo ya Mwalimu Nyerere kuwa madini ya nchi hii hayozi hivyo yasichimbwe hadi pale taifa litakapokuwa limejijengea uwezo wa kunufaika kutokana na raslimali hizo n.k
Kitendo cha Mahe John magufuli kuendelea mpaka leo kuwa mjumbe halali wa baraza la mawaziri kinathibitisha dhahiri kuwa yeye pia ni fisadi na hupiga kura za ndio kuruhusu hujuma zote ziliyotajwa hapo juu dhidi ya watanzania.
Aidha Mhe John Magufuli anayo role yake binafsi katika hujuma ya nyumba za serikali nchi nzima, kwa jinsi alivyotekeleza zoezi hilo na yeye mwenyewe, ndugu hata kufikia mawahara zake kugawiwa nyumba za serikali ni uthibitisho wa ufisadi wake.
Tuangalie kwa ufupi. Huyu bwana alipoingia bungeni ulikuwa wakati wa Msekwa ambapo bunge lilikuwa mhuri tu na haikuwa rahisi sana kujua wapiganaji kwa uwazi hasa ukiwa ndani ya chama. Halafu akawa waziri jambo lililombana zaidi.
Kurudi kwake bungeni tena bila kupingwa ni ishara ya kuwa wapiga kura wake walikubali kazi yake, na hiyo inamjengea hoja kuwa japo si msemaji ni mtendaji. Kama ni kweli au si kweli wananchi wa Chato wanamajibu sahihi.
Kukubalika kwake kunatokana na kufuata kanuni, sheria na mipango.J.P Magufuli ni kiongozi ambaye ametuonyesha mengi yaliyowashinda wenzake.mambo. Anaifahamu vizuri kazi yake na yupo tayari kusimamia sheria zetu wenyewe hata kama ni za kurithi kutoka kwa mkoloni.Kwanfano aliposimamia ujenzi wa bara bara, ile ni sehemu ya kutumia na kuendeleza rasilimali za taifa.Alipotuonyesha kuwa tumelala na watu wanavua samaki karibu na kigamboni alisimamia rasilimali za taifa.
J.P.M anaposema ujenzi haramu ndani ya hifadhi za bara bara anasimamia matumizi ya kile kidogo tulicho nacho kwa manufaa yetu sote,kwa kuzingatia sheria tulizozikubali sisi wenyewe na kumkabidhi azisimamie.
Kitendo cha viongozi wa juu kumsema mbele ya mikutano ni ukiukaji wa kanuni za uwajibikaji wa pamoja 'collective responsibility'. Sijui kama PM au Rais wameshindwa kuwasiliana naye faragha hadi kusimanga hadharani.
Viongozi wanajali kura zaidi na si sheria walizoapa kuzisimamia ' cheap popularity'. Utamaduni uliotufikisha mahali wizi, ubadhirifu na ufujaji ni sehemu ya uongozi.
La kushangaza,ni kitendo cha J.P kutojiuzulu. Kanuni za utawala bora zinasema kunapokuwa na tofauti za mitazamo wazi kiongozi anatakiwa ajiuzulu.
Magufuli anaweza kuwa kiongozi mzuri hata kama si msemaji wa wazi kama
mbunge, sijui anasubiri nini na kama anataka kuwa malaika ndani ya kundi la wahalifu.
Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.
Uzuri mmoja wa Maghufuli ni usimamizi wa sheria na maamuzi halali bila kuangalia makunyanzi ya yeyote. Sifa hii wanasiasa wengi hasa wa kuchaguliwa hawana. Analo tatizo la kutopima na kuona usahihi, uhalali na tija ya baadhi ya maamuzi kwa mfano Cabinet ya Mkapa ilipoamua wajiuzie nyumba na viwanja vya serikali.sasa kwa mfano akiwa Rais Magufuli atatuongozaje?
Naomba utaje hiyo sheria anayoisimamia ili tuijadili badala ya kutaja mambo kwa ujumla wakeUzuri mmoja wa Maghufuli ni usimamizi wa sheria
.na maamuzi halali bila kuangalia makunyanzi ya yeyote. Sifa hii wanasiasa wengi hasa wa kuchaguliwa hawana. Analo tatizo la kutopima na kuona usahihi, uhalali na tija ya baadhi ya maamuzi kwa mfano Cabinet ya Mkapa ilipoamua wajiuzie nyumba na viwanja vya serikali.
Kinachonifurahisha kwa masikitiko ni pale unapokuta waliomkoromea magufuli wanajulikana kwa kukosa meno na nguvu kiasi cha kuwa bendera ambayo hutikiswa hata na pumzi badala ya upepo! Mifano ipo mingi hasa kwenye epa,meremeta, kagoda, na hivi karibuni tuzo ya dowans ambapo tumewashuhudia watawala wakubwa kabisa wakigeuka kuwa bendera.
Anazitaja mara kwa mara kwa kila maamuzi anayofanya kama waziri mwenye dhamana ikiwemo hii ya kupandisha nauli ya feri. Alifuata taratibu zote.Naomba utaje hiyo sheria anayoisimamia ili tuijadili badala ya kutaja mambo kwa ujumla wake
Anazitaja mara kwa mara kwa kila maamuzi anayofanya kama waziri mwenye dhamana ikiwemo hii ya kupandisha nauli ya feri. Alifuata taratibu zote.
Kila anapozitaja sote tunasikia. Mimi huzitafuta na kuzisoma pia. Hakuna anakopindisha. Vinginevyo angenasa siku nyingi Bungeni ambako UONGO ni mwiko na unajua ana maadui wengi tu hasa ndani ya CCM, BUNGENI na serikalini kwa utendaji wake ambao wengi mnadhani anausaka URAIS. Acheni Maghufuli afanye kazi. Urais utakuja wenyewe. Hautafuti kama baadhi yenu.kwa hiyo unashabikia kitu blindly bila ya kujua hizo sheria zinasemaje, kwa taarifa yako Magufuli natumia sheria feki na hupindisha sheria to serve his purpose. Ndio maan wakubwa wake walimkemea kuacha ubabe. Ni vyema ukitaka kuzungumza mbele ya watu jielimishe kwanza hizo sheria ndipo huzitaje mbele ya watu.